Huyu dada simwelewi kabisa..!

mjasilia

JF-Expert Member
Aug 25, 2012
594
172
Kuna mdada mmoja tuliwahi kuwa wapenzi kwa kipindi kifupi sana. Siku moja tukapishana kiswahili akajifanya kuzila akawa hapokei simu zangu. Nilimbembeleza sana lakini akawa mugumu sana kunielewa.

Kiukweli upendo wangu ulikuwa juu sana kwake, baada ya kuona hataki tuyamalize niliumia sana nikaona nimtolee uvivu nikamtukana matusi ya lejaleja kujipunguzia maumivu ya kukataa kunisamehe yaishe.

Tulikaa miezi kama mitano nikawa nimemsahau kabisa maana nilipata kidemu kingine cha kuzugia kwa muda tuu, sasa juzi kati ghafla nikaona txt yake, anafanya kazi nje ya nchi nikamjibu nikajua hapa kajirudisha tukaanza kuchati nilipomuita mpenzi akabadirika na kuanza kuninunia tena.

Nikamuuliza labda mwenzangu umeisha ingia kwenye uhusiano akagoma kwamba bado yuko single nikashangaa sana. Kila nikimuomba turudiane hataki ila sasa nikimwambia basi tuache mawasiliano maana ananiumiza nikimuona nampenda ila hapendi tuwe wapenzi hataki pia.

Kiukweli nimemwambia asitegemee mimi anaweza kunigeuza kaka yake kutoka mpenzi wake nikamwomba basi tuachane na tupotezeane hataki pia anasema mimi ni mtu ambaye hawezi kunipoteza kirahisi simwelewii simwelii etii..!

Nisaidieni anataka nini kwangu huyu, huwa kuna wakati anatumia njia ya kujidai ananiazima pesa kidogo ili mradi apate upenyo wa kunikaribia maana ananiudhi mpka namchunia sana sometime..!

Nimfanyeje huyu mdada mkorifi hivi anapendwa afu anazingua ni mtu wa singida bonge la kitu aisei...
 
Ndiyo nini?
Tafuta Wimbo Wa Mrisho Mpoto Utaelewa

Ama Sikiliza E Fm Kipindi Cha Uhondo
Kuna Kibwagizo Kinasema Hivi:-
Sijui Kaenda Kwa Mganga Gani!!
Amenifunga Nisitoke Ndani X 2

Chorus
Uhondooo!!
Uhondoo!!!
 
Tafuta Wimbo Wa Mrisho Mpoto Utaelewa

Ama Sikiliza E Fm Kipindi Cha Uhondo
Kuna Kibwagizo Kinasema Hivi:-
Sijui Kaenda Kwa Mganga Gani!!
Amenifunga Nisitoke Ndani X 2

Chorus
Uhondooo!!
Uhondoo!!!
Hahahah! Haya bwanah..!
Kwangu siendi kwa mfanga nitamtolea uvivu siku moja..!
 
Inaonekana wewe ndo hueleweki kwake... anakuona bado una mambo ya kitoto lakini pia anategemea ipo siku utamwelewa na maisha yataenda vizuri. Fanya kupunguza kuwasiliana naye...akikutext jibu hata baada ya siku 2 au wiki. Taratibu ukweli utajulikana!!
 
Kuna mdada mmoja tuliwahi kuwa wapenzi kwa kipindi kifupi sana. Siku moja tukapishana kiswahili akajifanya kuzila akawa hapokei simu zangu. Nilimbembeleza sana lakini akawa mugumu sana kunielewa.

Kiukweli upendo wangu ulikuwa juu sana kwake, baada ya kuona hataki tuyamalize niliumia sana nikaona nimtolee uvivu nikamtukana matusi ya lejaleja kujipunguzia maumivu ya kukataa kunisamehe yaishe.

Tulikaa miezi kama mitano nikawa nimemsahau kabisa maana nilipata kidemu kingine cha kuzugia kwa muda tuu, sasa juzi kati ghafla nikaona txt yake, anafanya kazi nje ya nchi nikamjibu nikajua hapa kajirudisha tukaanza kuchati nilipomuita mpenzi akabadirika na kuanza kuninunia tena.

Nikamuuliza labda mwenzangu umeisha ingia kwenye uhusiano akagoma kwamba bado yuko single nikashangaa sana. Kila nikimuomba turudiane hataki ila sasa nikimwambia basi tuache mawasiliano maana ananiumiza nikimuona nampenda ila hapendi tuwe wapenzi hataki pia.

Kiukweli nimemwambia asitegemee mimi anaweza kunigeuza kaka yake kutoka mpenzi wake nikamwomba basi tuachane na tupotezeane hataki pia anasema mimi ni mtu ambaye hawezi kunipoteza kirahisi simwelewii simwelii etii..!

Nisaidieni anataka nini kwangu huyu, huwa kuna wakati anatumia njia ya kujidai ananiazima pesa kidogo ili mradi apate upenyo wa kunikaribia maana ananiudhi mpka namchunia sana sometime..!

Nimfanyeje huyu mdada mkorifi hivi anapendwa afu anazingua ni mtu wa singida bonge la kitu aisei...

Aisee we hiyo kama mimi vileeee!
 
Wewe ndio hueleweki, kwanini akikupigia na ukamjua ni yeye usikate au upokee lakini usimjibu unamuacha hewani tu anaongea mwenyewe na akituma sms usijibu .............. ukifanya hivi sijui kama ataendelea.
 
1464428403271.jpg
 
Sasa unataka ushauri gan labda???!wakati unajua wazi hakutaki na hakupendi!!
 
Jaribu hii. Jifanye ume-move on na una kitu mpya, hata kama si kweli. Unatupia picha nini, na kumsifia kiaina kila unapokuwa kwenye mawasiliano na dear ex. Ukifanya hayo, na bado akaendelea na msimamo wake, then kubali tu matokeo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom