Huyu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mbona simuelewi

Kusema ukweli kwenye paperwork kipindi Kile alikuwaga mtamu, ila kwenye presentation unaweza usiamini km ndo yy aliyeandika, ukimtekenya kidogo hakawii kupanic, sasa na hapa bungeni hapamtoshi angebaki tu ofisini kuandaa makaratasi, sasa ukichanganya chama alichopo na lisu kashamjulia huyu jamaa basi ni fulu kumpagawisha
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge(mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.
Wala huhitaji kumuomba Mungu msamaha kwani huo ni mtizamo wako. Kama watu wote wangekuwa na msimamo ambao unampendeza Mungu, wahubiri (mashehe na wachungaji) wangefanya kazi gani?
Juu ya hayo, kumbuka kwamba siasa ni sayansi ya jamii. Ni sayansi ambayo wote mnaweza kuingia maabara, mkatumia zana za aina moja (same apparatus), mkafanya uchambuzi wa pamoja (same observation) na mkawa na matokeo ya aina moja (same results) lakini kwenye hitimisho (conclusion) mkawa na lugha tofauti lakini yenye maudhui yale yale (different language but same concept).
Jitafakari!
 
Kuna baadhi ya wasomi na ma professor wakiingia kwenye siasa taaluma zao wanashikiwa na wateuzi na kujitoa fahamu inatia huruma
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge (mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.

Tuwekee alichokisema kulichokufanya wewe ufikie tamati hiyo, bila hivyo wewe ndiye uletae ushabiki wa kisiasa.
 
Huyo jamaa nashangaa hata alipewaje uanasheria mkuu.. Wapitie upya vyeti vyake aisee... Hata ukiweka ukada pembeni jamaa is very empty!
ooooh MG. Kinyume chake wewe vyeti vyako vipitiwe kama unavyo anway!
 
Tuwekee alichokisema kulichokufanya wewe ufikie tamati hiyo, bila hivyo wewe ndiye uletae ushabiki wa kisiasa.
Wanaofatilia bunge wanajua nasema nini.
Mimi sina chama wala sitakuja kua na chama
Kama Chadema na CCM wanawalipa ninyi fedha kutetea uozo mimi sipo huko wala sileti hapa uzi wa kuiponda ccm wala chadema.
Nikiwa na njaa ntatafuta kazi ya kutuliza njaa yangu ila sio ccm wala chadema wala chama chochote cha siasa.
 
Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
QUOTE] Inaonekana unatoa heshima kirahisirahisi mno. Tueleze kwanza ni nini kilikufanya umpe heshima 100% halafu ghafla bin vuu unazishusha mpaka 0%.
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge(mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.

Huenda umemshushia heshima moyoni mwako sababu hakukidhi matakwa ya nafsi yako. Lakini alichozungumza Masaju ni mshangao wake kwa vyombo vya dola kwa nini havijachukua hatua stahiki kuwahoji watu waliokaribu na mazingira ya kupotea kwa Ben Saanane (huenda ni pamoja na Mh. Mbowe mwenyewe) na hatua hii ni ya kikanuni ktk michakato ya kiuchunguzi sio suala la kisiasa hata kama watakuja hao makachero toka SCOTLAND YARD kama inavyodaiwa na Mh.Mbowe na watetea haki wengine, bado miongoni mwa watu wa kwanza kusaidia uchunguzi atakuwa ni pamoja na yeye Mh. Mbowe.
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge(mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.
Kumshusha na kumpandisha thamani yake ni juu yako mwenyewe wala haimtii hasara.
Ili uwewe na kaakili kidogo unatakiwa kuwa mtulivu wakati unasikiliza bunge. AG ni mshauri wa mambo ya sheria kwa serikali na bunge zima. Je hoja aliyochangia ni ya kisheria? Jibu ni ndio ni kuhusu kuleta wachunguzi kutoka Scotland Yard kuchunguza kupotea kwa Ben Sanane.
 
Rudi kaangalie clip upya alafu useme kama yule ni mbunge(mwanasiasa) au ni mwanasheria mkuu wa serikali(mtumishi wa umma), note yafuatayo: anavyotoa presentation ya hoja zake, anavyotaka uchunguzi ufanyike na anavyotoa maelekezo kama humjui utajua ni mbunge wa chama cha siasa.

Suppose humjui kwamba yule ndo George Masaju-AG sikiliza maongezi yake na hoja zake kisha useme ni kitu gani kinaweza kukutofautishia AG na mbunge iwe Chadema au CCM au chama chochote
 
Kabla sijaambiwa kuwa huyu ndiye mwanasheria wa serikali, nilijiuliza huyu ni mbunge wa jimbo gani kupitia CCM? Nikaambiwa ndiye mwanasheria wa serikali. Mungu wangu! Sikuamini. Sionagi tofauti ya yeye na Livingstone Lusinde (Kibajaji) ndani ya bunge kihoja. Ni kama vile naye ni mbunge. Hivi ataacha 'legacy' gani muda wake ukiisha? Ovyo kabisa.
 
Watu wananisakama hapa wanadhani mimi natetea chama hapana, mimi nasema nilichokiona bungeni, hayo mambo ya vyama watajua wenyewe mi sitaki vyama vyenu vya kulilia ugali
 
Kilichomuwepa pale ni UKANDA na sivingnevyo kwa maana kichwani ni empty space

Sena kweli ni ukanda kivipi?
Kama ni uteuzi aliteuliwa na Jk

Pia jana alilishangaa jeshi la polisi kuogopa kuwahoji watu wa karibu na Ben saa nane wakati viashiria vya mawasiliano vikionyesha watu wa mwisho kuwasiliana nao ni hao hao wanajifanya kutojua halafu wanaongoza kulalamika bungeni wakati walitakiwa kuisaidia polisi
 
Ameegemea upande upi?unatokwa na makamasi kwa kusikia habari ambazo hupendi kuzisikia?
Uwe tu na uvumilivu wa kisiasa,Mbowe amesema hakuna alie juu ya sheria,ni lazima Mbowe akamatwe ili awasaidie polisi,kwa nini katibu wake myeka amepotea kazini halafu yeye anapanda ndege anakwenda ulaya kunywa mvinyo
Huenda walienda naye kwa malengo maalumu.
 
Back
Top Bottom