Huwezi Kuua Maiti -Erick Shigongo

Huwezi Kuua Maiti -Erick Shigongo

SEHEMU YA 65

Alikumbuka kwamba ni kweli walitakiwa kumfikisha mtu yule mbele ya Wakuu wa Majeshi akiwa hai na sio vinginevyo. Japokuwa bibi yule anatisha kutokana na historia za mauaji makubwa na mazito ambayo ameyafanya, lakini kumfikisha kwa wakuu akiwa amekufa, ni matusi kwa mwanajeshi mwenye cheo kama yeye. Kumpeleka mtuhumiwa tena mwanamke kizee akiwa amekufa mbele ya wakuu? Atajielezaje? Kwamba ametusumbua sana? Msumbufu mwenyewe mwanamke!!? Tena kizee? Haikumuingia akilini.

Mwili wa bibi Nyanjige ulikuwa kama umekufa ganzi. Maumivu yalikuwa makubwa na akajikuta akianza kukata tamaa kutoka mikononi mwa watu wale. Hakujua wakati kama ule anahitaji kutumia mbinu ya namna gani kumuokoa. Suala la kufa, halikuwa na mjadala, alitambua kwamba ni lazima ndani ya siku chache zijazo atakuwa amekufa, lakini mateso atakayoyapata yatakuwa mabaya zaidi ya kifo!

Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akarudi kutoka nyuma ya gari alikokuwa ameegemea akiwa tayari na suluhisho. “Hebu muingize kwenye gari”. Dereva akamtazama katika hali ya kutoelewa, lakini Mkuu alishaingia kwenye gari na kufunga mlango wake. Dereva akatekeleza hilo, alimbeba na kumwingiza kwenye kiti cha nyuma, akazunguka na kuingia kwenye kiti cha mbele, akawasha gari.

“Wapi Mkuu?”
“Twende Hospitali.”
* * * * * * *
Umati wa watu ulikuwa umejazana nje ya Hospitali ya mkoa kutaka kumwona Bibi Nyanjige, mwanamke aliyevuma nchi nzima kutokana na vitendo vya mauaji ya kushangaza. Watu walitaka kuhakikisha kwamba ni kweli mwanamke anayelisumbua jeshi la nchi ni mtu mzima kwa kiasi kinachozungumzwa?

Wengi walihisi kwamba huenda mwanamke huyo akawa ni mtu wa makamo au kijana na sio mtu mzima sana kama inavyotangazwa kwa sababu kutokana na kiwango cha matatizo anayoyasababisha, inakuwa vigumu kuamini kwamba kikongwe kama hicho kinaweza kufanya yote hayo.

Polisi walikuwa na kazi ya ziada kujaribu kusuma sukuma wananchi waliokuwa wakilisogelea lango la hospitali ambako Bibi Nyanjige alikuwa ameingizwa.
 
SEHEMU YA 66

Baada ya kufanikiwa kumfikisha hospitali, Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi alijihisi kupumzika. Aliacha wamuingize kwenye chumba ambacho yeye hakufahamu ni cha nini, kisha akamgeukia daktari wa zamu.
“Ameshazinduka?”
“Hapana, inaelekea amepata kipigo kikubwa sana na itamchukua muda kuzinduka na.....”

“Hebu nambie, muda gani unafikiri atakuwa ameshazinduka?”
“Sina hakika Mheshimiwa, lakini nitajitahidi iwe haraka kama mnavyohitaji”
Msaidizi wa Mkuu wa Majeshi akavuta pumzi za matumaini, kisha akamgeukia tena. “Nambie, atapona huyu?”
“Siwezi kusema mapema hivyo, lakini sijaona kama ana majeraha makubwa sana, labda iwe ni ya ndani kwa ndani, hata hivyo tutafanya uchunguzi”.

“Sikiliza, mimi nataka apone,” baada ya maagizo hayo, mkuu aligeuka akatoka nje ya jengo. Wapiga picha za magazeti na televisheni pamoja na waandishi wa habari wakamfuata kwa kasi kutaka kumhoji, lakini hakuwa tayari kuongea kwa muda ule. Akapiga simu ya upepo ofisini kuwafahamisha mambo yalivyo. Muda mfupi baadaye, kundi la wanajeshi lilifika hospitalini kuweka ulinzi mkali ili bibi Nyanjige asitoroke.
* * * * * * * *

Bibi Nyanjige hakuwa amezimia kweli kama ilivyoeleweka. Alikuwa na fahamu zake kamili, lakini alifanya hivyo akiamini kwamba mbinu hiyo itamsaidia katika kumfanya apate mapumziko wakati akitafakari la kufanya.
Ukweli aliuona ni kwamba uhai wake uko hatarini kufuatia kuwekewa ulinzi mkali na wanajeshi. Aliwahi kufikiria kujiokoa kwa kuita wanyama waje pale pale hospitali na kusambaratisha madaktari na wanajeshi na yeye akapata nafasi ya kutoroka, lakini ilikuwa vigumu kwa vile kinywa chake kilitawaliwa na maumivu makubwa kufuatia buti alilopigwa na yule msaidizi wa Mkuu wa Majeshi.

Kufikishwa mbele ya Wakuu wa Majeshi kama alivyosikia wale wanajeshi wawili wakizungumza ni kitu kilichomuumiza kichwa sana. Juu ya kukata tamaa, lakini bado alijipa moyo kwamba atapata jibu la tatizo lake kadiri maumivu yatakavyopungua.
* * * * * * * * *
 
Maiti maanake tayari kufa. Sasa unauaje maiti? Labda ingekuwa kufufua.
 
SEHEMU YA 67

Siku tano baadaye.
Ukumbi wa mikutano wa Mkuu wa Majenzi ya Ulinzi ulikuwa kimya kana kwamba hakukuwa na watu. Soli za viatu vya Mkuu wa Majeshi pekee ndizo zilizosikika zikigongagonga sakafu, akiizunguka meza ile kubwa ya duara katika hali ya kuonyesha kuchanganyikiwa.

Ni kikao ambacho kilianza muda mrefu uliopita, wastani wa saa nzima, huku Mkuu wa Majeshi akifoka ukumbi mzima kutokana na operesheni ya kumshughulikia Bibi Nyanjige ilivyokwenda kizembe mpaka kumkamata tena kwa taabu kubwa.
Ni katika kikao hicho ambapo Makamanda wote waliokuwa wakishughulikia suala la bibi Nyanjige mpaka kufikia kuuawa kwa wapiganaji walifukuzwa katika jeshi na pia kutakiwa kuchukuliwa hatua maalum za kijeshi ili iwe funzo kwa wakuu wengine ambao ni wazembe kama hao.

Kwa muda wa dakika kumi zilizopita, Mkuu wa Majeshi alikuwa akizungumza kwa hasira mbele ya makamanda wake kutokana na uzembe uliokuwa umefanyika hata kumfanya Bibi Nyanjige kulinyanyasa jeshi na kuua wanajeshi pamoja na kufanya mambo mengine ya kishenzi huku jeshi likionekana dhahiri kushindwa kumkamata.

“Hamko ‘serious!’ Inakuaje jeshi zima linyanyaswe na mwanamke kikongwe? Ni ujinga gani unafanyika hapa. Tumetuma wanajeshi sitini na magari kwenda Kiambali kufuatilia taarifa za kuonekana kwa bibi huyu, wanarudi watu wawili! wengine wote wameuawa na ng’ombe?

Aibu gani hii? Ng’ombe wanafanya wapiganaji washindwe kufanya kazi yao? Ng’ombe?” Alipomaliza maneno hayo, akarudi kuketi. Kiha akaendelea kusema, “Ok, sasa tumeshamkamata Bibi Nyanjige na tunatakiwa kumuadhibu kwa adhabu ambayo itakuwa ni halali yake kwa jinsi alivyotusumbua kwa kipindi chote hiki na kutufedhehesha.” Alisema Mkuu wa Majeshi

“Hata hivyo, kwa kuwa hali yake inaridhisha, nataka aletwe hapa sasa hivi ili tuamue la kufanya mbele yake na utekelezaji ufanyike dakika hiyo hiyo ya makubaliano”.
Hakukuwa na wa kubisha wala kujadili chochote. Wanajeshi kadhaa waliitwa, wakapewa maagizo hayo kwamba wayatekeleze kwa muda mfupi ujao.

Kama umeme, wanajeshi wale walivaa bunduki zao, wakachukua gari na kwenda hospitali ya mkoa kumchukua bibi Nyanjige.
 
SEHEMU YA 68

Bibi Nyanjige aliletwa pale haraka kama ilivyotakiwa. Safari hii hakuwa uchi kama alivyokutwa wakati anakamatwa. Alikuwa amevaa gauni lililoraruka-raruka ambalo alipewa bila kujua lilikotoka.
Mkuu wa majeshi akaendelea na mazungumzo ambayo alikuwa akiyaongea kabla bibi Nyanjige hajafika pale. “Kwa hiyo kumchoma katika tanuru siamini kama kutatusaidia sisi na vizazi vyetu. Ni kweli ametuudhi zaidi, lakini tuangalieni adhabu nyingine ambazo tumezijadili hapa wakati huyu bibi hajafika.

“ Au kumkatakata na kumwagia acid kwenye sehemu za majeraha na mateso mengine makali tuliyokuwa tumeyajadili, pia sijaafiki kwamba ni adhabu anayostahili.”
Kutokea hapo, zilijadiliwa adhabu nyingine mbaya na za kutisha zaidi, lakini jibu halikupatikana mpaka ilipotangazwa adhabu ya kumkausha na kumweka katika jumba la makumbusho.

“Adhabu hii ninakubaliana nayo na anastahili kabisa.” Mkuu wa Majeshi alizungumza akitabasamu baada ya kazi nzito ya kutafuta jawabu linalostahili.
Bibi Nyanjige alishtuka! Hiyo ilikuwa ni adhabu kubwa na mbaya zaidi kutekelezwa kwake. Ingawa alijua kwamba wanajeshi wana tabia ya ukatili, lakini hakudhani kwamba adhabu ya kifo kwa kukaushwa ingepitishwa kwake.

Alijikuta akitetemeka kwa hofu, hasa baada ya kugundua kwamba kwa mazingira yaliyomzunguka, kujiokoa kilikuwa ni kitu kisichowezekana kabisa.
Eneo lote lilikuwa limezungukwa na wanajeshi wenye silaha nzito nzito.

Wakati akifikiria hivyo, alishtukia ameshikwa mikono na kuvutwa kinyumenyume mpaka kwenye chumba kipana ambacho hakikuwa na dirisha zaidi ya hewa ya mtambo wa kiyoyozi.
Moyo ulimdunda bibi Nyanjige. Alifahamu kwamba mbele ya wanajeshi, mwisho wa maisha yake umefika.

Alifikiri kuita wanyama waje kumsaidia, lakini kutokana na ukali wa silaha zilizoko pale jeshini, alihisi kwamba hilo halitawezekana, na zaidi kuingia ndani ya chumba alichowekwa, itakuwa vigumu kwa mnyama yeyote kuingia.

Alifungwa kitaalamu kwenye kiti maalum cha umeme ambacho kwa jinsi kilivyo madhubuti, hakuweza hata kujitikisa.Donge la hasira lilimkaba kooni.
 
SEHEMU YA 69

Chumba alichokuwamo kilifungwa na akabaki peke yake ndani. Baada ya dakika chache, wanajeshi zaidi ya 20 na wakuu wao wawili waliingia ndani ya chumba hicho, na kubamiza mlango kwa nyuma. Mlango huo ulikuwa na tundu ndogo kwa juu yenye nyavu zilizochakaa, tundu ambalo lingemwezesha mtuhumiwa anayewekwa mahabusu ndani ya chumba hiki, kuwasiliana na mlinzi yeyote endapo anapata tatizo.

Mwanajeshi mmoja alikuwa amekamata sindano na boksi lenye chupa yenye sumu. Akaelekea upande mmoja na kuminya sindano akivuta sumu ijae ndani yake.
Baada ya kumaliza kufanya hivyo, akamrudia bibi Nyanjige na kuinama mbele yake huku akitabasamu kuonyesha kwamba mwisho wake umefika. Akamshika mkono na kusogeza ncha ya sindano.

Bibi Nyanjige alipagawa, ghafla akapiga mluzi mkali sana katika namna ya ufundi iliyowashtua hata wale wanajeshi. Yule aliyeshika sindano alisita. Wale wengine wakatazamana kuonyesha kutoelewa kinachoendelea. Kusita huko kulimpa mwanya bibi Nyangije kuendelea kupiga uruzi wake wa ajabu.

Ghafla, kundi la kutisha la nyuki lilipenya kwenye kidirisha kidogo cha mlangoni, likaingia ndani ya chumba na kuwavamia wale wanajeshi. Bibi Nyanjige aliendelea kupiga uruzi na wale nyuki hawakumgusa. Wanajeshi walijaribu kufungua mlango na kukimbia nje, ikashindikana kwani nyuki walitawala chumba kizima. Pamoja na ujasiri wa kijeshi, lakini walijikuta wakilia na kupiga mayowe. Haikusaidia, nyuki walizidi kujaa ndani na kuwashambulia. Vishindo vya kuwakwepa nyuki na kuchanganyikiwa, vilikuwa vikubwa kupita kiasi.

Dakika tano baadaye, wanajeshi wote 20 walikuwa wameshakufa.
 
