Huyu mtu tupo pamoja?

Samahani jamani inaonekana nimeandika kwa ufupi sana,ni ngumu kueleza kila kitu. ndugu zangu wanakuja ila hawafiki ninapoishi wanapiga simu tunakutana sehemu walipo,kaka zangu walishakataa siku nyingi kuja ninapoishi,mdogo wangu wakike ndo wanafahamiana zaidi maana alikuwa anasoma mkoa tunaoishi alikuwa akija kunisalimia lakini kwa sasa hata yeye kasema haji tena maana anaona aibu maisha tunayoishi.mtoto wa pili nilijifungua kwa operation dada zangu waliniuguza kwa sharti nikae kwa dada sio kwangu. alikuwa anakuja kuniona kwa dada na huduma zote muhimu anatoa, ndugu zake ninao wajua ni binamu yake na mtoto wa dada yake ambao walikuja kwa sababu walikuwa wanasoma mkoa tunaoishi.kwetu kukiwa na tatizo au sherehe najifungasha mwenyewe naenda, ya kwao haniambii labda iwe bahati mbaya nimsikie akiongea kwenye simu .nishawahi kumwalika dadake alinambia atakuja bahati mbaya muda mrefu anaugua.
 
Tena nakushauri usiondoke hata kidogo kwa jinsi anavyoonekana mwehu, ukiondoka ujue watoto utalea peke yako, komaa naye mbona ni mume wako huyo tayari.
 
siku zote nilikuwa nafikiri kama unavyosema, na nilijali zaidi kuwa pamoja na tulee watoto pamoja, lakini siku zinavyozidi vituko vinaongezeka mfano ndo huo kila siku anaongea na huyo dada ambaye mwazo alinidanganya ni dada warafiki yake lakini kumbe aliwahi kuwa na mahusiano nae ambayo naamini yanaendelea ingawa yeye anapinga.alipojua nafuatilia basi ndo kila siku mara 2 au 3 lazima ampigie na wanaongea zaidi ya dakika kumi. bahati mbaya sijui vizuri lugha yao na akiniona karibu anaongea kwa kikwao. kuna siku mtoto anaumwa lakini aliondoka kwenda muziki akarudi saa kumi usiku eti mkizidiwa nipigie nitakuja.
 
duh shosti hapo jiongeze..cgapa lapa mapema kabla hayajakukuta makubwa. Ipo siku utaletewa mke mwenzio hapo. Lakini dearest,ulianzaje kuishi na mtu msizejuana kiasi hiki? Je hao watoto wenu watawajuaje ndugu zao?bibi na babu zao kwa mfano?
 
Changa la macho hilo dada kaa chonjo
Alikosea tokea mwanzo ilibidi ambane afunge ndoa, sasa saizi ameshakuzalisha kisha anapiga dana dana. Anaweza kuitumia loopwhole hiyo kuwaghiribu wanawake wengine kuwa atawaoa kwa kigezo kuwa hajafunga ndoa. Harusi siyo kipato chake pekee bali ni michango toka kwa ndugu na marafiki, yeye akijiandaa kwa 1.2 akaanzisha kamati yaani bonge la harusi linaweza kufanyika. Umezubaa sasa ukikuta mwana si wako huna wa kumlaumu. Tafakari chukua hatua.
 
For the sake of the children ni muhimu wafahamu ndugu zao. Inabidi wewe mwenyewe upange mkakati, kama unawasiliana nao kwa simu basi either uwakaribishe kwenu au wewe uende kwao na watoto.

Huyo dada anayewasiliana naye ni mpenzi wake, hata wewe utakuwa unajua hilo ila unataka reassurance kutoka hapa jamvini...

Kabla ya kung'ang'ania ndoa rasmi na huyo mwanaume juilize sana kama unataka kweli kuolewa naye. Mwenendo wake unaridhika nao, familia yake ni ya aina gani, malengo yake/yenu ya maisha ni yapi? Inasikitisha, wakati mwingine mtu anaingia kwenye ndoa akijua kabisa it wouldn't work... Think very carefully.
 
Hilo swali lingekua rahisi kujibu kabla hujazaa wawili. Sasa mmesha kaa pamoja kwa miaka 4 na mnawatoto wa2, basi mko pamoja. na hata kama inaonekana kuna kasoro, itabidi mkaee na mrekebishe pamoja.
Wewe kama wewe unataka nini? Unataka ndoa ao unataka tu muendelee kuishi pamoja? pia jiulize kitu kingine: kama mliweza kuishi kwa miaka yote bila familia, do you need them leo?
Umesema unaongea na familia yake but nani hasa? kama ni kaka zake ao dada zake, ni tofauti sana na kuongea na baba yake. hii pia inaweza kua alama ya kujua mwenzio anachukulia vipi uhusiano wenu.
Kwa leo huna haki ya kumkataza kuongea na ex wake maana we mwenyewe hujui uhusiano wenu ni nini. ukute yule ndio official, we ni mpango wa kando tu, sasa vita ya nini?
Jua kwanza wewe unataka nini na unasimamia wapi kabla ya kuongea na mwenzio.
 
Alikosea tokea mwanzo ilibidi ambane afunge ndoa, sasa saizi ameshakuzalisha kisha anapiga dana dana. Anaweza kuitumia loopwhole hiyo kuwaghiribu wanawake wengine kuwa atawaoa kwa kigezo kuwa hajafunga ndoa. Harusi siyo kipato chake pekee bali ni michango toka kwa ndugu na marafiki, yeye akijiandaa kwa 1.2 akaanzisha kamati yaani bonge la harusi linaweza kufanyika. Umezubaa sasa ukikuta mwana si wako huna wa kumlaumu. Tafakari chukua hatua.

Huyu dada hajakosea na pia kumlazimishia mtu ndoa si kitu kizuri, kibali cha ndoa kinatoka kwa mungu japo waweza lazimisha na ukafurahia kwa muda mfupi sana then after kipidi kidogo ukaiona hiyo pete kama kitanzi. Anatakiwa kumshukuru mungu kwamba, haya yote yanayotokea yamempata akiwa hajafunga nae ndoa. Huyo mwanaume na familia yake wote akili moja na hawamtaki dada wa wawatu. Cha muhim afanye utaratibu wake wa maisha mapya kwani wanaume wa hivyo hua hawabadiliki mpaka yakamshinde huko ndo arudi kwa magoti.
 
wewe nawe ulikuwa mzembe,mpaka unazalishwa watoto wawili hukumgundua tu kuwa huyo kaka hana interest na wewe?au na wewe ndio wale wenzetu wachache wanaoota kuolewa hata kama limtu halifai?kwa kifupi huyo kaka hakupendi na ndugu zake pia wanajua hilo,endelea kukaa naye for the sake of your children ila ujijue hauko peke yako!....kama kipato kinaruhusu i mean unaweza kujikimu kulea watoto mwenyewe then achana naye asije kukuletea magonjwa ndani,otherwise kama utaamua kukaa naye jua hatobadilika na hivyo ukae nae kiakili...mnh pole sana.
 
Pole ila hapa bwana kuna kila dalili za hatari ipo mifano mingi ya watu wenye matatizo kama yako.Ni kweli wapo watu hawapendi harusi lakini atleast angekutambulisha kwa wazazi kama wapo na wewe kujitambulisha kwa wazazi wake.Huyo inaonekana anakwepa majukumu na alikutamani tu hakukupenda.Ila jamani ilikuwaje mmezaa mpaka watoto 2?ingekuwa 1 tungesema bahati mbaya na kwamba kabla kuendelea kuzaa mngeweka mambo sawa.Ushauri angalia usizalishwe tena kabla hakijaeleweka mtawatesa hao watoto.
 
