Huyu mwanaume mimi namwacha

Huyu mwanaume mimi namwacha

CHONDE CHONDE Zinduna huyo akikuacha njoo kwangu mimi ni kijana mtulivu na mwenye adabu isipokuwa tu nimeishia la saba la mkoloni......
 
Last edited by a moderator:
HUKO KOTE UNAZUNGUKA TU MIMI NDIYE CHAGUO LAKO.....
SEMA NA MOYO WAKO KIMWANA Zinduna.....
 
Last edited by a moderator:
hakuna binadamu aliyekamilika, wote tunamapungufu....jitahidi sana kutumia saikolojia kutatua matatizo yako kwakumsoma mtu wako na si kufanya maamuzi fasta ambayo yanakuwa hayana tija kwani unaweza jikuta unakuwa na cv kubwa ya kuachana nawanaume. Pia, tatizo mabinti mnjielezaga sana juu ya mwanaume ambaye umewahi kuwa naye, hakuna kinachoboa kwa mwanaume kama kuelezea sana historia ya nyuma wewe umemsoma jamaa yako mpya then ukalimdhia kula mikausho namaisha yaendelee.
 
Mimi nasubiri Zinduna unyanyue hiyo APPLE ndio nitoe comment zangu

:A S 27::A S 27::A S 27: SLIM5, Kwi kwi kwi, yani badala ya kumsaidia Zinduna hapo unazidi kumpagawisha jamaa yake, jinsi alivyo na wivu pass word za demu wake zote anazo, sasa ngoja tusubiri tuone anavyokuja
 
1) wewe hujalelewa kwenye maadili, umelelewa kwe sampuli ya maadili. weye maadili awaggedani kabla ya ndoa
2) ana kila haki ya kuwa na wasiwasi na hao male frends wako becoz yeye mwenyewe alikupata mkiwa frends (another reason why u should never trust a lady saying he is just a frend)
3) anashika simu yako becoz he has every ryt to do so. kama haupo tayari kwa serious relationship basi usiingie kwenye relationship. relationship is about forgoing the i and believing in the we. kama upo clean basi hamna shida ya kulalamika yeye kushika simu yako
4) a decent woman doesnt discuss bedroom affairs in public....its just unlady like.
5) yeye kukuuliza wewe kama anakugegeda vizuri kuliko ex wako ni consequence ya wewe kugegedwa kabla ya ndoa....u shuld deal with it becoz its a choice u made and the price u pay. tatizo mwanadamu ana tabia ya kujidai yeye anajua kuliko Mungu.
6) last but not least u need to do a self evaluation, clearly ur selection of the husband material man needs polish. yule wa kwanza ulisema uliona atakuwa future husband huyu nae future husband but all have fallen short. it could be kuwa kweli hao wanaume bogus but sometyms u need to be careful with ur selection.

Nimeipenda comment hii
Najuaga we unahamasisha migegedano tu
 
Nimeipenda comment hii
Najuaga we unahamasisha migegedano tu

asante....kweli mie naongeaga sana kuhusu kugegedana a weakness i really have to get over. ila one thing is for sure i know what it means being in a serious relationship na nataka siku nikiamua kuwa in one basi i will be commited to it mia mia
 
Naomba na miye leo nifunguke.

Nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. Lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.

Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha Mungu.
Nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.

Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.

Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo.
Katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.

Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu.
Nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu.

Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.


Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.

Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.

Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.


Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini.

Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.


Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.


Nimeshindwa miye.
Atleast hujamfumania.ukimuacha uniambie niwe rafiki yako.na mimi nimeamia zanzibar
 
asante....kweli mie naongeaga sana kuhusu kugegedana a weakness i really have to get over. ila one thing is for sure i know what it means being in a serious relationship na nataka siku nikiamua kuwa in one basi i will be commited to it mia mia

All the best
Nimeangalia mara mbili mbili id..umekua tofauti sana leo. .again..all the best ukiamua kuwa committed
 
All the best
Nimeangalia mara mbili mbili id..umekua tofauti sana leo. .again..all the best ukiamua kuwa committed

well thanks i bliv kuwa nitapata tuu a decent lady and all shall be fyn ila drawback moja tuu na hili naona litafanya nisioe...sitaki mtoto
 
well thanks i bliv kuwa nitapata tuu a decent lady and all shall be fyn ila drawback moja tuu na hili naona litafanya nisioe...sitaki mtoto

Kwa nini hutaki mtoto?
Watoto ni blessing
 
Bidada no 1 z perfect..hapa 2mepata malalamiko yako 2 juu yake, hebu mlete huku na yey ajielez.
 
Zinduna hebu andika hii habari kwa mpangilio mzuri basi...

Weka paragraphs iwe rahisi kusoma kwa uzuri

Btw chapa lapa kama unaona umeshindwa kuvumilia wivu wa mpenzio

mbona imepangiliwa mkuu au ndio karekebisha tayari??
 
pole mwaya......... ila jitahidi kuongea nae kuwa apunguze hayo mambo na ajiamini... kachizika na wewe huyo...
 
Naomba kukuuliza swali dogo Zinduna
Kwa mfano ukiachana na huyo jamaa then ukatulia baada ya muda ukampata mwingine ambaye hatakua na tabia zinazofanana na huyu wa sasa, ila kwa bahati mbaya akawa na tabia mpya ambayo pia huipendi nae utamuacha? Na akaja mwingine nae ukamuacha
Utaacha wangapi??
 
charty huyu mwanaume habebeki na ni janga ka Boko Haram
Nishajisemesha mpaka basi. Ni mwepesi kuomba radhi, lakini habailiki.

Nitasubiri kama hatatokea mwanaume mwingine mwenye sifa angalau asilimia hamsini, bora nisiolewe

mwanamke kujiamini babu nimeku like bureeee
 
Last edited by a moderator:
Zinduna huyo jamaa ana gubu balaaa......

Hivi unazo khanga zimeandikwa wivu ni kidonda ukiushiriki utakonda? Hebu mvalie siku moja pengine msg itakua sent lol japo mie nna wivu ila huo too much wivu plus gubu na nongwa loh
 
Back
Top Bottom