Nataka kumuoa huyu binti ila tabia zake zinatetemesha sana

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Habari ndugu zangu,

Katika kundi la wanawake zangu kadhaa wa kadha nilionao, nimejikuta nimeangukia kumpenda binti anayetokea na kukulia maeneo ya Mlima Meru huku Arusha ndugu zangu.

Nipo nae kwenye mahusiano ya wastani lakini nimejikuta moyo unanisukuma sana kumuoa ila nikikumbuka mienendo yake na choka kabisa.

Yupo hivi ndugu zangu.

1. Ni binti mwenye umri wa miaka 23-25 na nimlokole haswa ila aliwahi kuwa na mahusiano ya kavunjika anasema mwanaume alimuacha tuu bila yeye kujua sababu ni nini, japo aliingia kwenye mahusiano mengine jamaa wazazi wakazingua na baadae mimi hapa ninae songa naye ndugu zangu.

2. Anapoabudu pana umbali wa si chini ya kilometa kumi kutoka anapoishi , japo huko kuna nyumba za ibada ila ndiyo hivyo.

3. Wazazi wa huyu binti waliwahi kumkataa mwanaume aliyetaka kumuoa huyu binti hapo nyuma kutokana na sababu binafsi za wazazi wake binti.

4. Wakati naanza nae mahusiano alionyesha kutokuniamini na baadae akaamua kukubaliana na mimi nikamuweka rasmi kwenye list yangu.

5. Hanitafuti kabisa mpaka ni mtafute mimi na nikisema nipige kimya tunaweza maliza hata mwezi ndugu zangu, yani ni ukweli usiopingika hanitafuti kabisa labda nianze kumtafuta mimi na siyo vinginevyo.

6. Alishawahi kuniambia mimi ndiye mwenye maamuzi ya kumuoa au kutomuoa maana yeye hajui nawaza nini kichwani mwangu.

7. Alishawahi kunambia ghafla tu hataki tena nyumbani kwao ili aje tuu geto tuanze maisha japo nilimjibu kuwa atulie asiwe na haraka nataka kumuoa hivi karibuni kwa kufata taratibu husika na halali ila baadae aliniambia alikua ananipima tuu.

8. Aliwahi kuniita majina ya mahaba mara moja tuu ila tokea hapo hajawahi niita tena kwa namna yeyote ile. Yani ikitokea tumewasiliana inakua ni kama kusalimiana na mpita njia tuu yani.

9. Hajawahi kuniomba Hela kabisa binti wa watu wala chochote kile huu ni ukweli na waambieni.

10. Yupo tayari kuwa mke wangu ila naona ni mgumu sana asee ikitokea nimesafiri anaweza asinitafute hata mwaka eti, kwajinsi tu alivyo kama mimi sitomtafuta wa kwanza.

11. Yupo tayari kua mama wa watoto wangu.

12. Yupo tayari kuishi maisha yoyote yale kwa mujibu wa maelezo yake na jinsi alivyo alivyo tuu ukimuona.

13. Hawezi kuvaa suruali au nguo yeyote fupi kwake hataki kabisa anapenda kuficha sana mwili wake.

Ndugu zangu nishaurini hapa nioe au niendelee kuongeza namba ya wanawake nilio nao wakuu maana naona kabisa hapa nikioa na ikitokea nimesafiri sijui kama atanitafuta huyu hatakujua huko nilipo naendeleaje kama mimi nisipo mtafuta.

Asanteni wakuu.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Yaani hakutafuti hadi umtafute wewe, hapo tu mimi ningehairisha ndoa.

Mpaka hapo inaonekana bado hamjuaji kwasababu hamwasiliani, ni bora ungekubali kukaq nae walau hata wiki moja ujue alivyo. Huenda yeye ndo tatizo ndio maana anaachwa.

Kwenye sababu za kuachwa hamna mty atasema yeye ndo alikosea, kila mtu anajiwekaga msafi.
 
Back
Top Bottom