Huyu mwanaume alichonitendea kimeniumiza sana

Huyu mwanaume alichonitendea kimeniumiza sana

Habari wana JF
Mimi ni binti wa miaka 22. Nmemaliza elimu yangu ya shahada mwaka huu.Kuna jambo fulani limetokea kuniumiza sana labda kwasababu nilikuwa nmesha expect something.Kuna familia flan ivi tajiri na ni family friends wetu ilikuja nyumbani kwetu kwa lengo la kuomba uchumba kwa ajili ya kijana wao.

Kwakua bado nlikua cjamalizia semester yangu ya mwisho ili nihitimu chuo nikawaambia ngoja kwanza nimalize af mengne yatafata.Kijana akaja mpaka nyumbani kwetu tukaongea akaeleza jambo lake bac tukaendelea kuwasiliana.Mda kidogo ukapita ghafla akakata mawasiliano.Lakini ndugu zake bado walikua wananitafuta kuulizia kwamba tumefkia wap na ndugu yao nkawaambia ck izi hata siongei nae alisha acha kunitafuta.

Bac nkaona ngoja nimuulize muhusika nni kinaendelea ili nijue kama hii issue bado ipo ama laa ili niache kufikiria haya mambo. Bac nkamtua text ili kujua nni kinaendelea lakn hata hakunijibu. Sikupenda alichofanya nkamtumia tena texts na zinakua received watsap lakn anazikaushia tuu kunionesha kabsa ana ni ignore...

Sasa kwann asinieleze tu kwamba amechange mind ama hakunielewa jaman kuliko kuni ignore ivo af ukizingatia walikuja wenyewe mpaka hme kwetu wazazi wake na yeye af saiv ana ni treat kama vile si exist jaman yan kanidharau.ni sawa kweli jaman ama ni mim tu ndo nlikua nshaanza kuweka expectations.
Kwani alishakukula?
Kama hajakukula achana nae,,,
You can't stop the rain.
 
Kama ulianza kumjibu text kama vile "my wangu" kwanini asikimbie, yote kwa yote, kama ulikua na boyfriend wako chuo, komaa nae utoboe nae usitegemee kitonga, uchumi wa kati huu
 
Kuolewa ni kuanza maisha upya,hasa ndio focus ya wanawake wengi. Kwa hiyo ilipaswa uolewe kwanza ndio ukiwa huko ndio ujue utaratibu unaofuata kutokea huko. Wanaume huwa hawasubirishwagi. Hapo anaweza akawa amempata mpya. Endele na maisha yako mengine tu. Sahau kuhusu utajiri wao. (Halafu umemwandikia tu sms,kitu msichokijua watu siku hizi,simu zina mambo mengi,unaweza kukuta sms hazimfikii,japo wewe unaona kama anazisoma,inaweza kuwa sio hivyo. Mpigie simu kabisa)
 
Sio kwamba nime ku ignore nili gundua Ulkua unataka umalizie utamu iyo semester naka boy ka chuo..pole sana nimesha move on we endelea na maisha yako tu
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]kumekucha
 
Mtu kaja unamsuburisha vuna ulichopanda Nakushauri mpotezee tu jua mambo yako maaana ulizungua
Na huu ndio ukweli mchungu.
Vibinti vya chuo huwa vina mashauzi na dharau sana.
Wakiwa kule chuoni hujisahau sana na kudhani wanavyopewa boom itakuwa ni milele wanapokea tu boom.
Hii humfanya mwanaume aliye serious kuwa disappointed na kukata tamaa.
Na kumbuka mtaani kuna warembo lukuki wanaisaka hiyo fursa usiku na mchana na wanakesha kwenye maombi na kwa waganga wapate wanaume wenye pesa na wanaojiweza.
 
Sa si bora kaku ignore km ya ndoa..


Mi mwanamke akinikataa kabla sijafunga nae ndoa sitakuja kumchukia kabisaaaa
 
Mke wangu, mshikaji, jamaa au rafiki yeyote akitaka kunitumia ujumbe anatakiwa awe makini sana na uandishi.

