....Huyo ni mkeo, sio mtumwa wako...

hapo kwenye bei ina maana hutaki ajue bei ili umchakachue?lol!
there is nothing more romantic like being in the kitchen na mwenzi wako, wakati mwingine mnamalizana huko huko. mengine tutakuambia kwenye kparty,lol
<b>mwanaume kujua fungu la nyanya sokoni ni sh ngapi na vitunguu vya mia ni vingapi ni haki? kila mtu akae kwa heshima zake bwana yaani mume wangu kabisa atwange tangawizi na kukuna nazi sipati photo</b>
<br />
<br />
 
Na ishu ya kuacha matumizi ya nyumbani mbona hujaiongelea??
Kila mtu ana roles zake kwenye familia mkuu!

mbona siku hizi tunasaidiana katika kutoa matumizi, kusomesha watoto, kujenga na mengineyo? Mbona basi tusisaidiane katika majukumu mengine ya nyumbani? Mie naona ni kuendekeza mfumo dume na kutotaka kukubali mabadiliko. Utakuta asubuhi mnadamka nyote kwenda kaznini, lakini mwanaume anataka aandaliwe chai, apigiwe pasi nguo zake awekewe maji ya kuoga, abrushiwe viatu, na briefcase yake aletewe.

Mh....!
 
Mabadiliko yapi unaongelea??

Mbona bailojia hazijabadilika??
 
Salaam wadau,
Nimejaribu kuangalia kwa kina maisha ya ndoa hasa hizi za kiafrika, kipekee za kitanzania na nimegundua kuwa wengi wa wanaume huwafanya wanawake kuwa ni "watumwa" wao.

Yaani wanaume huwatumikisha wake zao kupita kiasi. Kuanzia kufua, kupika, kuosha vyombo na mikazi mingine kibao....bado mume akiwa ameketi atataka apakuliwe chakula, atengewe, hadi mikono eti anawishwe...Hivi ni kweli wewe mwanaume unashindwa hata kupakua chakula kutoka kwenye hotpot hadi upakuliwe..?
Mara atataka anyooshewe nguo, viatu ang'arishiwe....dah too much jamani!

Hivi huyo ni mkeo au mtumishi wako..!?
Modern men need to change bwanaaa!

Swala la wanawake kuwahudumia waume zao lilianzia mbali sana, tangu enzi hizo, kuwa majukumu ya kazi za nyumbani ni za mama na baba kazi yake ilikuwa ni kutafuta mahitaji ya nyumbani na kuitunza familia.... sisi tumezaliwa tumekuta hivyo, sio rahisi leo hii umwambie kijana aliyelelewa na kukuta kwamba kazi zote za nyumbani kwao alikuwa anazifanya mama yake na baba yake alikuwa akishinda kwenye Bao au kwenye baraza la Kahawa leo umwambaie amsaidie mkewe kwa kuwa huo ni mgawanyo wa kazi, atakuona unamtusi.

Mimi binafsi niliwahi kushuhudia kaka akimfokea dada yake kisa eti kamuacha mumewe awapikie, alidai kuwa hayo ni matusi kwao, lakini kumbe mume aliamua kumsaidia mkewe kupika, kwao lilikuwa ni jambo la kawaida lakini kwa kaka mtu ilikuwa ni matusi.

Muingiliano wa tamaduni hasa kutoka Magharibi umeleta mabadiliko makubwa katika baadhi ya ndoa za vijana, wanasaidiana kazi kama ulivyobainisha, lakini hiyo ni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, siku hizi wanandoa wote wanatakiwa kuchangia pato la familia, kwa hiyo wote wanawajibika, lakini kwa kuwa bado baba anaonekana kuwa ni kichwa cha familia, hawezi kushiriki hizo kazi za nyumbani, ndio maana nafasi hiyo ikachukuliwa na mtumishi wa nyumbani tunaita House gir ni kwa nini?

Ni kwa sababu bado kuna wanaume ambao hawako tayari kubadilika kwa sababu jamii imewaambia kuwa hizo ni kazi za wanawake.

Lakini pia kuna malalamiko kuwa wanawake nao, wakisaidiwa, hujisahau na wakati mwingine huwavunjia waume zao heshima, pale ambapo kuna wageni mke anaweza kumuinua mume, tena bila haya na kumwambia 'leo ni zamu yako kupika' kuna wanaume wengine huchuklulia jambo hilo kama kudhalilishwa.....
 
Swala la wanawake kuwahudumia waume zao lilianzia mbali sana, tangu enzi hizo, kuwa majukumu ya kazi za nyumbani ni za mama na baba kazi yake ilikuwa ni kutafuta mahitaji ya nyumbani na kuitunza familia.... sisi tumezaliwa tumekuta hivyo, sio rahisi leo hii umwambie kijana aliyelelewa na kukuta kwamba kazi zote za nyumbani kwao alikuwa anazifanya mama yake na baba yake alikuwa akishinda kwenye Bao au kwenye baraza la Kahawa, leo umwambaie amsaidie mkewe kwa kuwa huo ni mgawanyo wa kazi, atakuona unamtusi. mimi binafsi niliwahi kushuhudia kaka akimfokea dada yake kisa eti kamuacha mumewe awapikie, alidai kuwa hayo ni matusi kwao, lakini kumbe mume aliamua kumsaidia mkewe kupika, kwao lilikuwa ni jambo la kawaida lakini kwa kaka mtu ilikuwa ni matusi.
Muingiliano wa tamaduni hasa kutoka Magharibi umeleta mabadiliko makubwa katika baadhi ya ndoa za vijana, wanasaidiana kazi kama ulivyobainisha, lakini hiyo ni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, siku hizi wanandoa wote wanatakiwa kuchangia pato la familia, kwa hiyo wote wanawajibika, lakini kwa kuwa bado baba anaonekana kuwa ni kichwa cha familia, hawezi kushiriki hizo kazi za nyumbani, ndio maana nafasi hiyo ikachukuliwa na mtumishi wa nyumbani tunaita House girl. ni kwa nini? Ni kwa sababu bado kuna wanaume ambao hawako tayari kubadilika kwa sababu jamii imewaambia kuwa hizo ni kazi za wanawake.

Lakini pia kuna malalamiko kuwa wanawake nao, wakisaidiwa, hujisahau na wakati mwingine huwavunjia waume zao heshima, pale ambapo kuna wageni mke anaweza kumuinua mume, tena bila haya na kumwambia 'leo ni zamu yako kupika' kuna wanaume wengine huchuklulia jambo hilo kama kudhalilishwa.....

Nimekosa font nzuri ya kukuzia hayo maneno ili hata wale wanaotumia miwani wayaone vizuri......

Tatizo kubwa linajikita hapo...Wahanga wa huo uzungu koko tuko wengi!!
 
Mabadiliko yapi unaongelea??

Mbona bailojia hazijabadilika??

Mbona umesoma kama vile una kengeza? Umeona hicho kipande tu, bila kukihusianisha na vipande vingine? Soma post ya mtambuzi hapo chini imenisaidia sana kujibu hoja yako. Asante
 
Kusaidiana kupo lakini sio kanuni,kazi za ndani zote zinamuhusu wife,ikimsaidia mara moja moja poa.Lakini kuto kumsaidia sio tatizo..na mwanamke mwenye kujitambua hilo sio tatizo kwake.We leta uzungu hapo kwako,kama unaosha vyombo kila mara ni majukumu yako tayari,na usipofanya mkeo atakuhoji.Kuwa makini na hilo,huduma hizo ndo zina thamani kubwa kwa mwanamume kufanyiwa na mkewe na zinamfanya mwanamume ampende mkewe zaidi.
 
Haya mambo ya ndoa hayana uniformity kwa sababu yanategemea mambo mengi: mila, dini, kiwango cha elimu, mazingira na mipango/ makubaliano binafsi ya wanandoa. Mtu huwezi kuweka formula au guidelines za kufuata kwa wanandoa wote.

Kitu cha maana ni kuheshimiana na kuthaminiana wanandoa. Kuhusu majukumu ya nyumbani kila mtu ajisikie kufanya hiki au kile bila kupigiana mahesabu. Naamini hakuna mwanaume atakataa kumsaidia mkewe eti kwa sababu tu ni mwanaume. Si kweli. Kuna mazingira mwanaume anaweza hata kufanya kufanya kazi nyingi tu za nyumbani tena bila kuombwa au kusukumwa na yeyote.

Lakini lingine ni kwamba kama kweli tunataka usawa katika ndoa basi tunapaswa kufanyia kazi mambo mengi ya msingi, mf. mambo ya mahari (kwangu ni udhalilishaji wa mwanamke), dhana ya "kuoa" na "kuolewa" , yaan mwanaume ndiye anayeoa na mwanamke ndiye anayeolewa. Dhana hizi ni mbovu kwani zinamwondolea hadhi mwanamke na kuonekana mtumwa wa mwanaume.

Kumbe kufikia heshima na hadhi ya mwanamke katika ndoa nyingi bado ina safari ndefu. mambo mengi lazima yafanyiwe kazi ili hata baadaye wanaume wengi ktk ndoa waweze kutambua umuhimu wa kuchangia shughuli za nyumbani badala ya kumwachia mwanamke peke yake.
 
Mbona umesoma kama vile una kengeza? Umeona hicho kipande tu, bila kukihusianisha na vipande vingine? Soma post ya mtambuzi hapo chini imenisaidia sana kujibu hoja yako. Asante

Ni mwendo wa hoja tu dada na wala siyo vingine....Suala la kusaidiana kazi halikwepeki lakini bado jamii zetu zinatambua majukumu ya kifamilia kuwa katika mgawanyo wa jinsia.....

Ndo maana watu wanajiuliza kwamba..mbona mama yangu na bibi zangu walizifanya hizo kazi vizuri tu na hukukuwa na tatizo?

Na kama ni suala la kufanya kazi....linaeleweka na ndio maana kuna wasaidizi wa kazi za ndani. Naamini hata wewe unajua kuwa siku hizi kazi karibia zote za ndani zinafanywa na wahudumu. Mama naye anakuwa kama msaidizi. Sidhani kama kuna mwanamume atamshinikiza mke wake anayeamka mapema kuwahi kazini amfanyie kila kitu!
 
Swala la wanawake kuwahudumia waume zao lilianzia mbali sana, tangu enzi hizo, kuwa majukumu ya kazi za nyumbani ni za mama na baba kazi yake ilikuwa ni kutafuta mahitaji ya nyumbani na kuitunza familia.... sisi tumezaliwa tumekuta hivyo, sio rahisi leo hii umwambie kijana aliyelelewa na kukuta kwamba kazi zote za nyumbani kwao alikuwa anazifanya mama yake na baba yake alikuwa akishinda kwenye Bao au kwenye baraza la Kahawa.

Leo umwambaie amsaidie mkewe kwa kuwa huo ni mgawanyo wa kazi, atakuona unamtusi. mimi binafsi niliwahi kushuhudia kaka akimfokea dada yake kisa eti kamuacha mumewe awapikie, alidai kuwa hayo ni matusi kwao, lakini kumbe mume aliamua kumsaidia mkewe kupika, kwao lilikuwa ni jambo la kawaida lakini kwa kaka mtu ilikuwa ni matusi.

Muingiliano wa tamaduni hasa kutoka Magharibi umeleta mabadiliko makubwa katika baadhi ya ndoa za vijana, wanasaidiana kazi kama ulivyobainisha, lakini hiyo ni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, siku hizi wanandoa wote wanatakiwa kuchangia pato la familia, kwa hiyo wote wanawajibika, lakini kwa kuwa bado baba anaonekana kuwa ni kichwa cha familia, hawezi kushiriki hizo kazi za nyumbani, ndio maana nafasi hiyo ikachukuliwa na mtumishi wa nyumbani tunaita House girl. ni kwa nini? Ni kwa sababu bado kuna wanaume ambao hawako tayari kubadilika kwa sababu jamii imewaambia kuwa hizo ni kazi za wanawake.

Lakini pia kuna malalamiko kuwa wanawake nao, wakisaidiwa, hujisahau na wakati mwingine huwavunjia waume zao heshima, pale ambapo kuna wageni mke anaweza kumuinua mume, tena bila haya na kumwambia 'leo ni zamu yako kupika' kuna wanaume wengine huchuklulia jambo hilo kama kudhalilishwa.....

Najua kwamba mfumo ndo umetutengeneza hivyo. Sasa kwa kutumia kigezo hicho hicho cha mfumo, ili tusionekane tumebadilika kwa kasi kwani kwa kufanya hivyo inakuwa ngumu kueleweka na jamii; basi si vibaya kufanya baadhi ya kazi hasa zile zinazotuhusu moja kwa moja kama mume, mfano kama nilivyoainisha awali: kunyoosha nguo zako, kung'arisha viatu...n.k

Kwani tukifanya kazi za aina hiyo nini kinaharibika hapo? Au hata wakikukuta watu unafanya kazi kama hizo ni aibu gani utapata hapo...bado sijaona ubaya! Si lazima tupike na kuosha vyombo.
 
Najua kwamba mfumo ndo umetutengeneza hivyo. Sasa kwa kutumia kigezo hicho hicho cha mfumo, ili tusionekane tumebadilika kwa kasi kwani kwa kufanya hivyo inakuwa ngumu kueleweka na jamii; basi si vibaya kufanya baadhi ya kazi hasa zile zinazotuhusu moja kwa moja kama mume, mfano kama nilivyoainisha awali: kunyoosha nguo zako, kung'arisha viatu...n.k. Kwani tukifanya kazi za aina hiyo nini kinaharibika hapo? Au hata wakikukuta watu unafanya kazi kama hizo ni aibu gani utapata hapo...bado sijaona ubaya! Si lazima tupike na kuosha vyombo.

Kwani nyumbani kwako anazifanya nani?

