Huyu mdada wa Dar atanifelisha michongo

Tangu mwaka uanze huu tuna ugomvi anataka biashara ya kufanya,kila saa yeye biashara tu na nyumba yangu anasema ni iuze tutafute kiwanja Dar tujenge yeye hawezi kuishi mikoani nyumba ipo location mbovu.

Hapa mahari nimepata lakini nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu huyu mwanamke, nina nia ya kumuoa ila anaonekana ana tamaa sana. Nampenda sana ila nahisi kukata tamaa kabisa.

Hizo paragraphs mbili zinajitosheleza kufanya maamuzi magumu sahihi.

Huna mchumba hapo ila umepata chuma ulete. Na ukimuoa tu, tarajia kufa kiuchumi kabisa na siku ukiishiwa atahama kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie huyo jamaa atoke nje ya nyumba yake ajipige pige Mikono kifuani huku akisema MIMI NI FALAAAAAA

dodge
 
Jifanye huna akili soon utapata unachotafuta

habari ya majukum wanajukwaa wenzangu, ni msichana ambae nimetumia muda mrefu sana kumpata tangu nikiwa sina kitu hadi sasa hivi angalau kidogo nasema nina uhakika wa matumizi ya kawaida ya kwangu na ya kwake pia.

Kwa mara ya kwanza nilionana nae Arusha mwaka 2017 nikiwa kwenye mishe mishe za kuhangaikia maisha yangu kwa maana kipindi hicho nilikuwa sina kazi rasmi ya kufanya kulingana na taaluma yangu niliosomea.

Nlimpenda sana nikavutiwa nae hadi nika fight kupata japo masaa mawili ya kuzungumza nae nimweleze ya moyoni. Ilikuwa ni moment ngumu sana kwangu kulifanikisha hilo ila nashukuru niliweza kuzungumza nae nikamfahamu kwa jina lake na akanipa namba yake ya simu.

Tuliendelea kuwasiliana ili kufahamiana zaidi na alinieleza kuwa yeye anaishi Dar Es Salaam ila Arusha amekuja tu kwa dada yake kumsalimia.

Niliendelea kukomaa nikamueleza kuhusu upendo wangu kwake na kama yupo tayari tuwe wachumba mambo yakiwa fresh tutafunga ndoa.

Alionekana kuwa mzito sana kutoa jibu akidai kwamba nimpe muda afikirie akipata muafaka mzuri atanifahamisha.

Kwangu haikuwa tatizo kusubiri japo changamoto iliyokuwepo alipunguza mawasiliano na kila nilipomkumbusha alijibu kwa ufupi sana kwamba mambo mazuri hayahitaji haraka kwa hiyo niliendelea kusubiri akiwa poa ataniambia.

Badae niliona kama atanipotezea muda nikaamua niachane nae niendelee na maisha mengine. Mwaka 2018 January nilifanikiwa kupata kazi kwenye taasisi moja ya private ambayo ndio nafanya kazi mpaka sasa hivi.

Maisha yali change kiukweli in positive way japo mshahara sio mkubwa kivile ila unatosha kutatua changamoto ndogo ndogo.

Hatukuwasiliana kwa muda mrefu sana ila mwezi wa tisa 2018 alianza kunitafuta whatsapp akidai amenimiss na ananipa hi tu.

Kwa akili yangu niliona nikomae nae tena nione muafaka unakuaje, hapo alikubali kuwa na mimi lakini tucheki time ya kuonana tuzungumze zaidi. Nikaona fresh haina shida tukapanga tuonane Morogoro japo alisita sita ila alikuja tukapiga story nyingi sana za life, nilikaa nae kwa siku tatu.

Katika vitu alivyoniambia moja nakumbuka alisema anatamani sana nikimuoa nimfungulie biashara ya kufanya, so long ni mipango ya badae hiyo haikuwa tatizo kwangu.

Baada ya hapo alirudi Dar na mimi nikarudi Arusha maisha yakaendelea. Miezi miwili badae alibadilika tena na kuwa kama mtu ambae anakosa time na mimi kila mara yuko busy na mambo yake, iliniuma sana lakini sikuwa na namna nikamuacha tu.

Uamuzi nilioufanya kipindi hicho ilikuwa kuachana na ishu za mapenzi kwanza nifanye mambo ya maendeleo. Nikatafuta kiwanja mapema 2019 nikaanza ujenzi wa nyumba ya kawaida ya kuanzia maisha ambao ulinichukua miezi nane mpaka kupiga bati.

Mwezi wa kumi 2019 alianza kunitafuta tena kwa fujo sana akidai kuwa anataka aje kupaona ninakoishi. Nilikubali aje ila kwa condition moja akija tucheki afya kwanza ndio mambo mengine yaendelee.

Alikubali yote lakini sasa alipokuja alikuja na begi la nguo kama mtu ambae anahamia kabisa. Tulicheki afya nashukuru mambo yalikuwa mazuri nikaamua tukae tu home tuendelee kuyapanga.

Alikaa mwezi mzima na wiki mbili tukapanga mambo mengi sana toka mwezi wa 10 mwishoni hadi mwezi wa 12 mwanzoni ila kilichonishangaza zaidi aliniuliza mara nyingi sana kuhusu mshahara wangu kazini anataka kujua nalipwa sh ngapi.

Tukapanga nicheki pesa ya mahari, ikikamilika niende kwao nikajitambulishe tuandae harusi ikiwezekana tufunge ndoa mwaka huu 2020 na biashara yake akija mara nyingine aikute.

Nilimueleza ukweli kwamba hivyo vitu kuwezekana kwa wakati mmoja ni ngumu sana na nikiangalia nipo kwenye ujenzi kwa hiyo avumilie tutafanya kimoja kimoja hadi vitakamilika vyote. Alinielewa akaondoka kiroho safi kabisa.

Tangu mwaka uanze huu tuna ugomvi anataka biashara ya kufanya,kila saa yeye biashara tu na nyumba yangu anasema ni iuze tutafute kiwanja Dar tujenge yeye hawezi kuishi mikoani nyumba ipo location mbovu.

Hapa mahari nimepata lakini nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu huyu mwanamke, nina nia ya kumuoa ila anaonekana ana tamaa sana. Nampenda sana ila nahisi kukata tamaa kabisa.

Tuna one week sasa hivi hatujawasiliana.
 
Huyo ni mzee wa fursa mkuu mwanzo aliona huna uelekeo akakuweka pending, sasa hv ameona uko njema ndo anajileta sasa ukitaka kuumia na kujuta maisha yako yote oa huyo manzi! Hajakupenda yuko kikazi zaidi.
 
Hivi umeshikiwa akili au, ipo wazi kabisa hamna muolewaji hapa ila unaomba ushauri

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kweli kabisa, tatizo jamaa yuko penzini nafikiri hata huu ushauri kwake, moyo unataka akili haitaki...
 
Tangu mwaka uanze huu tuna ugomvi anataka biashara ya kufanya,kila saa yeye biashara tu na nyumba yangu anasema ni iuze tutafute kiwanja Dar tujenge yeye hawezi kuishi mikoani nyumba ipo location mbovu.

Hapa mahari nimepata lakini nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu huyu mwanamke, nina nia ya kumuoa ila anaonekana ana tamaa sana. Nampenda sana ila nahisi kukata tamaa kabisa.

Hizo paragraphs mbili zinajitosheleza kufanya maamuzi magumu sahihi.

Huna mchumba hapo ila umepata chuma ulete. Na ukimuoa tu, tarajia kufa kiuchumi kabisa na siku ukiishiwa atahama kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
dah, so sad but no way.... acha ntulie tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom