Bitoz
JF-Expert Member
- Aug 27, 2015
- 30,822
- 126,643
Umekosea hapo uliposema "vijana wanaojiunga siku hizi" hujatenda haki ........kuna idadi kubwa ya wakongwe ambao ndo vinara wa kutupia makororokoro hapa Jf na hakuna anayewasemaSidhani labda ni mtazamo wangu tu wa kizamani....lakini vijana wanaojiunga JF hivi karibuni wanataka kubadilisha muonekano wa JF...kutoka kuwa Home of great thinker.....mpaka kuwa mtandao unaohamasisha ngono.....,
Kumekuwa na mlipuko mkubwa wa picha zisizo na maadili kwenye mtandao huu.....kana kwamba watu wanaperuzi mitandao ya ngono........
Hii si dalili nzuri kama hili jambo halitakemewa mapema.....inaweza ikafikia kipindi mtu anaweza akajirekodi yeye na mpenzi wake wakifanya ngono na kutupia huku.....
Maadili yanaporomoka kwa kasi sana hapa JF.....na bado mods wamelala usingizi wa pono......sijui kuwa na wao wanafurahi picha hizo au la......
Ombi langu ni kuwa kama mods wameshabadilisha maudhui ya mtandao huu watuambie....ili sisi wengine tujipime kuwa tunastahili kuendelea kuwepo hapa na kuutazama uchafu huu......
Au la basi mods wafanye kazi yao ipasavyo....maana naamini kabisa wanaweza wakalizuia hilo......
Hizi picha ni za kidhalilishaji na kufedhehesha hasa kwa dada zetu...mabinti zetu....na majirani zetu......
Hatua zichukuliwe ipassavyo....
Ungemkosoa tu mleta picha yeye km yeye na siyo kuwasemasema vijana(member wapya/wageni)
Nafikiri nimeeleweka
................................