Huyu mwanaume mimi namwacha

Huyu mwanaume mimi namwacha

Hayaa sasa zinduna mchagua nazi.................

Avumapo papa kumbe...............................

Ukimpata mwingine usisite kuja kutupatia vimbwanga vyake hapa paha jamvini.
 
Zinduna ,"Love & relationships don't require us to be at our best, only that we try to help one another to be the best", kusema kweli kupata mtu ambaye hata kuwa na kasoro au awe na kila kitu ukipendacho ni ngumu sana, ndo maana nataka kukuambia jaribu kwa kila uwezalo kumrekebisha otherwise Ghubu na kudeka ni vitu vidogo sana.

huyu mwanaume ana matatizo akimuoa atamsumbua sana,haiwezekani mtu kufuta namba zoo
te za wanaume kwenye simu,kwani yeye ana ndg wa kiume,pia inaelekea hana heshima huyo mwanaume.what kind of graduate he is ?
 
Last edited by a moderator:
Okay Zinduna enjoy your freedom.

Last edited by a moderator:
Naomba na miye leo nifunguke.

Nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. Lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.

Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha Mungu.
Nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.

Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.

Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo.
Katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.

Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu.
Nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu.

Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.

Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.

Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.

Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.

Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini.

Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.

Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.

Nimeshindwa miye.

Before you leave, hebu mwambie unataka abadilike na aweje? Ikishindikana Fanya kulianzisha, but I can't see future with that man, kwani haiwezekani tuanze kusomana tabia then Tuoane, there z no love there. Kozi mpo marafiki for so long
 
Mimi binafsi nina wasiwasi na uhalisia wa hii habar,,, Zinduna mbona hujanitag, au kuna mtu katumia ID yako? Wewe huyo wa kufanya madudu haya kwenye mahusiano?
 
[/QUOT
Mna mcha Mungu gani anayeruhusu uzinzi!?
 
Wewe utakua huna tabia nzuri,sisi tuko kwenye ndoa simu kushikiana ni kawaida tu sasa wewe hutaki kwa nini?Utaishia kibadili mabwana mwisho utapata magonjwa!
 
huyu mwanaume ana matatizo akimuoa atamsumbua sana,haiwezekani mtu kufuta namba zoo
te za wanaume kwenye simu,kwani yeye ana ndg wa kiume,pia inaelekea hana heshima huyo mwanaume.what kind of graduate he is ?

Mkuu tracy martins, nimekusoma ila sijamshauri akubali amuoe lakini ajaribu zaidi kumrekebisha na if possible kutumia msaada wa close frnds wa huyo mkaka kwani kwa mtazamo wangu hivyo vitabia vinarekebishika. Trust me, am a man and hizo kasoro ni ndogo sana. Huwezi pata a complete full package
 
Last edited by a moderator:
pole sana.. ushasema unamwacha basi mwache.. ila ungemuweka wazi kuwa unamwacha kwa sababu zipi.
 
naomba na miye leo nifunguke.nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu. Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha mungu.nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la mwakakogwa huko makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa. Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule. Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo. katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu. alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu. nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu. Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa maulid ya kuzaliwa mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake. Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini. Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.nimeshindwa miye.
kama kweli unampenda kwanin usimshauri abadarike, ushauri wa bure. Kabla huja engage na mtu kila mtu amwambie mwenzake utaratibu wake wa maisha nini hutaki kufanyiwa na nini unataka ufanyiwe kabla hata ya
 
Wewe Zinduna mapepe usikubali kupakuliwa ovyo ww. Unasema mwanamme mchamungu sasa mbona mnapakuana?
 
Mwanaume hana shida kaona alivyokupata na anajua kuna mtu mwingine atakupata mda si mrefu kwa maneno mengine amekusoma haujatulia ndo maana ana wasiwasi nawe na utazunguka mpaka mwisho ukifikiria dushe zilizo....... Utalia na hakuna aliyekuoa take care
 
na wewe kwa matamasha tu, mara tamasha la mwakasege, mara mkesha wa Idd kote huko upo?!! mi napenda tu usimulie ulivomfuma bwanaako na rafikiyo wa karibu, inaonekana genge lako haliaminiki katu!
 
na wewe kwa matamasha tu, mara tamasha la mwakasege, mara mkesha wa Idd kote huko upo?!! mi napenda tu usimulie ulivomfuma bwanaako na rafikiyo wa karibu, inaonekana genge lako haliaminiki katu!

Yameanza lini haya
 
Before you leave, hebu mwambie unataka abadilike na aweje? Ikishindikana Fanya kulianzisha, but I can't see future with that man, kwani haiwezekani tuanze kusomana tabia then Tuoane, there z no love there. Kozi mpo marafiki for so long

kusomana tabia ni kawaida, ssema watu wengi huwa hawaambiani kama wanasomana tabia!
 
Back
Top Bottom