Planett
JF-Expert Member
- Mar 20, 2014
- 10,561
- 16,339
habari ya majukum wanajukwaa wenzangu, ni msichana ambae nimetumia muda mrefu sana kumpata tangu nikiwa sina kitu hadi sasa hivi angalau kidogo nasema nina uhakika wa matumizi ya kawaida ya kwangu na ya kwake pia.
Kwa mara ya kwanza nilionana nae Arusha mwaka 2017 nikiwa kwenye mishe mishe za kuhangaikia maisha yangu kwa maana kipindi hicho nilikuwa sina kazi rasmi ya kufanya kulingana na taaluma yangu niliosomea.
Nlimpenda sana nikavutiwa nae hadi nika fight kupata japo masaa mawili ya kuzungumza nae nimweleze ya moyoni. Ilikuwa ni moment ngumu sana kwangu kulifanikisha hilo ila nashukuru niliweza kuzungumza nae nikamfahamu kwa jina lake na akanipa namba yake ya simu.
Tuliendelea kuwasiliana ili kufahamiana zaidi na alinieleza kuwa yeye anaishi Dar Es Salaam ila Arusha amekuja tu kwa dada yake kumsalimia.
Niliendelea kukomaa nikamueleza kuhusu upendo wangu kwake na kama yupo tayari tuwe wachumba mambo yakiwa fresh tutafunga ndoa.
Alionekana kuwa mzito sana kutoa jibu akidai kwamba nimpe muda afikirie akipata muafaka mzuri atanifahamisha.
Kwangu haikuwa tatizo kusubiri japo changamoto iliyokuwepo alipunguza mawasiliano na kila nilipomkumbusha alijibu kwa ufupi sana kwamba mambo mazuri hayahitaji haraka kwa hiyo niliendelea kusubiri akiwa poa ataniambia.
Badae niliona kama atanipotezea muda nikaamua niachane nae niendelee na maisha mengine. Mwaka 2018 January nilifanikiwa kupata kazi kwenye taasisi moja ya private ambayo ndio nafanya kazi mpaka sasa hivi.
Maisha yali change kiukweli in positive way japo mshahara sio mkubwa kivile ila unatosha kutatua changamoto ndogo ndogo.
Hatukuwasiliana kwa muda mrefu sana ila mwezi wa tisa 2018 alianza kunitafuta whatsapp akidai amenimiss na ananipa hi tu.
Kwa akili yangu niliona nikomae nae tena nione muafaka unakuaje, hapo alikubali kuwa na mimi lakini tucheki time ya kuonana tuzungumze zaidi. Nikaona fresh haina shida tukapanga tuonane Morogoro japo alisita sita ila alikuja tukapiga story nyingi sana za life, nilikaa nae kwa siku tatu.
Katika vitu alivyoniambia moja nakumbuka alisema anatamani sana nikimuoa nimfungulie biashara ya kufanya, so long ni mipango ya badae hiyo haikuwa tatizo kwangu.
Baada ya hapo alirudi Dar na mimi nikarudi Arusha maisha yakaendelea. Miezi miwili badae alibadilika tena na kuwa kama mtu ambae anakosa time na mimi kila mara yuko busy na mambo yake, iliniuma sana lakini sikuwa na namna nikamuacha tu.
Uamuzi nilioufanya kipindi hicho ilikuwa kuachana na ishu za mapenzi kwanza nifanye mambo ya maendeleo. Nikatafuta kiwanja mapema 2019 nikaanza ujenzi wa nyumba ya kawaida ya kuanzia maisha ambao ulinichukua miezi nane mpaka kupiga bati.
Mwezi wa kumi 2019 alianza kunitafuta tena kwa fujo sana akidai kuwa anataka aje kupaona ninakoishi. Nilikubali aje ila kwa condition moja akija tucheki afya kwanza ndio mambo mengine yaendelee.
Alikubali yote lakini sasa alipokuja alikuja na begi la nguo kama mtu ambae anahamia kabisa. Tulicheki afya nashukuru mambo yalikuwa mazuri nikaamua tukae tu home tuendelee kuyapanga.
Alikaa mwezi mzima na wiki mbili tukapanga mambo mengi sana toka mwezi wa 10 mwishoni hadi mwezi wa 12 mwanzoni ila kilichonishangaza zaidi aliniuliza mara nyingi sana kuhusu mshahara wangu kazini anataka kujua nalipwa sh ngapi.
Tukapanga nicheki pesa ya mahari, ikikamilika niende kwao nikajitambulishe tuandae harusi ikiwezekana tufunge ndoa mwaka huu 2020 na biashara yake akija mara nyingine aikute.
Nilimueleza ukweli kwamba hivyo vitu kuwezekana kwa wakati mmoja ni ngumu sana na nikiangalia nipo kwenye ujenzi kwa hiyo avumilie tutafanya kimoja kimoja hadi vitakamilika vyote. Alinielewa akaondoka kiroho safi kabisa.
Tangu mwaka uanze huu tuna ugomvi anataka biashara ya kufanya,kila saa yeye biashara tu na nyumba yangu anasema ni iuze tutafute kiwanja Dar tujenge yeye hawezi kuishi mikoani nyumba ipo location mbovu.
Hapa mahari nimepata lakini nina wasiwasi mkubwa sana kuhusu huyu mwanamke, nina nia ya kumuoa ila anaonekana ana tamaa sana. Nampenda sana ila nahisi kukata tamaa kabisa.
Tuna one week sasa hivi hatujawasiliana.
Ok ok ni kweliHakuna mwanamke hapo
Endelea na maisha yako
Kweli mkuu hapa nmeona nimkaushiee
Huyo asepe, ni dana danaa sanaHapo Kaka inaonekana wewe ni miongoni mwa wanaume wanateswa na mapenzi! Kwa ninavyojua mimi mwanamke akipenda haweki Conditions
Hapo bila shaka ukimuacha itakuwa heri kwako kuliko kuendelea kumfuatilia
Jambo la kukupongeza umeamua kujenga ulivoona mapenzi sio kipaumbele ila saizi unayumba kutaka umuoe mwanamke kama huyo.
Yeye anadai hawezi kuishi nje ya Dsm inamaana kuna shughuli za msingi anafanya Dsm bora kuliko wewe na kazi yako ya huko Arusha.
Hivyo ili uwe nae inakubidi uache kazi uje Dsm ndio utaweza kuwa nae kisha umfungulie Biashara usipotimiza masharti humpati hapo huna mwanamke.
Mwanamke mwenye akili angekubali kuja Arusha maana unaonekana kumpenda angekaa kwako ungemfungulia biashara hata mkiachana anajua biashara anabaki nayo
Huyo ana wake huko sema muda haujafika, acha kuforce vitu kaka yangu, kimbia kama ulikuwa naye kimasihara na nyuma usigeukeAsntee sana. Na mm nahisi hivo atakua na mipango yake labda
Haha kimasihara sioHuyo ana wake huko sema muda haujafika, acha kuforce vitu kaka yangu, kimbia kama ulikuwa naye kimasihara na nyuma usigeuke
Kabisa watu tunatofautiana uelewa sana, anajua kabisa hali ya kimaisha saizi, mtu kujenga ni dream come true, yeye analeta upumbavu.Unajua kuna baadhi ya wanawake ni mashetani?,huyo anaweza akakushauri uuze hio nyumba akatafuna hio hela makusudi akiona umeyumba tuu anapita hivi bila soni yyoyote,yaan kimbiaaaaa kabisa hapo,mm nashukuru Mungu kuna ngema ilikuwa kama hiyo yako ilikuwa imejitega mahali inaangukie lkn nashukuru Mungu ameniokoa man
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamani si mnafisiana hapa kula kimasihara na kusepa au siyo nyinyi.Haha kimasihara sio
Dar sijui kuna tatizo gani, tamaa sana hukoKabisa watu tunatofautiana uelewa sana, anajua kabisa hali ya kimaisha saizi, mtu kujenga ni dream come true, yeye analeta upumbavu.
Mtu badala achangie mawazo chanya analeta upuuzi, apite kushoto
Sio mm bhana, naona vijana wanakula kimasihara na wanasemaJamani si mnafisiana hapa kula kimasihara na kusepa au siyo nyinyi
MUOEKivip Mkuu cjakuelewa..
Hahaa hewa mbovuHio mahari ipeleke kwenye ujenzi huna mke apo. Una chuma ulete.
Kuna mtu wa karibu kaoa kidada cha dar kinampelekesha balaa na mkoani hakitaki hata kuja kusalimia eti hewa mbovu![]()
Mkuu nimeghairiMUOE
Right kabisa, hamna haja kupoteza time kwa mtu ambae hana shukraniTatizo Moyo!!
Ila bro you must grow up!!
Wanawake wapigaji wapo wengi sna,, focus on your goals!
Nina uhakika utampata wa kuendana nae !
Punguza vigezo sna,, angalia Mtu mwenye upendo na wew ,, am sure wapo!
And everything will be ok!
Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kichwa ngumu kuelewa eti? Mtu hamjaoana anakomaa ajue mshahara wako, anakukomalia umfungulie biashara zaidi ya yote uuze mjengo wako eti mkajenge Dar yeye hawezi kuishi mikoani. Bado unakuja JF kuomba ushauri, unashauriwa bado unajifanya huelewi. Dah sikio la kufa.Kivip Mkuu cjakuelewa..