Huyu dada leo kanichana ukweli

Huyu dada leo kanichana ukweli

Siku hizi Kuna hata za kupima tu unapata Kwa bei cheese kulingana MLS unazotaka na kipato chako. Sio lazima uchukue mls kubwa za bei ghali. Tafuta za mls ndogo Kwa bei ndogo afu fanya cocktail. Utanipa majibu

Wewe tena
 
Ndugu zangu itabidi mnielekeze wapi napata Pafyum a.k.a Unyunyu wa kushantoo. Kilichonipata leo kimenibadili.

Kama kawaida leo jioni natoka maskani naingia mtaa kidogo- lengo kunyoosha misuli, kupunga upepo na kutazama uumbaji nitakao kutana nao.

Nikakutana na huyo binti, mzuri kawaida, kapendeza zake.
Nikawaza kwanini nisifanyie mazoezi uwezo wangu kutongoza niliofundishwa na Mwalimu wangu, Jacksonian.

Basi nikamsogelea binti wa watu,. Salamu, kisha blaablaa kadhaa (ambazo huwa hatuzikumbuki hata tulisema nini).

Binti alikuwa anaonesha ushirikiano wa kawaida, kama ilivyokawaida yao.

Basi nikaona nisipoteze muda ngoja niamie kwenye kile kipengele muhimu zama hizi( kuomba namba).
Nilivyomuomba tuu namba, binti akafikiria kama dakika 1.
Ile nataka kufungua mdomo ili nikazie zaidi.

Ghafra binti akasimama, kama vile kasahau kitu. Akaniuliza unaitwa nani rafiki, nikamjibu kama vile sikumwambia hapo awali.

Akaanza "MaT2B unatumia pyafum gan?" Nikajifnya kuuliza mbona mimi sijapulizia leo pafyum."
Yeye: Why?
Mimi: Nimetoka kuoga sasa hivi, sijaona haja ya kupulizia.

Yeye: No, no. Tafuta pafyum nzuri, the next day you approach a lady, make sure unanukia harufu nzuri ya pafyum. Itakuongezea point, mvutie mtu kwa harufu yako.
Mimi: ..........

Yeye: and I don't mean unanukia vibaya, no, sijanusa harufu yoyote kutoka kwako.

Mimi: But sio kwamba huwa sijipulizi ila nimependa tuu kuwa out of pafyum leo.

Yeye: ok you gotme, and am sorry, taken already. Do what i told you en you will find a beautiful lady.

Nikawa sina neno, nikamwambia Ok goodnight.

Nikabaki kumuona mtoto mzuri ana ambaa ambaa huyo.

Kwa fedheha niliyopata, nikaamua haraka nimpigie demu angu, Jesca. Hajali haya mambo. Kwanza kale la body spray kangu huwa anang'ang'gana nimnunulie na yeye.

Ila wakuu nipeni jina la pafyum nzuri kwa hela yangu isiyozidi 30K. Sina gari, hata kunukia vizuri nisinukie kweli?
Yaani inakaa mwili unatema harufu balaa! Wewe si mtumiaji wa perfume baba!
 
Kama kweli unafanya mazoezi basi tumia perfumes ndugu acha longolongo. Piga nguo zako za mazoezi chukua perfumes zako mbili piga cocktail ukasemeshe wadada barabarani huko ndio tunafanya wanaume wenzako huku.
 
Karibu Mkuu
Naziuza 25k tu


Dar unaletewa hadi stand ya daladala.
Mkoani natuma

Invicto wengi wanaisifia sana na ni nzuri mno
Aventos ndio hivyohivyo
Suspenso Aisee hiki kitu mimi nimekielewa mno, Mwanaume ananukia vizuri

Mousuf kigunia,perfume ya taifa.

Aventos unanukia kigentleman.

Ramz hii Kuna mtu humu Jana tu ameichukua na ameipenda mno, na inapendwa na wengi.


Ninazo pia za kupima,
16K mils30View attachment 2513646View attachment 2513647View attachment 2513650View attachment 2513652View attachment 2513653
Wewe Saint Anne
Natafuta hiyo Spray ya Aventos.
Huwa inauzwa pamoja na perfume yake ama naweza ipata peke yake.

Duka niliponunua Aventos perfume walisema eti hawana Spray yake.
 
Watu wengi hapa mnatibu effects badala ya cause.

Perfume na hayo ma deodorant haitibu tatizo la kunuka.

Ukiona mwili unatoa harufu ujue shida inaanzia ndani ya mwili. Chakula gani unakula, pombe unazokunywa, unakula matunda?, unavuta sigara? Unakula matunda ya kutosha? Unaoga na sabuni gani - ya acid au alkali?

Angalia hizo mambo hapo juu kabla ya kukimbilia kwenye ma perfume na deodorant.

Mbona kuna wengine tunamiaka zaidi ya 10 hatujajipulizia hayo ma perfume?

Unaweza kukuta mwili wako unatoa sumu halafu unachanganya hilo jasho la sumu linalonuka na ma perfume, si ndo ma kansa yanaanziaga hapo????
 
Watu wengi hapa mnatibu effects badala ya cause.

Perfume na hayo ma deodorant haitibu tatizo la kunuka.

Ukiona mwili unatoa harufu ujue shida inaanzia ndani ya mwili. Chakula gani unakula, pombe unazokunywa, unakula matunda?, unavuta sigara? Unakula matunda ya kutosha? Unaoga na sabuni gani - ya acid au alkali?

Angalia hizo mambo hapo juu kabla ya kukimbilia kwenye ma perfume na deodorant.

Mbona kuna wengine tunamiaka zaidi ya 10 hatujajipulizia hayo ma perfume?

Unaweza kukuta mwili wako unatoa sumu halafu unachanganya hilo jasho la sumu linalonuka na ma perfume, si ndo ma kansa yanaanziaga hapo????
Hili nalo la kuzingatia, pia akiona kwapa linazidi kutema atafute limao/ndimu asugue akate huo ubeberu
 
Back
Top Bottom