KWELI NI AJABU SANA,Miaka 4 bila ya kuwajua nduguze wote mko tz..
Hata ile coincidence ya kugongana na ndugu yako hata mmoja haijawahi kutokea in 4 years?? Kwa hiyo katika miaka minne hujatembelewa na ndugu zako my dear?? au wakikutembelea yeye anajificha?? samahani kwa maswali mengi, nashindwa kuamini macho yangu...

Enewei, ngoja nitoe ushauri... huyu hataki kuoa, yeye hapo ameshafika, mambo ya harusi unayawaza we peke ako... for him everything is perfect just the way it is... Sidhani hata kama huko nje anasemaga anaishi na mwanamke, anaishiaga kusema "I have 2 wonderful kids", Ili siku akitaka kuoa, aoe mwingine, halafu aseme huyu nilizaa nae tu...
Labda muwe mnaishi huko maulaya...ila kwetu Tanzania, you guys are abnormal... mi naona inabidi muanze upya...yeye aje kwenu apajue, mtambulishe kwa wazazi..na yeye akupeleke kwao ukapajue... akikataa..basi mama inabidi utembee na amani ya bwana, maana huyo atakua hakutakii mema... akikubali kufanya hivi then tunaweza sasa kufikiria ndoa... to some pipo ndoa ni kuishi pamoja, so hapa italingana na makubaliano yenu... Ila bwana katambulishananeni kwa ndugu zenu, This is our culture... This is the way to go my dear!!!
 
binadamu tupo tofauti...
unapoongea na ndugu zake kwenye simu,kwa nini usiwaalike waje uwatambue?
wewe nani kakuzuia kuleta ndugu zako awaone???????

wapo watu wengi hawapendi harusi.........
sio wote wanaoitwa mke na mume walifunga ndoa rasmi ya kanisa au msikiti....

kwa ufupi nyinyi ni tayari mke na mume....
Ni kweli mbele ya sheria ya ndoa ni mke tayari ingawa cheti cha ndoa huna. Kuhusu ndugu wote nyie wasanii. Kwa sababu huwezi zaa watoto wanne halafu mseme ndugu zenu hawafahamiani, ina maana ikifika likizo kila mtu anaenda kwao? Au hamuendi hata likizo? Hebu walete ndugu zako uone atafanya nini ndo hapo utajua msimamo wake. Kama alikua anatafuta kifaa cha kutotoa watoto au mke.
 
Samahani jamani inaonekana nimeandika kwa ufupi sana,ni ngumu kueleza kila kitu. ndugu zangu wanakuja ila hawafiki ninapoishi wanapiga simu tunakutana sehemu walipo,kaka zangu walishakataa siku nyingi kuja ninapoishi,mdogo wangu wakike ndo wanafahamiana zaidi maana alikuwa anasoma mkoa tunaoishi alikuwa akija kunisalimia lakini kwa sasa hata yeye kasema haji tena maana anaona aibu maisha tunayoishi.mtoto wa pili nilijifungua kwa operation dada zangu waliniuguza kwa sharti nikae kwa dada sio kwangu. alikuwa anakuja kuniona kwa dada na huduma zote muhimu anatoa, ndugu zake ninao wajua ni binamu yake na mtoto wa dada yake ambao walikuja kwa sababu walikuwa wanasoma mkoa tunaoishi.kwetu kukiwa na tatizo au sherehe najifungasha mwenyewe naenda, ya kwao haniambii labda iwe bahati mbaya nimsikie akiongea kwenye simu .nishawahi kumwalika dadake alinambia atakuja bahati mbaya muda mrefu anaugua.
Pole sana dada yangu hizo ni changamoto za maisha, kila mmoja anazake. Nakushauri husiongeze mtoto mwingine kwa sasa, maana inawezekana huo mzigo wa watoto ni wako!Maishani ukipata tatizo na akiri inakomaa, matatizo mengine yanaweza kuisha with time lakini mengine ni ya maisha. Mtegemee Mungu na wewe binafsi pima kwa jinsi unavyomuona na uchukue maamuzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom