Rayns
JF-Expert Member
- Jul 29, 2023
- 3,552
- 7,723
Habari za wakati huu wote,
Leo Ningependa kushare nanyi hili tukio ambalo lilinitokea, na sio zuri kuliendekeza kwa wale wanaofanya. Nimejikuta nakumbuka mojawapo ya DHARAU kubwa sana kuwahi kufanyiwa.
Kwanza kabisa niseme kuna watu tunadharaulika, nilifananishwa na bulb (Taa), au Mbu wale wanaoeneza na Malaria! Iko hivi...
Mwaka jana mwezi wa 9 nilienda kumtembelea brother angu mmoja hivi alisoma shule ya msingi niliyosoma mimi. Yeye alikuwa mbele maana nilipokuwa darasa 2 yeye alikuwa darasa 7 na alikuwa mwenye akili sana darasani kwao, alikuwa akishika namba 1 kila mitihani. Alikuwa anapenda sana kukaa na madogo kuliko vijana wa rika lake.
Wakati naenda kumtembelea yeye hakuwepo lakini alinambia atarudi baada ya siku mbili alisafiri kidogo, akasema nitapokelewa na mshikaji ambae alikuwa akifanya nae kazi ofsini walikuwa wanaishi wote.
Nilifika Mida ya saa nane mchana hivi, na yule jamaa akanipokea fresh tu, yule jamaa niliemkuta pale alikuwa ananizidi miaka kama 5 au 6 hivi na yeye alikuwa analingana umri na yule brother kwa kuwaangalia.
Siku hiyo jioni tukaenda kutembea kidogo, sasa mimi sio mtu wa madem na sipendi kabisa. Siku hiyo tumetoka kuzurura mtaan kidogo alikuw anachatchat kwenye simu yake, akanambia kuna mtu anaenda kutana nae, nikamuuliza ni nani akasema ni dem wake, nikamwambia fresh lakini akifika me ntawapisha kidogo muongee, akasema tutatembea na huyo dem kwenda mtaa wetu kisha tutamrudisha tena mtaa wa pili ambako huyo Dem alikuwa akikaa huko.
Sasa mimi nilikuwa muoga sana sana yaani siwezi kabisa kuongea na msichana siwezi, nikasema hapa sasa si ntakuwa mpenzi msikilizaji wa maongezi ya watu. Nikamwambia bro mimi Siwezagi kuongea mbele ya madem siwezi kabisa, sasa akija me ntawasikiliza tu, na yule dem ataniona je? Hata kama ni dem wako ila natakiwa niwe nachangia mada kidogo.
Akasema utajitahidi hivo hivo, basi tumetembea tunapiga stori kuelekea ule mtaa wa pili kwa yule dem, dem tukamkuta mitaa fulan kapiga pamba kali sana na alipendeza kwakweli. Nikamsalimia tu pale alikuwa mchangamfu, baada ya salamu nikauchuna kama kawaida yangu kimyaaa.
Wakati tunatembea tembea mtaani, nikapata wazo nijifanye kununua kijuice ili muda uende, ni aibu sana kutembea na jamaa akiwa na dem wake alafu wewe unawafuatafuata kama bodyguard.
Nikawaambia, me napendag sana kunywa juice mida ya jioni, twende Sehemu tukatulie tupate juice kidogo, tukaelekea Sehem moja kuna viti pana uwazi wanauzaga mazaga kama yote, tumekaa pale me nikachukua kiti changu nikawa nakunywa juice yangu tamu taratibu huku nachezea simu.
Yule jamaa nae akakaa na dem wake wanakunywa juice pale kwenye meza yao. Sasa Kakaja ka dogo pale kanaomba juice, kumbe kaliagizwa na mtu na huyo mtu baadae kidogo tu alikuja pale nilipokuwa mimi, nikakapa elfu tano kanunue na wenzake wagawane, kale kadogo kameondoka kakanunua kakarudi na wenzake kama kumi hivi wananishukuru.
Walivoondoka pale nipo na juice yangu nakunywa taratibu akaja Mdada mmoja kukaa nilipokuwa mimi, akanisalimia pale nikaitikia, amekaaa kama dakika tatu ananiongelesha namjibu kwa shida sana, naona kila mtu ananiangalia, yule Dem wa yule jamaa akaniita "Shem njoo huku karibu mbona umetutenga?" Nikamwambia Kuwa na amani Shem.
Yule sista pale alienikuta Akaniuliza kama nimekuja na wale, nikamjibu ndio ila kuna mtu namsubiri hapa(Ili aniache mwenyewe). Mfukoni nilikuwa na elfu kumi, nikawa nawaza sijui nimnunulie juice na yeye, nikasema hapa sina msaada na mtu.
Nikajikuta nimeropoka bhana, Dada karibu juice, si akaipokea bhana, akanywa mara moja akanirudishia tena 😂 yule dem wa bro akaniita tena "We shem njoo". Yaani wakati huo natetemeka tu nawaza leo kwisha habari yangu 😂.
