Huwezi Kuua Maiti -Erick Shigongo

Huwezi Kuua Maiti -Erick Shigongo

SEHEMU YA 03...

Ilikuwa si rahisi kumwona bibi Nyanjige kwa ulinzi mkali uliokuwepo nyumbani kwake porini, nyumba yake ilizungukwa na Tembo wasiopungua kumi, waliomlinda usiku na mchana! Wazungu wengi waliojaribu kumfikia ili kupata picha yake waliuawa kwa kunyangwa na Tembo!

Mzungu mmoja aliyekwenda porini kwa helkopta alifanikiwa kuipata picha ya bibi Nyanjige akiwa katikati ya tembo!
Ni picha hiyo iliyoleta matatizo kwani ilipochapishwa katika magazeti na majarida mbalimbali nchini Uingereza na Marekani serikali ya Tanzania ilishtuka na kuamini kuwa mtu aliyekuwa akitafutwa alikuwa porini nchini Kongo.

Bila kuchelewa ilituma wanajeshi wapatao ishirini waliopewa msaada na askari wengine kumi wa Kongo! Walifika hadi msituni lakini hawakufanikiwa kumkamata bibi Nyanjige na pia hawakufanikiwa kurudi salama nyumbani! Wote walikufa kifo hichohicho cha kukanyagwa na Tembo!

Mpaka mwezi moja baada ya askari hao kuondoka hapakuwa na mawasiliano yoyote kutoka msituni, simu zao za upepo ziliendelea kuita bila majibu! Hilo lilionyesha wazi watu hao hawakuwa hai!

Ilibidi serikali za Tanzania na Kongo kwa kushirikiana ziandae jeshi kubwa lenye askari wasiopungua elfu tano waondoke kwenda msituni kumsaka bibi Nyanjige!
Maaskari wote 5000 walilizunguka pori wakiwa na silaha kali mikononi mwao na ndege za kivita zilipita angani!

Askari ndani ya ndege hizo walipoangalia chini ka kutumia viona mbali waliziona maiti za askari wenzao zikiwa ardhini na tembo wengi wakiwa wamezunguka kibanda kidogo kilichoonekana kuwa kama nyumba.

Ghafla mamia kwa maelfu ya ndege walionekana angani, hawakujulikana walikotokea! Wengi walitua kwenye vioo vya mbele vya ndege hizo na kuwafanya marubani washindwe kuendesha ndege zao vizuri kwa sababu hawakuona mbele.
“Tufanya nini sasa?”

“Turudi tukatue kwanza, vinginevyo hawa ndege watasababisha tuangushe ndege ni wengi mno na sielewi wametoka wapi!”
“Sawa geuza basi!”

Wakati wanageuza ndege nyingine ilishafika karibu yao ikipita katikati ya makundi ya ndege, zote mbili ziligongana na kuwaka moto zikiwa angani! Askari waliokuwa wakitembea kwa miguu walishangaa kuona ndege zikigongana.

Inaendelea.
Nzuri
 
SEHEMU YA 36...

Bibi Nyanjige alisogea hadi eneo walipoangukia na kugundua wote walikuwa wamekufa! Alitembea kwenda mbele na kuchungulia ndani ya basi lililobondeka aliona watu wengi wakiwa wamelala ndani ya basi damu nyingi zikiwatoka, maiti nyingi hazikuwa na viungo muhimu kama vichwa, mikono na hata miguu!

Jeneza lililobebea maiti wakiondoka Dar es Salaam lilikuwa wazi na maiti haikuwa ndani yake! Ilikuwa ni ajali mbaya kuliko ajali zote ambazo bibi Nyanjige aliwahi kushuhudia maishani mwake!
Ghafla wazo lilimwijia kichwani mwake lilikuwa wazo la kujiokoa lilikuwa wazo zuri kuliko mawazo yote aliyowahi kuyawaza!

