Huyu kaka hataki tuachane, nifanyaje?

Huyu kaka hataki tuachane, nifanyaje?

Niko kwenye mahusiano ambayo kiukweli siyafurahii hata kidogo, huyu kaka ananipenda ila kuna tabia zake za kuwasiliana na wanawake naamanisha akipigiwa simu namba huwa anafuta na mimi ni bonge la mpekuzi.

Isitoshe siku ya J2 ya wiki hii anakuja kutoa mahari na kunivisha pete na nilishamwambia kuwa tuachane hataki.

Nifanye nini ili tuachane na sina mpango wa kuja kumzalia mtoto, na siku ya jana niliamua kumsaliti na mwanaume wangu wa utotoni.

Nilimpa taarifa kuwa naenda kulala na mwanaume mwingine baada ya kuona huyo dada akimpigia simu then akaja kumzimia baada ya kuona ugomvi ukaanzia hapo.

Naombeni mnishauri lengo langu ni kuachana naye ila yeye hataki tuachane, nimfanyie kitu gani kitakachomuumiza moyo wake mpaka anyooshe mkono juu asepe aende zake.
Ungekuwa humpendi usingemruhusu aje kwenu kujitambulisha hadi kufikia hata ya mahsri

Huu ni uongo dhahiri kabisa. Acha kudanganya watu
 
Back
Top Bottom