Nikawa nanyanyuka niondoke, niwafuate walipo, nikampa ile juice yule dada akaipokea tena bila wasiwasi, nimefika pale kwa bro yule dem akasem "Usiwe na mazoea na watu wa huku kaa hapa", bro akadakia "Si umwache mtoto wa kiume huyu bhana". Yule dada kule niliempa juice akaniita tena "Samahan kaka nanii njoo"
Kugeuka hivi naona kawekewa msosi wa gharama sana mezani pale, akatoa na hela akalipia me naona kwa mbali, nikamjibu "Asante dada we kula usijali." Akasema "Njoo mara moja tu."
Yule dem wa bro akasema "ole wako uende, Nawe dada si udeal na mambo yako unashindwa kujiheshimu vp". Nikawa nimetulia tu pale sielewi natetemeka naogopa sana yaani.
Ilikuwa saa mbili usiku tukawa tumenyanyuka tuanze kurudi home sasa. yule dada akasema tena "bro hata kuniaga pia, sio vizuri jamani ". Nikasema "Aah sema umeniwahi, nakutakia usiku mwema, bye 👋". Akatikisa kichwa kuitikia.
Tumerudi home njiani yule dem wa bro ananiongelesha sana af yule jamaa katulia tuli. mimi naulizwa maswali mawili mawili nakosa majibu yaani sijiamini kabisa. Tumefka ghetto tumekaa kama lisaa tumekula pale, jamaa akaniaga ampeleke dem wake kumrudisha home.
DHARAU! DHARAU! DHARAU!
Kesho yake jioni jamaa hakuondoka na mimi, na mimi sikutaka tena kutembea nae, nikabaki pale nacheck movie ghetto, akanambia kuna mahali anaelekea anaweza kuchelewa kurudi.
Kumbe bhana jamaa alimfuata dem mmoja hivi sijui malaya hata sielewi, akamleta ghetto, akapanda Kwenye kitanda chake na yule Malaya wakaanza kufanya mapenzi mbele yangu asee!
Mimi nipo tu pale Nimeshindwa hata kuzima TV nacheck movie, na jamaa kafunga mlango funguo anazo yeye, kile chumba kilikuwa ni sebule tu kipana na kina kila kitu, kwaharaka haraka nikajua huyu jamaa hayuko sawa. nikavumilia ile DHARAU.
Alipiga kama viwili kisha wakatoka nje, Akachukua kama nusu saa akaja tena na yule dem wake mkali yule wa jana. Wakati huo me nilitoka kidogo niwapishe, jamaa hakusema chochote mbele ya yule Dem, baada ya dakika kama 45 akanitumia meseji "dogo njoo kashaondoka".
Nikarudi, kufungua mlango nakuta jamaa anakula dem sikuamini na yule dem nae akashtuka, kumbe jamaa alimdanganya kuwa nimeondoka kwenda ghetto kwangu na alimwambia kuwa mimi siishi pale.
Nikatoka nje kwa hasira, nikawa nasikia purukushani mule ndani kale ka dada kanalalamika kanaomba nguo zake kavae kaondoke, jamaa hataki kabisa ameng'ang'ania zile nguo.
Nikapiga mahesabu yangu chap chap nikasema hapa silali leo, nikamsubiri yule dada ametoka ndani na yule jamaa wanabishana bishana nje pale na me nikazama ndani nikaweka vinguo vyangu kwenye bag, nikachomoka fyuuuu, nikaenda kutafuta guest house nikalipia 7000 nikalala pale.
Kesho yake asubuhi nikampigia simu jamaa angu ambae ndio alikuwa dhumuni langu mimi kumtembelea na sio yule muhuni, bro hakuwepo wakati haya yote yanatokea maana alikuwa kasafiri kidogo, nikamwambia kuna dharura imetokea narudi nyumbani kwanza.
Nikamtumia meseji na yule jamaa alienifanyia dharau nikamwambia "Bro, me nimeondoka ila brother sijamwambia chochote kilichotokea. kuwa na amani".
Jamaa akaniuliza niko wapi kwa sasa, sikumjibu chochote nikabadili na laini 😂, nikageuza nyumbani.
Na sikumwambia mtu yeyote kuwa nimefananishwa na bulb yaani watu wanafanya Mapenzi mbele yangu bila kuogopa chochote, so sad 😭
AISEE KUFANYA MAPENZI NA MSICHANA MBELE YA RAFIKI YAKO AU MTU AMBAYE HUMFAHAMU SIO BUSARA.
Kilichonifanya nisimulie hili tukio, ni kwamba limenitokea mara 3, la kwanza lilikuwa ni kabla ya hili, la pili ndio hili, na la tatu limenitokea Majuzi kati tu hapo.
Hii tabia sio nzuri kwakweli, kwanza ni Kudharauliana.