Huyu mtu tupo pamoja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huyu mtu tupo pamoja?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MAMAMO, Mar 11, 2011.

 1. M

  MAMAMO Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nashindwa nimwite nani, ila nibwana tumezaa watoto 2,tunaishi pamoja mwaka wa 4 sasa. sikujui kwao hakujui kwetu naongea tu na ndugu zake kwenye simu, lini tutafunga ndoa anadai akipata hela wakati huo anmshahara takehome zaidi ya laki 8,nami pia ninamshahara wanguzaidi ya laki 4. zaidi kila kukicha lazima awasiliane na dada mmoja mwazo alidai dada wa rafiki yake nilipombana akadai ni x-girlfriend wake.nikimwambia naondoka anajifanya hanielewi hataki ni ondoke.mpaka najihisi kuchanganyikiwa rafiki ndugu hawatuelewi.
   
 2. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Changa la macho hilo dada kaa chonjo
   
 3. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sasa mmewezaje kuishi miaka minne bila kujuliana familia zenu?we huogopi unaweza kuwa unaishi na jini?... Duh! Maajabu
   
 4. k

  kisukari JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,766
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  huyo si muoaji,anaona kila anapoutaka mchezo,upo.inabidi jaribu kujipanga mwenyewe maisha yako
   
 5. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,275
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  tena hili wala sio changa ni kokoto la macho
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  binadamu tupo tofauti...
  unapoongea na ndugu zake kwenye simu,kwa nini usiwaalike waje uwatambue?
  wewe nani kakuzuia kuleta ndugu zako awaone???????

  wapo watu wengi hawapendi harusi.........
  sio wote wanaoitwa mke na mume walifunga ndoa rasmi ya kanisa au msikiti....

  kwa ufupi nyinyi ni tayari mke na mume....
   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani mnakaa pamoja na mna mpaka watoto na sio mtoto alafu hupajui kwao?Na yeye hapajui kwenu?Sababu ya kutojulikana kwa pande zote mbili ni zipi?Nwy kama hamna sababu poleni maana sio tu mnapotezeana muda ila nawaonea huruma hao watoto zaidi!Labda kama ndugu zenu wako nchi nyingine,.zaidi ya hapo ni bora tu muachane mapema kama hamna mpango wakua pamoja kiukweli!
   
 8. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160

  Duh umenichekesha kweli
   
 9. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Kumbe una akili namna hii wewe kweli ni The Boss.

  Point sana umeongea aisee
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280

  dena upo?
  nilijua utasoma ndo maana nikajaza pointi...
  sasa iliyobaki ni kuleta posa kwenu lol
   
 11. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Hiyo posa nilivyokuwa naisubiri!!!???
  Yaani fanya hima mapema mori usijekwisha
   
 12. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #12
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana kwakweli. Inaonekana huyo ndugu amekuchoka, na anatafuta wa kufunga naye! Ongea naye ujue msimamo wake, kufunga ndoa sio lazima iwe ya sherehe kubwa!
   
 13. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #13
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ooh DA ulikua hujajua si the boss tu, bali mtaani anaitwa mzee wa wa busara?
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  jambo mamushka?
  missing you...
   
 15. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #15
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh, sipati picha, hata inakuaje hata ukijifungua kusitokee ndugu hata mmoja wa pande yako wala yake kuja kuona mtoto. What kind of life style is that, mh hata na wewe ndugu yangu inamaana huna ndugu, wote hamjielewi.:juggle:
   
 16. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #16
  Mar 12, 2011
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Chukua hatua haraka huwezi jua..mpaka sasa bado hujamfahamu vizuri jamaa
   
 17. s

  shosti JF-Expert Member

  #17
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  :lol::lol::lol: maana:hatari:
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Mar 12, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mna watoto sasa inabidi ujue upande wa pili wa familia
   
 19. L

  Leney JF-Expert Member

  #19
  Mar 12, 2011
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 315
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata ile coincidence ya kugongana na ndugu yako hata mmoja haijawahi kutokea in 4 years?? Kwa hiyo katika miaka minne hujatembelewa na ndugu zako my dear?? au wakikutembelea yeye anajificha?? samahani kwa maswali mengi, nashindwa kuamini macho yangu...

  Enewei, ngoja nitoe ushauri... huyu hataki kuoa, yeye hapo ameshafika, mambo ya harusi unayawaza we peke ako... for him everything is perfect just the way it is... Sidhani hata kama huko nje anasemaga anaishi na mwanamke, anaishiaga kusema "I have 2 wonderful kids", Ili siku akitaka kuoa, aoe mwingine, halafu aseme huyu nilizaa nae tu...
  Labda muwe mnaishi huko maulaya...ila kwetu Tanzania, you guys are abnormal... mi naona inabidi muanze upya...yeye aje kwenu apajue, mtambulishe kwa wazazi..na yeye akupeleke kwao ukapajue... akikataa..basi mama inabidi utembee na amani ya bwana, maana huyo atakua hakutakii mema... akikubali kufanya hivi then tunaweza sasa kufikiria ndoa... to some pipo ndoa ni kuishi pamoja, so hapa italingana na makubaliano yenu... Ila bwana katambulishananeni kwa ndugu zenu, This is our culture... This is the way to go my dear!!!
   
 20. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #20
  Mar 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  hana mpango wowote na wewe, keshakufanya kama kiwanda cha kufyetulia watoto, na hiyo kujifanya hataki uondoke ni vunga hana lolote huyo!
   
Loading...