Huyu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mbona simuelewi

Utani pembeni Masaju ni msomi kweli kweli wa sheria kama vile 'Mwaki Embe'! Hawa wasomi wakiwemo maprofesa wanaacha taaluma zao nje wanapoingia siasani. Sasa huyu masaju anajua fika kuwa yuko bungeni kwa kofia ya mwanasheria mkuu lakini keshajivika ukada wa mamlaka ya uteuzi. Huwezi tarajia la maana!
Historia haidanganyi baada ya muhula huu jina lake linajifuta kwani historia itamhukumu
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge(mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.
Hata akina Nyoka wenye makengeza walipitia njia hiyo hiyo!!
 
Povu linawatoka kwa sababu kaongea kitu ambacho hamkipendi kusikia, Kaka Mkuu wa cdm inatakiwa mda huu anasaidia polisi hakuna aliye juu ya sheria ndipo alioowakumbusha msemo wa mbowe sasa kelele za nn?
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge(mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.
Huyu siku zote anaegemea serikali.
Werema alikuwa anaegemea serikali hivyo hivyo ila ngoma ya escrow ikamuwia ngumu akacheua.
Hawanaga ushauri wowote wa kisheria hawa jamaa. Kazi kuleta siasa ktk sheria
 
Nahisi Magu hatakaa naye huyu maana ni jipu kubwa sana na ameonyesha uwezo mdogo kwa kulingana na kasi ya sasa
 
Ulishawahi kufanya nae kazi ...ukamfahamu kwa karibu...ama ni kelele mingi huku mitandaoni
Mtazame akiwa anaongea bungeni
Kama huwajua wanasheria anza mazoezi ya kuwafatilia then tofautisha mwanasheria na mbunge asiyekua mwanasheria utaelewa nasema nini
 
Ameegemea upande upi?unatokwa na makamasi kwa kusikia habari ambazo hupendi kuzisikia?
Uwe tu na uvumilivu wa kisiasa,Mbowe amesema hakuna alie juu ya sheria,ni lazima Mbowe akamatwe ili awasaidie polisi,kwa nini katibu wake myeka amepotea kazini halafu yeye anapanda ndege anakwenda ulaya kunywa mvinyo
Soma uzi kwa kuelewa, Masaju anaongea kama mwanasiasa anayetetea serikali sio kama mwanasheria mkuu wa serikali, alafu usijekudhani mimi nina chama cha siasa, wenye njaa ndo wanahangaika na hivyo vyama vya kinafiki mara chadema mara ccm kwangu hilo hakuna, kipato changu kinanifaa nikihitaji pesa ntatafuta kwingine sio chadema, ccm au CUF na vyama vingine vya kipuuzi puuzi kujazana unafiki tu.
Uzi wangu unazungumzia mwanasheria mkuu huyu hapaswi kuegemea ccm wala chadema ndio maana nazungumzia.
Angekua mwanasiasa wa ccm au chadema au chama chochote usingeona naandika uzi hapa.
 
Povu linawatoka kwa sababu kaongea kitu ambacho hamkipendi kusikia, Kaka Mkuu wa cdm inatakiwa mda huu anasaidia polisi hakuna aliye juu ya sheria ndipo alioowakumbusha msemo wa mbowe sasa kelele za nn?
Mimi sihusiki na chadema wala ccm njaa zenu ziendekezeni nyinyi tu sio kila mtu.
Chadema wapuuzi tu ccm nao wapuuzi tu hakuna mwenye afadhari ukienda CUF nako profesa analilia ugali, wale akina Zitto nao njaa kali alafu mimi nishabikie siasa ili iweje kwa mfano?
 
Wakuu kama mnafuatilia mijadala ya bunge kuna jambo linashangaza, huyu mwanasheria mkuu wa serikali Bw. George Masaju mbona amevaa sura ya ubunge(mwanasiasa) kuliko sura ya utumishi wa umma.

Nasema hivi kwa sababu sheria ya utumishi wa umma inamtaka mtumishi asiegemee upande wowote wa chama cha siasa lakini huyu Masaju ukimuangalia anaongea kiushabiki wa chama cha siasa.

Hii ni hatari kama tumefikia huku, alafu nimejikuta namshusha heshima zake kutoka 100% mpaka 0%.
Mungu anisamehe kwa mtazamo huu.
Ili hii nchi ipige hatua ni lazima ama ccm ibadir mifumo ya kuongoza nchi au sera ya wagombea binafsi ifanye kazi ili tusiwe na uccm na uchadema bungeni
 
mkuu kwani wewe hujui kuwa hao vigogo woote huko serikalini wana kadi za ccm...

kuanzia jaji mkuu, mkuu wa majeshi, IGP, Makamanda wa polisi mkoa, wakuu wa mashirika na taasisi za serikali nk...

Wote hao wana kadi za CCM
 
Inawezekana anaakili lkn kwenye kupangilia maneno aongeapo changanya na ile sauti yake kwakweli hashawishi kabisa...anakuwa Kama yule mbunge flani wa chadema bunge lilopita sijui prof. Kaige?! mhaya flani ivi. Huyu huwa anaongea Kama ananung'unika!!
 
Ulitegemea aweje wakati amewekwa na chama chake, ni lazima akitetee, suluhisho hapa ni katiba mpyaa.
 
Kilichomuwepa pale ni UKANDA na sivingnevyo kwa maana kichwani ni empty space
Namkumbuka Tundu Lissu wakati wa kujadili ripori ya Escrow, alisema Masaju hawezi kuwa mshauri wake wa kisheria, kwa sababu ni "mweupe" sana kwenye anga hizo za sheria.
 
Back
Top Bottom