Wewe kama mwanaume mpenzi wako anakuandikia enti (xaxa xweet, ctakuja, 2taonana n.k) harafu ukaendelea kucheka nae basi wote mtakuwa na tabia moja ya uandishi.
Wewe uandishi wako umeuangalia kwa makini!! Unaandika harafu then unakosoa uandishi wawenzako😆😆😆😆
 
Mabinti wa siku hizi mnadharau sana ndoa inapowagongea hodi halafu ni wepesi sana kuanza kulalamika baadae kuwa mnachezewa na kuhangaika nyumba za ibada kutafuta ndoa....
Lakini alikuwa anasoma mkuu, what's wrong kuwaambia wasubiri amalize masomo yake kwanza? Kuna nyakati mtu anatakiwa kuishi kwa malengo yake na sio utashi wa jamii.
 
Huo uandishi wako ndio maana jamaa kakuacha wewe utaandikaje....

Mda badala ya (Muda)
Bac badala ya (Basi)
Cku izi badala ya (Siku hizi)
Ivi badala ya (Hivi)
Af badala ya (Harafu)
Saiv badala ya (Sasa hivi)

Wanawake badilikeni huo uandishi kuna wanaume wengine hatupendi kuandikiwa hivyo.
[emoji2211][emoji2211]
Harafu????
 
Mkuu vipi hapa (haraka au ni halaka? ) furaha au fulaha)

Wote, nyote ni sawa tu.

Pia mimi nimemaanisha uandishi huu xaxa badala ya (sasa) cku izi badala ya (siku hizi)
Kubali tu kwamba umekosea
Hakuna neno "harafu" kwenye kiswahili.
 
Mwanaume yoyote huwa hapendezwi na kusubirishwa na watu wengi hawaelewi kuoa na kuolewa sio jambo lakupigana tarehe ikiwa mtu kaonyesha nia mambo yanatakiwa fasta fasta
 
Kabisa na mshkuru Mungu lakn atleast ata angeniweka wazi tu sio kuni ignore ivo haipendez maana walianzisha mada wenyewe wakaja hadi kwetu
Jitahid kumtafuta,physically usihujumu kwa simu tu,usikute amepewa taarfa zisizo za kweli kuhus wewe na akaziamn kwahyo yuko dillema,au anaweza kuwa anapitia kipind kigumu kias cha kuona kila mtu n msaliti au mbaya kwake...(hii inatokeaga sana kwa wanaume).. Jitahid kuwa POSITIVE ila usitegemee ndoa Bali tegemea kujifunza mkuu...May God be with Your heart
 
Mshukuru sana Mungu wako kwa hili..kuna maumivu makubwa umeepushiwa mbeleni...just imagine mngefunga ndoa halafu ukawa ignored kama sasa ungejisikiaje?
Hakika sometimes unaweza laumu bure kumbe umeepukana na janga Kubwa tu.
 
Hapana kuwa ignored ndo imeniumiza halafu pia he already started openning up na kunieleza kwamba anaitaji niwe mke wake af ghafla akakata mawasiliano
May be Mshukur Mungu kukufundsha kuwa Usiharakie ndoa ,usije kuharakia kuwa mtumwa au kuumia...everyone had own destiny
 
Wanawake katika baadhi ya mambo mnafeli sana;

1:Humtafuti mpaka akutafute (wewe ndiye uliyeanza kumpotezea)

2:Kutozijibu sms zako haimaanishi kuwa kakudharau kwa sababu hujui anapitia katika hali gani, kwanini basi usimdhanie vizuri?

Btw Wewe mwenyewe ndiye uliyesema kuwa usubiriwe mpaka umalize chuo, vipi ishamaliza hicho chuo?

NB:
Usimlaumu mtu kabla hujajua anapitia mazingira gani kwa wakati huo hii itakusaidia kuyakimbiza maradhi ya presha na kisukari na pia unaweza ukaepukana na mengi mabaya na kuyapata mengi mazuri.

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
Smart mkuuu
 
Back
Top Bottom