Huyu mwanaume mimi namwacha

Huyu mwanaume mimi namwacha

Naomba kukuuliza swali dogo Zinduna
Kwa mfano ukiachana na huyo jamaa then ukatulia baada ya muda ukampata mwingine ambaye hatakua na tabia zinazofanana na huyu wa sasa, ila kwa bahati mbaya akawa na tabia mpya ambayo pia huipendi nae utamuacha? Na akaja mwingine nae ukamuacha
Utaacha wangapi??

Nalo neno hakuna mkamilifu duniani ila afadhali ya huku shemegi yetu kuna wengine visa vyao havisemeki.......
 
Sa unaomba ushauri au ushafikia muafaka/maamuz? Na ni waz kwamb humpend na kama unampenda kwa nin usimwambie ukwel akabadilika? Wanawake wengine bana majanga. Haya muache ka unafikiri mwingine utakaye mpata atakuwa dizain hiyo unayoitaka.
 
Wewe kama unajua hakuna kibaya unachowasiliana na hao watu wako, kuna haja gani ya kumzuia asipekue sim yako? mambo mengine ni hatua za kimakuzi tu, sio kweli kwamba hiyo tabia atakuwa nayo miaka yote.
Wewe jaribu kumuacha halafu upate mwanaume mwenye tabia ya kutembeza kichapo au malaya ndio utajuta.
 
Zinduna we hutaki kumsifia, kumdekeza na asikuonee wivu unataka amuonee wivu nani inaonyesha huko vizuri ww
 
Kama unaona mapenzi ni jambo la muhimu kwako, basi vumilia, ndiyo mapenzi hayo, ukimwacha tena huyo halafu ukatafuta mwingine, si ajabu huyo ukamfumania hata na shangazi yako, Wengine tumeamua mapenzi yasiwe jambo la muhimu, mimi tukilala na wewe leo, kesho tunapishana tu hata nikukute na Rashid mi sina tatizo...
 
Kama kweli umelelewa katika maadili ya dini basi jitahidi ata kubadilisha Avatar yako maana inawapa wakati mgumu watu wengine hapahapa ndani, weka picha ambayo inaendana na maadili ya dini

Avatar yako ikoje mi siioni, lol
 
Zinduna ,"Love & relationships don't require us to be at our best, only that we try to help one another to be the best", kusema kweli kupata mtu ambaye hata kuwa na kasoro au awe na kila kitu ukipendacho ni ngumu sana, ndo maana nataka kukuambia jaribu kwa kila uwezalo kumrekebisha otherwise Ghubu na kudeka ni vitu vidogo sana.
 
Last edited by a moderator:
Kama unaona mapenzi ni jambo la muhimu kwako, basi vumilia, ndiyo mapenzi hayo, ukimwacha tena huyo halafu ukatafuta mwingine, si ajabu huyo ukamfumania hata na shangazi yako, Wengine tumeamua mapenzi yasiwe jambo la muhimu, mimi tukilala na wewe leo, kesho tunapishana tu hata nikukute na Rashid mi sina tatizo...

umemaliza kila kitu
 
Mi na wangu huwa tuna share simu,mi lazima simu yake nishike na uzuri ye pia huwa lazima ashike simu yangu,so tumefanana kwa interests na wivu,but why iwe ngumu ye kushika simu yako?
 
Naomba na miye leo nifunguke.

Nina mwanaume tumekuwa kwenye uhusiano kimapenzi (namaanisha kimapenzi) kwa takriban mwaka mmoja sasa. Lakini tulijuana miaka mitatu iliyopita akiwa kama rafiki mwema kwangu.

Ni kijana mwenye sifa nizipendazo, yaani ni mtaratibu, mwerevu, mwelewa, mwenye malengo na pia mcha Mungu.
Nilikutana na huyu kijana wakati wa tamasha la Mwakakogwa huko Makunduchi, basi kuanzia hapo tukawa marafiki. Aliwahi kunitamkia kuhusu kuwa na urafiki wa kimapenzi,lakini sikumkubalia kwa sababu nilikuwa na uhusiano na mwanaume mwingine ambaye tulikuwa na malengo ya kufunga ndoa.