Alijua ni lazima ingegundulika alisafiri na basi lililosafirisha maiti, hivyo ili kupoteza kabisa habari zake aliamua kuufanya ulimwengu wote uamini kuwa naye alikufa katika ajali hiyo.
“Hakuna mtu atakayeamini nimeokoka katika ajali hii hivyo ni lazima niyafanye mawazo yao yawe kweli!” Aliwaza bibi Nyanjige.

Alipita katika dirisha lililovunjika na kuingia ndani ya basi lililobondeka na kuivuta moja ya maiti iliyoharibika vibaya haikuwa na kichwa kabisa, alikiona kichwa cha maiti hiyo pembeni lakini hakukijali, aliubeba mwili na kutoka nao hadi nje kupitia dirishani, alikuwa bibi kizee lakini mwenye nguvu za ajabu.

Alipoifikisha maiti hiyo nje aliilaza chini na kuruka tena hadi ndani ya basi ambako alikichukua kichwa na kutoka nacho hadi nje! Ilikuwa ni kazi ya kutisha lakini aliifanya bila hofu, mikono yake yote ilitapakaa damu kutoka shingoni mwa kichwa alichokibeba na damu hiyo ilipenya katika vipele alivyokuwa navyo mikononi mwake lakini hakujali.

Alikiweka kichwa hicho pembeni na bila kuchelewa aliamua kutekeleza mpango aliokuwa nao, aliivua maiti hiyo nguo ilizovaa na kuzitupa pembeni kisha akavua gauni lake na kubaki kama alivyozaliwa, kwa haraka aliivalisha maiti hiyo gauni lake na pia mkufu wake wa shaba ulioandikwa jina lake! Alitaka kuidanganya dunia kuwa hata yeye alikufa katika ajali hiyo ili aweze kuandaa jeshi zuri zaidi porini.
 
SEHEMU YA 37...

Alipomaliza tu kazi ya kuivalisha maiti gauni lake alisikia muungurumo wa gari nyuma na alipogeuza macho yake kuangalia barabarani aliliona gari la polisi na maaskari wapatao watatu waliteremka ndani ya gari hilo huku bunduki zikiwa mikononi mwao.

Alijua wazi watu hao walikuwa wakimtafuta yeye hakuna kilichokuwa mbele yake zaidi ya kujiokoa tena, ili kutimia lengo lake alikichukua kichwa cha marehemu na kuanza kukimbia nacho mbio kuelekea vichakani.
“Jamani yule anayekimbia ni mtu au nyani?”

“Mtu yule!”
“Hapana labda ni nyani sidhani kama kuna binadamu mweusi kiasi kile hapa duniani!” Alijibu mmoja wa maaskari.
Kabla hata hawajalifikia basi walikutana na maiti moja na mmoja wao maaskari alibaki akiimulika maiti hiyo na tochi, wenzake walinyoosha moja kwa moja hadi mahali lilipokuwa basi hilo, walipomulika ndani walishuhudia maiti nyingi zikiwa zimelaliana, hapakuwa na mtu aliyeonekana kuwa hai, maiti nyingi zilikuwa zimekatikatika vibaya!

“Masikini hii ina maana hata bibi Nyanjige atakuwa amekufa au?”
“Ni lazima itakuwa hivyo!” Maaskari waliokuwa wakilikagua gari waliongea na ghafla walisikia mwenzao akipiga kelele.
“Huyu hapa?”
“Nani?”
“Bibi Nyanjige!”

Waliokuwa ndani ya basi walitoka ndani ya basi mbio na kurudi hadi mahali mwenzao alipokuwa akipiga kelele, hawakuamini macho yao kuukuta mwili uliovaa gauni la bibi Nyanjige ukiwa hauna kichwa!
“Kichwa chake kiko wapi? Ni lazima tuupeleke pamoja na kichwa vinginevyo hakuna mtu atakayeamini kuwa huyu ni bibi Nyanjige!”

“Lakini ni afadhali amekufa ametuhangaisha sana!”
“Huyu bibi alikuwa hatari mno!”
Walijaribu kukitafuta kichwa cha marehemu bila mafanikio mwisho wakaamua kupiga simu ya upepo Chalinze kuomba msaada na dakika kama ishirini baadaye gari kubwa la polisi liliwasili na kupakia maiti zote zilizokuwa ndani ya basi hilo na kuondoka nazo.
“Na hiyo?” Aliuliza mmoja wa askari waliokuwa wakipakia maiti.
 
