Huyu dada leo kanichana ukweli

Huyu dada leo kanichana ukweli

Ndugu zangu itabidi mnielekeze wapi napata Pafyum a.k.a Unyunyu wa kushantoo. Kilichonipata leo kimenibadili.

Kama kawaida leo jioni natoka maskani naingia mtaa kidogo- lengo kunyoosha misuli, kupunga upepo na kutazama uumbaji nitakao kutana nao.

Nikakutana na huyo binti, mzuri kawaida, kapendeza zake.
Nikawaza kwanini nisifanyie mazoezi uwezo wangu kutongoza niliofundishwa na Mwalimu wangu, Jacksonian.

Basi nikamsogelea binti wa watu,. Salamu, kisha blaablaa kadhaa (ambazo huwa hatuzikumbuki hata tulisema nini).

Binti alikuwa anaonesha ushirikiano wa kawaida, kama ilivyokawaida yao.

Basi nikaona nisipoteze muda ngoja niamie kwenye kile kipengele muhimu zama hizi( kuomba namba).
Nilivyomuomba tuu namba, binti akafikiria kama dakika 1.
Ile nataka kufungua mdomo ili nikazie zaidi.

Ghafra binti akasimama, kama vile kasahau kitu. Akaniuliza unaitwa nani rafiki, nikamjibu kama vile sikumwambia hapo awali.

Akaanza "MaT2B unatumia pyafum gan?" Nikajifnya kuuliza mbona mimi sijapulizia leo pafyum."
Yeye: Why?
Mimi: Nimetoka kuoga sasa hivi, sijaona haja ya kupulizia.

Yeye: No, no. Tafuta pafyum nzuri, the next day you approach a lady, make sure unanukia harufu nzuri ya pafyum. Itakuongezea point, mvutie mtu kwa harufu yako.
Mimi: ..........

Yeye: and I don't mean unanukia vibaya, no, sijanusa harufu yoyote kutoka kwako.

Mimi: But sio kwamba huwa sijipulizi ila nimependa tuu kuwa out of pafyum leo.

Yeye: ok you gotme, and am sorry, taken already. Do what i told you en you will find a beautiful lady.

Nikawa sina neno, nikamwambia Ok goodnight.

Nikabaki kumuona mtoto mzuri ana ambaa ambaa huyo.

Kwa fedheha niliyopata, nikaamua haraka nimpigie demu angu, Jesca. Hajali haya mambo. Kwanza kale la body spray kangu huwa anang'ang'gana nimnunulie na yeye.

Ila wakuu nipeni jina la pafyum nzuri kwa hela yangu isiyozidi 30K. Sina gari, hata kunukia vizuri nisinukie kweli?
Hakuna perfume nzuri ya bei hii
 
Nauza Oil Based Perfumes aina mbalimbali, Best Quality, Long Lasting, Free Delivery. Bei zetu ni 25k (30ml), 35k (50ml), 55k (100ml). Atakayehitaji anicheki inbox.
 
Wewe Saint Anne
Natafuta hiyo Spray ya Aventos.
Huwa inauzwa pamoja na perfume yake ama naweza ipata peke yake.

Duka niliponunua Aventos perfume walisema eti hawana Spray yake.
Aventos perfume Ina spray yake ndani
Yani set yake ni perfume na spray ndani.
Spray pekeyake hakuna
IMG-20230127-WA0013.jpg
 
Sio zote mkuu, inategemea unanunua kwa nani, hizi perfumes za kuchanganya zimevamiwa na watu ambao hawana ujuzi wowote ndo hao wanaharibu industry. Njoo nunua hizi za kwangu scent ikibadilika kama ulivyosema nakurudishia hela yako.
Upo wapi

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Kabla ya yote hakikisha unatumua kitu kinaitwa shower to shower deodorant. Unapakaa huwa inakata hali ya jasho na inanukia bomba sana. Ukijazia na perfume mambo yanakuwa mchubuyu!
 
Pole sana Mkuu kwa fedheha

Njoo nikuuzie perfume kwa 25k tu.
Zipo nyingine 15k oil perfumes.

Anza na Black Opium,
Chukua Creed Aventus
Chukua Mousuf.
Chukua Sauvage
Chukua Invictus.

Hizo ni Basic ati ambazo mwanaume hutakiwi kukosa .
Nimezipanga kwa preference yangu.

Ukiwa nayo moja katika hizo hakuna mtu atakuchomolea.
Noma sana!
 
Back
Top Bottom