SEHEMU YA 70

Baada ya lile kundi la nyuki kutoka humo chumbani, ndipo Bibi Nyanjige alipogundua kwamba nyuma ya kiti alichofungwa, kuna swichi ya kuwasha au kuzima kiti kile. Kwa kutumia mguu wake mmoja, aliigusa swichi ile, na hapo, kamba maalum zilizofungwa sambamba na kiti cha umeme zikaachia.

Hakuchelewa, akajitoa kwenye kamba na kumvua nguo mmoja wa wale wakuu wawili waliokuwa wameingia mle ndani, akavaa yeye pamoja na miwani! Akaufungua mlango kisha akatoka nje.

Wanajeshi wote walipomwona wakampigia saluti. Akaenda mpaka yalipoegeshwa magari, akachagua mojawapo, akachomeka funguo na kuliwasha. Akaliondoa taratibu huku wanajeshi wakiendelea kumpigia saluti kwenye kila kizuizi alikopita!!

Bibi Nyanjige akarudi kuelekea Morogoro. Akapita Chalinze na masaa kadhaa baadaye, akawa ameshaingia kwenye mbuga za wanyama za Mikumi.
Hapo akaliacha gari na kuingia kwenye msitu mzito.

Ni huko alikoamua kuwa ndiko kutakuwa kambi yake wakati akiunda jeshi la aina yake litakaloshirikisha wanyama wote kwa mpango kwamba baada ya miaka mitano arejee kufanya shambulio zito la kuivamia nchi.
 
SEHEMU YA 71

NI kama machale yalimcheza bibi Nyanjige kwani wakati bomu likilipuka hakuwa eneo hilo wanyama wake wawili walikuwa wakichimba chini kwa kasi kuelekea upande wa pili moshi wa bomu ulimfikia hadi mahali alipokuwa lakini alizidi kutambaa akiwafuata chimbachimba wake kwa nyuma , kasi yao ya kuchimba ardhini hata yeye mwenyewe ilimshangaza .

Walipokuwa wamekwenda kama umbali wa mita ishirini chimbachimba walianza kuchimba kuelekea juu kwa amri ya bibi Nyanjige , udongo ukawa ukiporomoka kumfunika lakini bado alipenyenya katikati ya udongo huo na kulipanda … taratibu kuelekea juu ya ardhi.

Alikuwa amechoka taabani na hakujua nini cha kufanya ghafla alishtukia minong’ono ya watu ikija nyuma yake ! Alipogeuza kichwa kuangalia nyuma aliwaona maaskari wasiopungua ishirini wakiwa na bunduki aina ya SMG mikononi mwao na wote walipiga kelele wakimuamuru atulie vinginevyo wangemuua kwa risasi .

Tulia hapo hapo ulipo vinginevyo tutakumaliza umetusumbua kwa muda mrefu sana leo mwisho wako umefika !’’
Hilo hata mimi nalifahamu na ninaomba mniue haraka iwezekanavyo nimechoka kukimbia , lakini hata hivyo niliyowafanyia yanatosha kuwa kisasi kwa waliomuua mama yangu !’’

Wanajeshi wote walibaki … kwa mshangao kusikia baba Nyangije aliua watu wengi kiasi hicho kwa kisasi cha mtu mmoja ilikuwa siyo rahisi kwao kuamini kuwa hatimaye bibi Nyanjige walikuwa wamemtia mikononi mwao .
Leo hakuna ujanja ni lazima ufe tu!’’ Hilo ninalolitaka mimi !’

Hebu lifanyeni haraka basi!” Hasira ilizidi kuwapanda wanajeshi na wote kwa walijikuta wakiziandaa bunduki zao tayari kwa mashambulizi , hawakutaka kupoteza muda zaidi walichotaka ni kung’oa roho ya bibi Nyanjige mtu aliyewahangaisha kwa muda mrefu .
Jamani hebu sikilizeni !”

mmoja wa wanajeshi alisema Tusikilize nini ?” wote waligeuka na kumuuliza
Ni vema tukafuata maagizo ya mkuu majeshi kuwa tukimkamata hai tumpeleke kwake akiwa hai “
Haiwezekani kwani huko nyuma tulikwishafanya hivyo akatoroka ! Leo kosa hilo halifanyiki ni lazima tuulie mbali”
 
SEHEMU YA 72

Yalitokea mabishano kidogo baadhi ya wanajeshi wakisema haikuwa sahihi kumuua bibi Nyanjige , wengi walikubali kumbeba na kumpeleka moja kwa moja hadi makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam ambako mkuu wa majeshi angeamua kitu cha kumfanyia bibi huyo hatari na machachari aliyetingisha jeshi .

Kwa kauli moja wanajeshi wote walikubaliana juu ya kumsafirisha bibi Nyanjige akafungwa kwa kamba mikono na miguu yake pamoja , kipande cha mti kilipitishwa katikati ya mikono na miguu yake na wanajeshi walimbeba kwa kutumia mti huo kama mzega wa maji au mnyamapori na kutembea naye moja kwa moja hadi barabarani walikoacha magari yao.

“ Jamani hivi kweli mmeshindwa kuniua mpaka mnipeleke kwa huyo mkuu wenu ?” “ Wee kitimoto kaa kimya na ufunge kabisa hilo domo lako !” “Yaani unaniita mimi kitimoto ? Kijana umechoka kuishi siyo ? Nguruwe mkubwa wee! Bibi Nyanjige alifoka aliwatukana sana wanajeshi lengo lake likiwa ni kuwatia hasira ili wamshambulie kwa risasi afe kifo cha mara moja ! Alijua wazi mateso yaliyokuwa mbele yake talikuwa makubwa na hakutaka kukutana nayo .

Wewe hata utukane matusi gani Dar es salaam lazima ufike tu na kwa taarifa yako unakwenda kukaushwa na kutunzwa katika makumbusho ya taifa ili hata wajukuu zetu waje kuelewa ulikuwa mtu hatari kiasi gani !”
Aisee kwa hiyo nitakuwa mtu maarufu kama V.L Lenin au Mao siyo ? Hicho ndito nilichotaka , siku zote niliota kuwa maarufu na kweli nimekuwa Hureeeeeeee!”

Bibi Nyanjige alicheka na kushangilia kw dharau .
Aliyoyafanya yote yalizidi kuwachefua wanajeshi lakini kwa sababu walishagundua nia yake walizidi kumvumilia na kumpakia ndani ya gari , mawasiliano kati ya vikosi vyote yalifanyika magari yalikusanywa na msafara wa kurudi Dar es salaam ulianza mara moja . Ilikuwa furaha kubwa mno kwa wanajeshi kumpata mtu aliyehangaisha nchi
 
SEHEMU YA 72

Yalitokea mabishano kidogo baadhi ya wanajeshi wakisema haikuwa sahihi kumuua bibi Nyanjige , wengi walikubali kumbeba na kumpeleka moja kwa moja hadi makao makuu ya jeshi jijini Dar es salaam ambako mkuu wa majeshi angeamua kitu cha kumfanyia bibi huyo hatari na machachari aliyetingisha jeshi .

Kwa kauli moja wanajeshi wote walikubaliana juu ya kumsafirisha bibi Nyanjige akafungwa kwa kamba mikono na miguu yake pamoja , kipande cha mti kilipitishwa katikati ya mikono na miguu yake na wanajeshi walimbeba kwa kutumia mti huo kama mzega wa maji au mnyamapori na kutembea naye moja kwa moja hadi barabarani walikoacha magari yao.

“ Jamani hivi kweli mmeshindwa kuniua mpaka mnipeleke kwa huyo mkuu wenu ?” “ Wee kitimoto kaa kimya na ufunge kabisa hilo domo lako !” “Yaani unaniita mimi kitimoto ? Kijana umechoka kuishi siyo ? Nguruwe mkubwa wee! Bibi Nyanjige alifoka aliwatukana sana wanajeshi lengo lake likiwa ni kuwatia hasira ili wamshambulie kwa risasi afe kifo cha mara moja ! Alijua wazi mateso yaliyokuwa mbele yake talikuwa makubwa na hakutaka kukutana nayo .

Wewe hata utukane matusi gani Dar es salaam lazima ufike tu na kwa taarifa yako unakwenda kukaushwa na kutunzwa katika makumbusho ya taifa ili hata wajukuu zetu waje kuelewa ulikuwa mtu hatari kiasi gani !”
Aisee kwa hiyo nitakuwa mtu maarufu kama V.L Lenin au Mao siyo ? Hicho ndito nilichotaka , siku zote niliota kuwa maarufu na kweli nimekuwa Hureeeeeeee!” Bibi Nyanjige alicheka na kushangilia kw dharau .

Aliyoyafanya yote yalizidi kuwachefua wanajeshi lakini kwa sababu walishagundua nia yake walizidi kumvumilia na kumpakia ndani ya gari , mawasiliano kati ya vikosi vyote yalifanyika magari yalikusanywa na msafara wa kurudi Dar es salaam ulianza mara moja . Ilikuwa furaha kubwa mno kwa wanajeshi kumpata mtu aliyehangaisha nchi
 
Back
Top Bottom