Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 338
- 891
Nina mwanangu wa kike mwenye umri kama wa miaka 12 hivi. Ana matatizo mawili ambayo nimeshindwa kupata ufumbuzi wake ndio maana nikaamua kuleta huu uzi hapa ili muweze kunishauri.
Tatizo la kwanza ni kwamba binti huyo anakojoa sana kitandani kwa hivi sasa licha ya umri huo alionao. Mwanzoni wakati alipokuwa mdogo hakuwa hivyo ila kadri anavyozidi kukua tatizo linaongezeka. Huu unaweza kuwa ni ugonjwa? Na kama ni ugonjwa tiba yake ni nini?
Tatizo la pili ni kwamba kwa kuwa binti ni kikojozi, basi amekuwa akiamshwa mara kwa mara usiku ili ajisaidie ingawa hiyo haijasaidia. Hata hivyo anapoamshwa, anakuwa kama mtu mlevi au aliyepoteza kumbukumbu.
Anaweza akazunguka nyumba nzima na kufungua milango yote akitafuta choo kilipo. Akishindwa anatoka hadi nje na ikishindikana kabisa atazunguka hadi anajikojolea.
Anakuwa kama yuko ndotoni hivi. Hii pia inaweza kuwa nini? Naombeni msaada wenu.