Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,854
- 10,089
Huyu wakala ni jirani yangu, kila muda ninapotaka kufanya miamala ya kipesa huwa nafanyia kwenye ofisi yake
Huyu binti nadhani hana moyo wa kupenda, na sidhani kama amewahi kumuonesha mtu dalili za kumpenda licha ya uzuri wa sura na rangi aliokuwa nao. Tumempachika jina na kumuita Wakala Eunice kutokana na hali ya kukosa hisia kabisa na wanamme
Jioni ya leo nikaona wacha nijiwekee salio la tigopesa kwenye kilaini changu kipya nilichosajiliwa na mwenyekiti wa mtaa, nikamkabidhi kitita cha 12,000 anidumbukizie kwa laini. Saa ngapi jina lisije Regina Mapyumpyu! Akabaki ameduwaa na kuanza kupatwa na sintofahamu huku wateja wengine wakijaribu kuduwaa
Kwa sisi tuliosomea Cuba tumepata kuelewa kuwa kumbe binti huwa ananipenda, ni vile tu hivi viumbe vimenyimwa uhuru wa kutamka yaliyo moyoni mwao, maake sio kwa mpapatuko ule alionionesha
Mpaka sasa bado nastaajabu mahala pa kuanzia