Kusema kweli nilivutiwa na huyu kijana ila nilishindwa kukubali kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kwa sababu nilishaji commit kwa mwanaume mwingine, na miye ni binti niliyelelewa katika maadili kwa hiyo sikuwa tayari kumpaka mafuta huyu kijana wa watu kwa nyuma ya chupa, yaani kuwa mnafiki na ndumilakuwili wa kutaka huku na kule.

Urafiki wetu na huyu kijana ulikuwa ni wakawaida tu na mara chache tulikuwa tunakutana kwa mazungumzo ya hapa na pale katika kubadilishana mawazo.
Katika kipindi ambacho huyu mwanaume niliyekuwa naye nilipomfumania na shogangu wa kupika na kupakua wakiwa kitandani wakifanya tendo, nilimsimulia huyu kijana kama rafiki mwema ili kupata ushauri na pia kufarijiwa kwa sababu tulishakuwa marafiki kwa muda mrefu.

Alinishawishi sana nisivunje uhusiano na mpenzi wangu, akinisihi nimsamehe kwani ni ibilisitu alimpitia, lakini kutokana na kuumizwa na usaliti niliofanyiwa na mpenzi wangu niliyemuamini sana nilikata shauri niuvunje uhusiano na kushika hamsini zangu.
Nilikaa kwa muda wa miezi sita bila kuwa na uhusiano, lakini pia nilisita kuwa karibu na huyu rafiki yangu kwa muda wote huo nikitaka kutafakari kilichonitokea nikiwa peke yangu.

Yule kijana wala hakufanya makeke ya kunitafuta, na yeye alikata mawasiliano. Baada ya hiyo miezi sita ya kuachana na mpenzi wangu, nikarudisha mawasiliano na huyu rafiki yangu baada ya kukutana kwenye mkesha wa Maulid ya kuzaliwa Mtume. Baada ya kurudisha mawasiliano ndipo akanitaka tuanzishe uhusiano wa kimapenzi akiniahidi kwamba tutaoana iwapo kila mmoja ataridhika na tabia za mwenzake.


Tukaanzisha uhusiano wa kimapenzi na nilijenga imani kwamba, huyu atakuwa mume mwema kwa sababu anazo zifa zote nizitakazo, na tulishafahamiana kwa takriban miaka miwili nyuma kama marafiki na kila mmoja alikuwa anafahamu kuhusu mahusiano ya mwenzake.

Kwa upande wake, yeye aliwahi kunisimulia kwamba alikuwa na mpenzi wake ambaye alikuwa hajatulia, na hawaendani na hivyo aliamua kuvunja uhusiano huo.

Lakini baada ya miezi kadhaa tangu kuanzisha uhusiano na huyu kijana, na yeye akaanza vibweka. Kwanza ana wivu kupindukia, na anapenda sana kuzungumzia mahusiano yangu ya nyuma kwa namna ya kuniumiza kihisia. Wakati mwingine tukiwa kitandani anataka kujua ni nani mzuri zaidi kati yake na huyo bwanangu wa zamani katika swala zima la kitandani.


Hata nimsifie, lakini anahisi kama namnafiki tu na anapenda sana kusifiwa sifiwa na kudekezwa na kunithibiti nisiwasiliane na marafiki zangu. Hamuanini mtu yeyote wa jinsia ya kiume kuwa karibu na mimi, na hivi sasa anataka kuingilia mawasiliano yangu ya simu akitaka kujua nawasiliana na nani na kwa nini.

Kuna wakati aliwahi kufuta namba zote za wanaume niliowasevu kwenye simu yangu ambao wote ni jamaa zangu ambao nina nasaba nao.


Nimeshindwamiye, bora yeshe, mwanaume gani huyu asiyejiamini, hivi tu ni wapenzi akijanioa si atanigeuza mdoli wa kuniweka hapo asubuhi na akirudi jioni anikute hapohapo.


Nimeshindwa miye.
Kwahiyo upo singo au????
 
Ha ha ha ha ha ha ha ha miye mechekaaa mpaka basiiiii jamaniii
 
Back
Top Bottom