Huyu mtoto ni wangu???

Huyu mtoto ni wangu???

rafikimkweli

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2013
Posts
349
Reaction score
121
Kipindi tunakutana tulikua tukiishi mikoa tofauti, kufahamiana kukazua usiku mmoja mrefu, kila mmoja akarudi alikotoka, baada ya mwezi nikasikia toka kwake anadai yu mjamzito, kipindi hicho sikua tayari kwa hilo, nikamjibu kua sina uhakika kama mimi ni mhusika maana ilikua only a one night stand, akakasirika akanambia anaitoa, i never heard from her ever again, nimekuja angalia fb page naona yupo na katoto, kazuri kweli, macho pua na masikio ni mimi waungwana, a copy of me, siku zikapita nikahama nikawa naishi mkoa anaoishi yeye napita mahali namuona kabeba mwanae, ananiona anakimbia na mwanae , washa moto gari mbio,hapokei simu zangu wal ahajibu sms, sipafahamu kwao, kila nikionesha watu picha hizo wanadai ni mali yangu, nikihesabu umri wa mtoto kwenye picha na umri tukio lililotokea kuna uhusiano nikahusika, nifanye nini..
 
Wewe si umekataa ujauzito?Kinachokufanya umtake huyo mtoto sasa ni nini?Kwani wewe unataka ufanye nini?
kwa kipindi kile haikua rahisi under the circumstances, ila kama nahusika kwanini akimbie asijibu simu wala sms?? nahisi nahusika, kama nahusika kuna ubaya kukutanishwa na damu yangu??
 
kwa kipindi kile haikua rahisi under the circumstances, ila kama nahusika kwanini akimbie asijibu simu wala sms?? nahisi nahusika, kama nahusika kuna ubaya kukutanishwa na damu yangu??
Suala sio unahisi unahusika,UNAHUSIKA na alishakujulisha hilo ukakataa ujauzito!Kwanini ukutanishwe sasa na ulikataa jukumu tangia mwanzoni?Unajua amepata shida kiasi gani kulea ujauzito na mtoto wenu peke yake?Kusema kweli ana kila haki yakukata mawasiliano yote na ww!Unaujua uchungu wa mtoto wewe?
 
I thought people use condoms on their night stands,,,

Mh wenzio wanadai zinawaumiza,wengine wanadai hawawezi kula pipi na maganda,yaani wakati huo mimba wala magonjwa havikumbukwi ila one nite stand ikiisha ndo akili inawakaa sawa
 
Suala sio unahisi unahusika,UNAHUSIKA na alishakujulisha hilo ukakataa ujauzito!Kwanini ukutanishwe sasa na ulikataa jukumu tangia mwanzoni?Unajua amepata shida kiasi gani kulea ujauzito na mtoto wenu peke yake?Kusema kweli ana kila haki yakukata mawasiliano yote na ww!Unaujua uchungu wa mtoto wewe?
But she called to tell that anaitoa, nikajua its no more , mpaka kuja kuunganisha hizi habari, sasa hapo ningefanya nini tena??
 
Kukataa mtoto ni dhambi kubwa sana. Eniwei nakupa heshima kwa kulitambua hilo na kuamua kujirudi. Anachofanya huyo mwanamke na wanawake wa aina yake kuficha watoto kwa baba zao ni kosa kubwa pia kwa Mungu na mwana-adamu. Kila mtoto anastahili kumjua mama na baba yake. Wanawake dizaini hizo huwajaza watoto wao na chuki dhidi ya baba zao. Haistahili na ni kumtendea ubaya mtoto wako. Gangamaa na hakikisha unapata kumuona mwanao na kumpa matunzo yote kama baba. Ikiwezekana mchukue uishi naye ili apate upendo wa baba ambao ni muhimu sana kwa maisha ya mtoto. Huyo mwanamke msamehe tu ila kamwe usikubali akufarakanishe na mtoto wako.
 
Kama umejiridhisha kuwa huyo mtoto ni wa kwako. Tafuta watu wa kuongea na huyo dada. Uombe samahani na kuahidi kuwajibika kwake. Na kama unampenda na ikiwa bado hajaolewa mnaweza kubaliana kuanziasha familia. Kila la kheri mkuu
 
But she called to tell that anaitoa, nikajua its no more , mpaka kuja kuunganisha hizi habari, sasa hapo ningefanya nini tena??
Hujui yaloyojiri kwahio usikimbilie kumhukumu,aliamua kutoa kwasababu wewe hukuonesha ushirikiano na inawezekana ulimrubuni afanye hivo ,na ni dhambi kubwa sana kuua kiumbe!Astakafirullah
Labda watu wenye hekima na busara zao wamemshauri azae,ulitaka akushirikishe wewe kimpangilio gani wakati huna muamana wowote?
 