Kwangu zinafanywa na wasichana wa kazi....Kwa hiyo hata hoja ya kumsaidia wife siioni kwani keshasaidiwa long time!!
 
Kusaidiana kupo lakini sio kanuni,kazi za ndani zote zinamuhusu wife,ikimsaidia mara moja moja poa.Lakini kuto kumsaidia sio tatizo..na mwanamke mwenye kujitambua hilo sio tatizo kwake.We leta uzungu hapo kwako,kama unaosha vyombo kila mara ni majukumu yako tayari,na usipofanya mkeo atakuhoji.Kuwa makini na hilo,huduma hizo ndo zina thamani kubwa kwa mwanamume kufanyiwa na mkewe na zinamfanya mwanamume ampende mkewe zaidi.

Watu msipotoshe hoja.
Hivi kazi za nyumbani mmeona ni kupika na kuosha vyombo tu.
Hebu jiulize katika kazi zote anazofanya mwanamke nyumbani, hakuna hata moja ambayo mwanaume anaweza kufanya na kusiwe na madhara yoyote..? Kama umeoa utakuwa unazijua zipo nyingi tu. Kwani ukinyoosha nguo zako unazovaa wewe mwenyewe hata akikukuta rafiki yako wapi aibu hapo? Au ni kasumba?
 
swala ni whom you get married to,olewa na mzungu hizo kazi za nyumbani mtazigawanya 50/50...olewa na mbongo utafua hadi sox zake.....msitutusakame mnapoona tunakimbilia kuolewa na wazungu hata kama ni vibabu......at least hawatakutreat kama mtumwa!..
 
Sidhani na siamini kama kuna mtu anapenda kumtreat mke wake kama mtumwa...Kwanza anachoka sana hadi anashindwa kuandaa futari!!

Hata hivyo katika maisha...mtu hupata shea aliyoiomba na kuikubali (we always get what we asked for or bargained)!!
 
Najua kwamba mfumo ndo umetutengeneza hivyo. Sasa kwa kutumia kigezo hicho hicho cha mfumo, ili tusionekane tumebadilika kwa kasi kwani kwa kufanya hivyo inakuwa ngumu kueleweka na jamii; basi si vibaya kufanya baadhi ya kazi hasa zile zinazotuhusu moja kwa moja kama mume, mfano kama nilivyoainisha awali: kunyoosha nguo zako, kung'arisha viatu...n.k. Kwani tukifanya kazi za aina hiyo nini kinaharibika hapo? Au hata wakikukuta watu unafanya kazi kama hizo ni aibu gani utapata hapo...bado sijaona ubaya! Si lazima tupike na kuosha vyombo.

Uko sahihi, lakini kuna wanawake ambao hawataki waume zao wafanye hizo kazi kwa kuwa malezi yamewafundisha kuwa kazi za nyumbani ni zao....
Hapo napo mume atalaumiwa?
 
Kusaidiana kupo lakini sio kanuni,kazi za ndani zote zinamuhusu wife,ikimsaidia mara moja moja poa.Lakini kuto kumsaidia sio tatizo..na mwanamke mwenye kujitambua hilo sio tatizo kwake.We leta uzungu hapo kwako,kama unaosha vyombo kila mara ni majukumu yako tayari,na usipofanya mkeo atakuhoji.Kuwa makini na hilo,huduma hizo ndo zina thamani kubwa kwa mwanamume kufanyiwa na mkewe na zinamfanya mwanamume ampende mkewe zaidi.

kazi za ndani ni majukumu ya wote,unless mna house girl napo huwezi kumuachia kila kitu,kabla hujaoa wakati unaishi peke yako nani alikuwa anakupikia anakuoshea vyombo kama sio mwenyewe??? leo umeoa unataka umutumikishe mwenzio??eti mume kumpenda zaidi mkewe akifanya kazi za ndani mmnh hii mpya na mke je????au huu upendo unatakiwa uwe wa upande mmoja mume kumpenda mke pekee ndiko kunahitajika na sio wote wawili kupendana??hakuna jambo linalomfanya mke kuona anajaliwa na mumewe ni considerate kama kusaidiwa kazi za ndani na mumewe,kwanza hii inamfanya mke kutochoka sana na kuwa tayari kwa ajili ya tendo la ndoa zile ndoa ambazo mke na mume wanasaidiana kazi za ndani ziko happier kuliko za mmoja kumtumikisha mwengine zaidi....
 
swala ni whom you get married to,olewa na mzungu hizo kazi za nyumbani mtazigawanya 50/50...olewa na mbongo utafua hadi sox zake.....msitutusakame mnapoona tunakimbilia kuolewa na wazungu hata kama ni vibabu......at least hawatakutreat kama mtumwa!..

Aisee!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom