Ilibidi harusi ifanyike leo ila kutokana na bibi harusi kushinikiza vitu ambavyo vipo nje ya uwezo wa bwana harusi sherehe na ndoa vimeahirishwa. Bibi harusi amekataa Ukumbi (hauna hadhi), Keki ya bei ndogo, Wasimamizi sijui amewaona walugaluga, Gari pamoja na salon ya kumpamba vyote amesema vipo chini ya kiwango.
Tangu Jumatano wanafanya vikao vya kumbembeleza ila haelewi kitu wala hajibu kitu hadi atimiziwe haja zake. Ndugu wa bwana harusi wameshauri kijana aachane na binti na mahari asahau ila kijana hajatoa msimamo zaidi ya kuahirisha harusi.
Kijana ni mwalimu shule ya private na binti ana degree ya ualimu ila hana kazi. Wamesoma darasa moja na bwana harusi wakamaliza 2017.
Nimeongea na kaka wa bwana harusi nikamwambia "HUYO BINTI NI MUUAJI".