Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
Mh. Madam speaker, kwa kuwa serikali yetu inaajiri wanajeshi kila mwaka, na kwa kuwa hakuna kitu wafanyacho zaidi ya kula na kukimbizana na raia. Na kwa kuwa serikali yetu inanunua silaha kila mwaka na silaha hizo hazitumiki ipasavyo na kwa wakati na hatimaye kuharibika na kudhuru raia kama ilivyotokea Mbagala na G'mboto. Je serikali haioni umuhimu wa kukodisha wanajesh wetu ili tupate nyongeza ya pato la kigeni? Na je, serikali haioni umuhimu wa kuomba vita vya kirafiki na jirani zetu ili kuchangamsha wanajeshi wetu na kutumia silaha ili zisilipuke ovyo?