Tuliza ball rafikimkweli. Huyo mtoto si wako na ana baba yake anayemlea. Katafute wako na usijitie presha na kwenda kuharibu ndoa za watu. Ulishajifanya mjuaji ukakataa wakati unajua kabisa ulimla kavu kavu, unaambiwa mimba unadai eti mbona ni mara moja tu...simu za nini sasa? Tena umuombe Mungu sana isije ikawa kambegu kenyewe ndio kalikuwa kale kale.... BIG POLE.
 
Last edited by a moderator:
Suala sio unahisi unahusika,UNAHUSIKA na alishakujulisha hilo ukakataa ujauzito!Kwanini ukutanishwe sasa na ulikataa jukumu tangia mwanzoni?Unajua amepata shida kiasi gani kulea ujauzito na mtoto wenu peke yake?Kusema kweli ana kila haki yakukata mawasiliano yote na ww!Unaujua uchungu wa mtoto wewe?

Na hii ndio dawa ya wanaume wasiopenda kukubali mimba,unampa taarifa kua una mimba,akijifanya hausiki sijui unataka kumbambikizia wala hakuna kuhangaika nae unalea mimba af unamsubiri huyo mwanaume aje kudai mtoto ni wake,yan hata mimi ningekufanyia hivo hivo,kilichokufanya usiamini mimba ni yako ni nin?haukujua matokeo ya kufanya mapenzi bila kinga?tena amuache mdada wa watu alee mtoto wake
 
kwa kipindi kile haikua rahisi under the circumstances, ila kama nahusika kwanini akimbie asijibu simu wala sms?? nahisi nahusika, kama nahusika kuna ubaya kukutanishwa na damu yangu??

hakuna herufi ntakayoandika itakayoendana na adhabu unayostahili, hata hiyo ya kutopokea simu yako ni adhabu ndogo, hivi we unadhaqni ulipokua mazingira hayakuruhusu wewe kubeba jukum lako , ye ndio yalimruhusu au aliamua tu ajikaze asiue kiumbe, wanaume wengine bana
 
ulishamkataa tokea tumboni sasa nini tena jamani, mwache amlee mwanae akiona una umuhimu atakutafuta, though sidhani kwa sababu hajauona umuhimu wakati akiwa na ujauzito.

pili usije mwaribiha yawezekana amepata mtu wa kumbambikiza huyo mtoto, ka utamuoa endelea kumtafuta lakini kama shida ni mtoto tu mwache dada wa watu.
 
Mh wenzio wanadai zinawaumiza,wengine wanadai hawawezi kula pipi na maganda,yaani wakati huo mimba wala magonjwa havikumbukwi ila one nite stand ikiisha ndo akili inawakaa sawa
Mwanaume akiamua kutumia condom atatumia tu!!Kwani hajui ni jukumu lake akiambukizwa magonjwa au mwanamke akipata ujauzito??Wote wawili walikuwa irresponsible na yeye kukana mimba WONT JUSTIFY ANYTHING FOR HIM!!
 
Kama umejiridhisha kuwa huyo mtoto ni wa kwako. Tafuta watu wa kuongea na huyo dada. Uombe samahani na kuahidi kuwajibika kwake. Na kama unampenda na ikiwa bado hajaolewa mnaweza kubaliana kuanziasha familia. Kila la kheri mkuu
mkuu kila nikizitazama naona kama mimi mkuu, yaani pua, masikio na macho, kopi yangu mkuu, it happened kwa staili ambayo sina ukaribu na marafiki zake wala ndugu zake, ninayemfahamu ni yeye, kwao pia sipafahamu hakuwahi nielekeza..
 
Aendelee tu kukimbia tena aongeze speed maana hukutakiwa kumpa stress kwa wakati ule.
 
ulishamkataa tokea tumboni sasa nini tena jamani, mwache amlee mwanae akiona una umuhimu atakutafuta, though sidhani kwa sababu hajauona umuhimu wakati akiwa na ujauzito.

pili usije mwaribiha yawezekana amepata mtu wa kumbambikiza huyo mtoto, ka utamuoa endelea kumtafuta lakini kama shida ni mtoto tu mwache dada wa watu.

naweza kuhisi hivyo, ila ni vyema akaamua kuniambia ukweli ili nikae nikijua even if something happens i know mahali kuna trace yangu..naijumuisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom