Poleni wafiwa hasa familia zilizoguswa moja kwa moja na msiba huu. Poleni viongozi wa CHADEMA ambao tukio hili la mlipuko wa bomu la kutupwa kwa mkono(kwa mujibu wa Waziri Nchimbi kupitia gazeti la Mwananchi la leo tarehe 17/06/2013) lilitokea baada ya kumaliza mkutao wenu wa hadhara. Poleni watanzania wote (na mimi nikiwemo) mnaopenda amani , umoja,utulivu na mshikamano wa kijamii usiobagua kundi moja dhidi ya lingine ndani ya jamii.
Matukio haya hayakubaliki kabisa.....kwa mujibu wa Mh. Mbowe ni kuwa tukio hili liliwalenga wao (rejea gaeziti la mwananchi la leo). Mh. Mbowe ana haki ya kusema haya kwani lilitokea katika eneo ambalo alikuwa yeye.
Hata hivyo binafsi si jamuelewa Mh. Nchimbi ( Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi)na kauli yake ya kuwa hakuna yeyote aliyekamatwa na wanaendelea kuchunguza kujua mlipuko ule ulikuwa wa aina gani.
Hivi ilikudhibiti matendo haya ya kulipua mabomu na kuua raia unatakiwa kuchunguza aina ya mlipuko au unachunguza aliyepanga na kulipua bomu hilo ilipelekwe kwenye vyombo vya sheria kwaajili ya kuhukumiwa?
Swali ninalojiuliza hapa hivi ni kwa nini matukio haya (kulipua mabomu) yanatokea wakati tuna mijadala mizito nchini juu ya:
1. Rasimu ya katiba mpya....ambayo bado imeleta mkanganyiko juu ya namna ya muungano.
2. Bajeti ya Serikali ya mwaka 2013/2014 ambayo imeutwa majina mengi kama majanga, maumivu, katili, n.k