Kipindi tunakutana tulikua tukiishi mikoa tofauti, kufahamiana kukazua usiku mmoja mrefu, kila mmoja akarudi alikotoka, baada ya mwezi nikasikia toka kwake anadai yu mjamzito, kipindi hicho sikua tayari kwa hilo, nikamjibu kua sina uhakika kama mimi ni mhusika maana ilikua only a one night stand, akakasirika akanambia anaitoa, i never heard from her ever again, nimekuja angalia fb page naona yupo na katoto, kazuri kweli, macho pua na masikio ni mimi waungwana, a copy of me, siku zikapita nikahama nikawa naishi mkoa anaoishi yeye napita mahali namuona kabeba mwanae, ananiona anakimbia na mwanae , washa moto gari mbio,hapokei simu zangu wal ahajibu sms, sipafahamu kwao, kila nikionesha watu picha hizo wanadai ni mali yangu, nikihesabu umri wa mtoto kwenye picha na umri tukio lililotokea kuna uhusiano nikahusika, nifanye nini..