Huwezi Kuua Maiti -Erick Shigongo

Huwezi Kuua Maiti -Erick Shigongo

Shunie mbona hujashusha vitu??? Ponya hii arosto aisee
Shunie baby, hebu shusha nondo usinilazimishe niende msata kilingeni niombe msaada wakukaushe usingizi ili ukeshe unashusha nondo tu [emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
Jaman ndio nimeingia hapa nilikua natafuta hela napambana na vyuma kukaza
 
SEHEMU YA 41...

Ilikuwa ni siku ya nne akiwa amejificha kichakani miguu yake ikiwa imevimba kama matende kwa sababu ya safari, mwili wote ulikuwa umechoka na alikuwa akijaribu kuwaza angefanya nini ili aendelee na safari yake hadi Serengeti ambako alitaka kwenda kuunda jeshi kama alilokuwa nalo Kongo ili kupambana na majeshi ya serikali.

Akiwa katika mawazo hayo ghafla alisikia sauti za watu nyuma ya kichaka alichojificha! Zilikuwa ni sauti za wanaume wakitembea kuelekea eneo alilokuwa, alipenyeza macho yake katika majani ya kichaka na kuangalia nje! Aliliona kundi kubwa la askari waliovaa magwanda ya kijeshi wote walikuwa na bunduki mikononi mwao alitetemeka akijua tayari alishaingia mikononi mwa wabaya wake.

“Na hizi alama za miguu ni za nani?” Aliuliza mmoja wa askari huku akiangalia ardhini.
Swali hilo lilimfanya bibi Nyanjige afe ganzi mwili mzima na kuona mwisho wake ulikuwa umefika, meno yake yaligongana ovyo,alijua ni nyayo zake zilizoongelewa na maaskari walizigundua sababu ya mvua kubwa iliyonyesha siku moja kabla.

“Bwana achana na nyayo za wachungaji wa kimasai tuendelee na msako na siku nitakayomtia mkononi huyo bibi yenu atanikoma sababu kanisumbua sana!” Alisema mmoja wa maaskari hao na kupiga risasi kama tatu hivi hewani ili kuonyesha hasira aliyokuwa nayo dhidi ya bibi Nyanjige.

“Wee acha tu watu tumeacha wake zetu kuja kuhangaika hapa porini na baridi sababu ya kibibi kijingajinga!” Mwingine alidakia
Lilikuwa kundi la maaskari wengi mno na walizidi kupita pembeni ya kichaka taratibu hakuna askari hata mmoja aliyefikiria kuchungulia ndani ya kichaka hicho kuona kilichokuwemo Bibi alizidi kutetemeka kwa hofu.

“Sitakiwi kulaza damu hata kidogo lazima nijiokoe hata nikifa kazi niliyoifanya ni kubwa!” Aliwaza Bibi Nyanjige na sekunde chache baadaye alipata wazo alitaka kuitumia nafasi hiyo ya kupita maaskari kuokoa maisha yake, alitaka kumwiiga Sylivester Stallone Rambo katika sinema zake.
 
SEHEMU YA 42...

“Nafikiri na mimi nikitumia utaalam ule ule nitamnasa mmoja!” Aliwaza bibi Nyanjige na kusimama wima akiupima mwili wake nguvu.
“Niko bombaaa!” Alijitapa na kuamua kujaribu kutumia nafasi hiyo
Aliangaza macho yake pembeni na kuona mzizi mkubwa wa mti ukiwa chini, akajinyoosha na kwa kutumia nguvu nyingi aliukata na kuushika mkononi, ulikuwa mgumu na ulifanana kabisa na kamba.

Alipatwa na ujasiri wa ajabu na kujisogeza hadi pembeni kabisa mwa kichaka alichojificha na kuwashuhudia maaskari wakizidi kupita taratibu bunduki zao zikiwa mkononi, hakuwa na shida nao wote alimtaka mmoja tu! Alitulia akisubiri wa mwisho apite huyo ndiye alikuwa mlengwa.

Wengi walipita akamuona mmoja wao ambaye aliamini alikuwa wa mwisho akija taratibu, yeye alibeba mtambo mkubwa zaidi ya wenzake uliomuelemea kwa uzito! Alitembea peke yake akionekana kuchoka kupita kiasi na alikuwa legelege na mwenye afya mbovu.

“Huyu huyu ananitosha!” Aliwaza bibi Nyanjige huku akiweka mzizi wake vizuri, askari alipofika karibu yake bibi Nyanjige aliruka kwa kasi na kuuzungusha mzizi aliokuwa nao shingoni mwa askari kama ambavyo vibaka hufanya wanapomkaba mtu.

Mwanajeshi hakupiga kelele hata kidogo bali alianguka chini kimyakimya,macho yalimtoka vibaya askari, bibi Nyanjige naye akazidi kubana kwa mzizi kwa dakika kama mbili huku akiwaangalia wanajeshi wenzake waliozidi kutokomea bila kujua yaliyompata mwenzao! Bibi Nyanjige alijipongeza kwa kazi aliyoifanya.

Kwa haraka alimvutia askari huyo na kumwingiza ndani ya kichaka ambako alimbana zaidi na mzizi hadi akafa!
“Sasa mambo yameanza upya!” Alisema bibi huku akimvua askari huyo magwanda yake na kuyavaa mwilini mwake! Ingawa yalimbana sana aliyalazimisha. Kofia ya jeshi aliyovaa askari huyo ilikuwa kubwa kiasi kwamba bibi Nyanjige alipoiweka kichwani ilimfunika uso wake wote, haikuwa rahisi hata kidogo kumtambua.
 
43...

Baada ya kumaliza kuvaa mabuti ya jeshi aliuchukua mtambo aliokuwa nao askari huyo na kuubeba begani mwake, kwa utaalam wa kijeshi aliojifunza akiwa masomoni huko Uingereza ambako ilikuwa lazima kwa wanafunzi wa chuo kikuu kupata mafunzo ya jeshi aligundua mtambo huo ulikuwa ni wakutungulia ndege.

“Sasa watanitambua na nina uhakika kwa nilivyovaa hakuna hata askari mmoja atakayegundua kuwa mimi ndiye bibi Nyanjige wanayehangaika kumsaka! Na kwa kutumia mtambo huu leo hii nafanya kazi ambayo dunia haijawahi kushuhudia!” Aliwaza bibi Nyanjige akiwa amebeba mtambo wake begani!

Ulikuwa mtambo mzito kiasi cha kumyumbisha ukizingatia umri wake kuwa mkubwa, lakini mazoezi ya mwili aliyoyafanya akiwa kijana na aina za vyakula alivyokula vilimfanya awe imara hata kuwa na uwezo wa kubeba mtambo mzito kama ule.

Ghafla alishuhudia helkopta mbili zikija angani nyuma yake badala ya kusikitika kama ilivyokuwa awali alifurahia! Alilala chini na kuuelekeza mtambo angani akiwa ameilenga vilivyo moja ya helkopta bila kusita aliachia kombora moja zito lililokwenda moja kwa moja na kuilipua ndege,bibi Nyanjige alichekelea.
Kabla helkopta ya pili haijafika mbali nayo ilipokea kombora jingine na kuanza kuwaka moto ikielekea ardhini!

“Wamefanya kosa sana kunipa mtambo huu hii ni sawa na kumpa mwehu rungu! Sasa na hakikisha kila ndege inayopita hapa inapokea kipigo na kulipuka leo ni le…….!” Kabla hajamalizia sentensi yake alisikia muungurumo mwingine tena upande wa Mashariki, furaha nyingine tena ilimjaa moyoni na kuunyanyua mtambo wake na kuitungua helkopta hiyo ilidondoka chini mara moja huku ikiwaka moto na alifanya hivyo hivyo kwa ndege ya pili pia!

Matukio hayo yalimshangaza karibu kila mtu aliyekuwepo porini, walishindwa kuelewa ni nani aliyefanya ukatili huo kwani ni ndiyo waliokuwa na mtambo wa kulipulia ndege katika pori hilo jambo lililoonyesha kuwa mtu aliyekuwa akizilipua ndege hizo alikuwa mwanajeshi mwenzao, lakini nani? Hilo ndilo lilibaki swali la kila mmoja wao ikabidi mkuu wa kikosi apige kipenga ili wanajeshi wote wakusanyike kuhesabiwa.
 
SEHEMU YA 44...

Bibi Nyanjige aliposikia mlio wa kipenga ha jeshi alijua mambo yameharibika! Alichukua mtambo wake na kwenda kuuficha porini mahali alipofahamu yeye mwenyewe alirudi haraka na kujichanganya ndani ya kundi la askari mia mbili bila kugundulika! Mpaka wakati huo hapakuwa na askari mmoja wa jeshi la nchi kavu aliyekuwa ameuawa!
“Jamani nani amekabidhiwa mtambo wa kutungulia ndege?”

“Ni afande Laurian!”
“Yupo wapi sasa?”
‘Hatujui afande ila alikuwa anakuja kwa nyuma!”
“Na mtambo wenyewe upo wapi?”
“Alikuwa nao, ila sababu ya uzito wake alitembea taratibu nyuma yetu!”
“Mmekwishajaribu kumtafuta?”
Hakuna mtu aliyejibu swali hilo askari wote walianza kuzungusha macho yao huku na kule wakimwangalia askari huyo bila mafanikio yoyote.

“Haya hesabuni nambaaaa!” Kamanda wa kikosi aliamuru na maaskari wote walianza kuhesabu namba zao taratibu wakianzia na moja hadi kufikia mia mbili! Hesabu ilitimia.
“Jamani mbona hesabu yetu imetimia yupo wapi Laurian?” Aliuliza mkuu wa kikosi na kuamuru askari wahesabu tena namba zao taratibu lakini bado hesabu ilikuja ile ile na kumshangaza Kamanda.

“Laurian! Laurian!” Kamanda aliita lakini bado hakuitikiwa na mtu yeyote, kila askari alishangaa na walishindwa kuelewa kitu gani kilikuwa kimetokea kwani kama askari huyo asingekuwepo ni lazima idadi ya askari ingepungua mtu mmoja.

“Haya wote kaeni katika mstari ili nikague lakini kama nikimpata huyo Laurian adhabu yake itakuwa kifo hawezi kunihangaisha kiasi hiki!” Alisema kamanda na wanajeshi wote walijipanga tena mstari na Kamanda alianza kupita taratibu akiwakagua mmoja baada ya mwingine juu hadi chini kama vile ambayo mwalimu mkuu hufanya shuleni anapokagua usafi!

Bibi Nyanjige alikuwa amesimama katika mstari wa nyuma akitetemeka kwa hofu, alijua tayari alishaingia matatizoni alikuwa na uhakika wa kugundulika kwa sababu angejulikana ni mwanamke na kugundulika kwake kungemaanisha ni yeye aliyekuwa akizilipua helkopta.
 
SEHEMU YA 45...

“Afande simama wima mbona umejikunja hapa mgongoni? Na huo mguu sawa ulioweka si wenyewe panga vizuri miguu yako hunioni mimi? Huyu kamanda anaweza kukuletea matatizo makubwa sana sababu amekasirika!”
Askari mmoja aliyekuwa jirani alimwambia bibi Nyanjige lakini alipojaribu kujinyoosha mgongo ilishindikana kwa sababu mgongo wake ulipindwa na uzee!

“Nyooooka kidogo afande huu mgongo utakuletea matatizo!” Alisema tena askari huyo lakini Bibi Nyanjige hakujibu kitu alijua kufanya hivyo kungefanya agundulike na kuhatarisha maisha yake alizidi kuinamisha kichwa chake chini.
“Hebu toeni kofia zenu kichwani upesi ili niwaone vizuri!”Kamanda aliamuru na kwa sababu ilikuwa ni amri hapakuwa na njia yoyote ile ya kubisha, askari wote walianza kutoa kofia zao vichwani na mkuu wa kikosi alipita kwa askari mmoja baada ya mwingine.

Macho ya askari aliyesimama jirani na bibi Nyanjige yalimfuata kamanda kila alikopita akikagua na kumsahau kabisa bibi Nyanjige, alipogeuza kichwa chake dakika chache baadaye alishangaa kukuta askari mwenzake hayupo! Hakutaka kuuliza sababu Kamanda alikuwa amekaribia sana eneo hilo, alizidi kukauka ili kuonyesha heshima ya jeshi.

“Mbona idadi imebaki ileile 199! Kuna askari amepotea na huyo ndiye anatungua ndege zetu wenyewe, sijui anatumiwa? Ni lazima asakwe” Alisema kamanda. ************
Bibi Nyanjige alikuwa katikati ya vichaka akitembea kuelekea mahali alipouacha mtambo wake wa kulipulia ndege alipokuta bado upo alifurahi kupita kiasi na nusu saa baadaye akiwa bado katikati ya nyasi alianza kuona maaskari wakipita kuelekea mahali walikotokea.

Aliiona hiyo kama bahati nyingine kubwa zaidi alinyata taratibu na kujichanganya katikati maaskari bila kugundulika na kuanza kutembea pamoja nao, hakuna aliyeligundua jambo hilo! Umbali wa kilometa kama kumi na tano katikati ya pori walifika kambini na wanajeshi walijipumisha ndani ya mahema waliyojenga.
 
Back
Top Bottom