SEHEMU YA 38...

“Hii hapana! Tunakwenda nayo Dar es Salaam makao makuu ni lazima tuipelekea hospitali kuu ya Jeshi ili wakubwa waione tena usiku wa leo hii hii! Maana huyu bibi aliisumbua sana dunia!”
“Sasa wataamimi vipi bila kichwa?”

“Alama zote zipo, hii cheni yake imeandikwa jina lake si unaona!” Alisema askari mmoja na akamwonyesha askari mkufu ulioandikwa neno Nyanjige walioukuta shingoni mwa maiti!
“Na hata hizi nguo alizovaa ndio zake kabisa!” Alisema askari huyo.

Magari yote yaliondoka moja likiwa kimbeba maiti zote kuelekea hospitali ya Tumbi na gari jingine la polisi likiwa limebeba maiti moja lilielekea Dar es Salaam! Gari hilo la polisi halikusimama Chalinze lilinyoosha moja kwa moja kuelekea jijini Dar es Salaam ambako lilifika baada ya kama dakika arobaini na tano!

Maiti ilipelekwa moja kwa moja hadi chumba cha maiti cha hospitali ya jeshi ambako usiku huohuo wakuu wa jeshi walifika na kuanza kuikagua maiti hiyo.
“Jamani mna uhakika huyu mliyemleta ni bibi Nyanjige kweli?”

“Ni yeye afande si mnaona hata huu mkufu wake afande!!”
“Hebu niuone!” Afande Mwita Mitiro aliuomba mkufu huo, alipokabidhiwa alianza kuukagua, alipoliona jina la Nyanjige kwenye mkufu huo hata yeye aliamini ulikuwa ni mwili wa bibi Nyanjige.
 
SEHEMU YA 39...

“Kweli bwana si unaona hata gauni ndilo lilelile lililopo katika hii picha!” Alisema mkuu huyo huku akiimulika picha aliyoshika mkononi mwake kwa tochi.
“Hebu ivueni hiyo maiti hizo nguo ili tuikague zaidi!”

Bila kuchelewa vijana waliikamata maiti hiyo na kuivua nguo zote ilizovaa hakuna aliyekuwa tayari kuamini macho yake walipokuta mwili maiti hiyo una sehemu nyeti za kiume! Waligundua bibi Nyanjige aliwachezea tena mchezo.
“Ni akina nani walioileta maiti hii?”
“Ni sisi afande!”

“Yaani mmetuletea maiti ya mwanaume?” Aliuliza afande kwa ukali.
“Hatukujua afande!”
“Hebu wawekeni mahabusu hawa haraka na msako ni lazima uendelee!

Bibi Nyanjige atakuwa hai amefanya tena ujanja wake wa kuvalisha nguo maiti, nataka akamatwe mara moja na kuletwa hapa!” Askari mia mbili waondoke kwa magari na helkopta tano zifuate usiku huu huu kwenda kuuzunguka msitu wote ulio jirani na mahali ajali ilipotokea nina uhakika atakuwa maeneo hayo hayo!

Mpaka kesho saa sita kamili namtaka awe hapa akiwa hai mmesikia?” Aliuliza mkuu wa majeshi hasira zikiwa zimempanda.
“Ndiyo afande!”
Kipenga kilipulizwa wanajeshi wote wakakusanyika na dakika kama ishirini baadaye mkuu wa majeshi alishuhudia helkopta na magari yakiondoka kwa kasi, kila askari alikuwa na bunduki yake mkononi!

Hofu kubwa ya wanajeshi ilikuwa ni wadudu na nzige ambao bibi Nyanjige aliwatumia, ingawa alikuwa nchini Tanzania ambako hapakuwa na nzige wala mbung’o bado wanajeshi waliogopa vita vya wadudu!

Itaendelea
 
Back
Top Bottom