Miss Neddy
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 14,684
- 8,754
mapenzi kizunguzungu
1) wewe hujalelewa kwenye maadili, umelelewa kwe sampuli ya maadili. weye maadili awaggedani kabla ya ndoa
2) ana kila haki ya kuwa na wasiwasi na hao male frends wako becoz yeye mwenyewe alikupata mkiwa frends (another reason why u should never trust a lady saying he is just a frend)
3) anashika simu yako becoz he has every ryt to do so. kama haupo tayari kwa serious relationship basi usiingie kwenye relationship. relationship is about forgoing the i and believing in the we. kama upo clean basi hamna shida ya kulalamika yeye kushika simu yako
4) a decent woman doesnt discuss bedroom affairs in public....its just unlady like.
5) yeye kukuuliza wewe kama anakugegeda vizuri kuliko ex wako ni consequence ya wewe kugegedwa kabla ya ndoa....u shuld deal with it becoz its a choice u made and the price u pay. tatizo mwanadamu ana tabia ya kujidai yeye anajua kuliko Mungu.
6) last but not least u need to do a self evaluation, clearly ur selection of the husband material man needs polish. yule wa kwanza ulisema uliona atakuwa future husband huyu nae future husband but all have fallen short. it could be kuwa kweli hao wanaume bogus but sometyms u need to be careful with ur selection.
We must learn to compliment each other and compromise. Mr. Perfect anapatikana sayari ya Mars, huku duniani hamna mr. Perfect.
Mweh! na wewe unaongea sana bwana!
Haya ndiyo hivyo nishaamua kuachia ngazi nawapisha wengine.
Naomba na miye leo nifunguke.
Nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. Lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.
Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha Mungu.Nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.
Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.
Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo. Katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.
Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu. Nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu.
Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.
Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.
Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.
Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.
Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini.
Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.
Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.
Nimeshindwa miye.
mapenzi kizunguzungu
Sa mmeduu wakati hamjafunga ndoa ama sijaelewa?
Bora yesheee shost.........huyo hafai........