Huyu mwanaume mimi namwacha

Huyu mwanaume mimi namwacha

Mwanaume wa hivyo hakufai

Ila mshauri akamwone mshauri nasaha amsaidie kuovwrcone inferiority complex aliyonayo

Pia ni Mtambuzi alitoa somo kuhusu wanaume wa hivyo... wafujaji kihisia.....

Sepa shosti


Tena akimbie haraka mana mijitu kama hii ikikuoa inaweza kataza hata usiende salimia ndugu zako.................
 
Naomba
na miye leo nifunguke.


Nina mwanaume tumekuwa kwenye
uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa.
Lakini
tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.

Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa,
mwenye malengo na pia mcha
Mungu.
Nilikutana
na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi
kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na
urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano
na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.

Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na
uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume
mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa
tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa
mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.

Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache
tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana
mawazo.
Katika
kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na
shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo,
nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia
kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.


Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi
nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na
usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri
niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu.
Nilikaa kwa
muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa
karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari
kilichonitokea nikiwa peke yangu.

Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata
mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu,
nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye
mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo
akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana
iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za
mwenzake.


Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu
atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na
tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila
mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.

Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake
ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja
uhusiano huo.

Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na
yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana
kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia.
Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati
yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la
kitandani.


Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana
kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki
zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na
hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua
nawasiliana na nani na kwa nini.

Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu
yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba
nao.


Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni
wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na
akirudi jioni anikute hapohapo.


Nimeshindwa
miye.

we ni muhuni, kwenda zako..!
 
wivu wakati mwingine ni kupenda kupindukia , zungumzeni hilo tatizo ili muishi pamoja
 
pole sana,,,,awali ni awali hakuna awali mbovu,halafu nimeona hapo jamaa alivotamani akupate kirahisi japo ktk mahusiano hutokea mengi kipindi cha kuachana na mwenza wako wa kwanza ukakimbilia chap kwa huyo dah sikukushaur kabisa hvi we hukosei halafu ukiachana na huyo utatafuta tena mwingine kwa style hiyo utadate na wangapi?? hvi ukimwacha ndo utakua umepata suluhu?


ukisha jibu hayo ntaja na mengine
Mamaafacebook, huyu mwanaume kwa kweli nimeshindwana naye, na kwa kadiri nilivyompima sitoweza, nitajakufa kwa presha, miye bado ni binti mdogo wa 20s sijazeeka bado eh, na sina kasoro, kwa hiyo sina haraka miye
 
Last edited by a moderator:
Mamaafacebook, huyu mwanaume kwa kweli nimeshindwana naye, na kwa kadiri nilivyompima sitoweza, nitajakufa kwa presha, miye bado ni binti mdogo wa 20s sijazeeka bado eh, na sina kasoro, kwa hiyo sina haraka miye

Owh kumbe bas sawa
 
Last edited by a moderator:
Sifa kubwa ya mwanaume ni kujiamini, wivu unahusishwa kwenye mapenzi ya kweli ila usipitilize. Vilevile kuna swali apo, ivi kwenye mapenzi mwanaume nae uwa anadeka???
 
urafiki wa kawaida wa mabinti tena wa 20s na wananume kwangu kwangu ni ngumu kuamini.Yaani manzi wangu aniambie yule ni rafiki tu sitamwelewa maana hata mimi nina marafiki wa kike tu lakini ni michepuko ya kushibana.
wivu kwenye mapenzi muhimu
 
kifupi ni kwamba hiyu jamaa ameshajua hisia zako na udhaifu wako hivyo anaona anaweza kukupelekesha anavyopenda, ni vizuri kama mnapendana kwa dhati na mna malengo ya kuishi kama mume na mke mkae chini muelezana kila mtu ajue ni nini asichokipenda mwenzake ukiona hamna mabadiliko bora UANGALIE USTAARABU WAKO MAPEMA SHOSTITO
 
ikiwa vipi mpige chini huyo wa makunduchi....
 
1) wewe hujalelewa kwenye maadili, umelelewa kwe sampuli ya maadili. weye maadili awaggedani kabla ya ndoa
2) ana kila haki ya kuwa na wasiwasi na hao male frends wako becoz yeye mwenyewe alikupata mkiwa frends (another reason why u should never trust a lady saying he is just a frend)
3) anashika simu yako becoz he has every ryt to do so. kama haupo tayari kwa serious relationship basi usiingie kwenye relationship. relationship is about forgoing the i and believing in the we. kama upo clean basi hamna shida ya kulalamika yeye kushika simu yako
4) a decent woman doesnt discuss bedroom affairs in public....its just unlady like.
5) yeye kukuuliza wewe kama anakugegeda vizuri kuliko ex wako ni consequence ya wewe kugegedwa kabla ya ndoa....u shuld deal with it becoz its a choice u made and the price u pay. tatizo mwanadamu ana tabia ya kujidai yeye anajua kuliko Mungu.
6) last but not least u need to do a self evaluation, clearly ur selection of the husband material man needs polish. yule wa kwanza ulisema uliona atakuwa future husband huyu nae future husband but all have fallen short. it could be kuwa kweli hao wanaume bogus but sometyms u need to be careful with ur selection.

Man..everything you've written makes a lot of sense. Couldn't agree more!
 
Naomba na miye leo nifunguke.

Nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. Lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.

Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha Mungu.
Nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.

Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.

Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo.
Katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.

Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu.
Nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu.

Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.


Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.

Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.

Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.


Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini.

Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.


Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.


Nimeshindwa miye.

Hawezi kumuamini yeyote sababu mwanzo wa uhusiano wenu ni urafiki kwaiyo usitegemee ataendelea kukuacha una marafiki wa kiume wakija kumgeuka? na urafiki wa huo hakuna ndio maana ata nyie mmeishia katika mapenzi, pili huyo ana wivu ndio maana haishi kufanya comparison kati yake na hao wengine hii akiiendeleza itawasumbua sana mana sometime mnaweza gombana sababu ya mambo ya kale, 3. Kuwa makini sana na uhusiano huu maana huyu mtu anakujua in and out anaweza take advantage ya kukuumiza kutwa kwa kufanya reference ya maisha uliyopitia
 
Kama kweli umelelewa katika maadili ya dini basi jitahidi ata kubadilisha Avatar yako maana inawapa wakati mgumu watu wengine hapahapa ndani, weka picha ambayo inaendana na maadili ya dini
 
Back
Top Bottom