Huwezi badili tabia ya mwanamke hata ufanye nini

paruta

Member
Mar 22, 2017
7
28
Salute wakuu!

Mimi ni kijana wa miaka 27,kipindi na soma chuo niliwahi kutongonzwa na binti ambaye alikuwa tayari ana mtoto sikuona kuwa ni shida maana kila nlipo kuwa na hamu nae alinipa bila usumbufu wowote.

Kwa mwanzo nlikuwa sijajua maisha yake taratibu nikaanza kumjua, kumbe ni binti ambaye alikuwa hana kazi Maalumu alikuwa anawapenzi wengi ambao ndio walikuwa wakimuweka mjini ubaya nlikuwa tayari nimesha mpenda.

Kwa kupungukiwa akili nikasema wacha nimbadilishe nilijua shida yake inayo msumbua ni pesa nikawa na muhudimia japo sikuweza kutimiza mahitaji yake yote,kwahyo tabia ya kuruka na wanaume ikaendelea japo kwa uchache.

Kabla sijamaliza chuo alinetegeshea mimba nyumbani wakajua ila wakanishauri nisitishe mawasiliano na huyo binti Mpaka ntakapo maliza chuo, ila tutaendelea kumuhudumia huyo binti na ikawa hvyo.
Baada ya yeye kujifungua akapata Mpenzi alikuwa kinyozi wa saloon, meanwhile huduma zote mimi ndio nlikuwa natoa pale anapoishi,sikuona kama ni shida yeye kuwa na mahusiano mengine.

Siku zikapita nikamaliza chuo nikawa nikienda kumona mtoto na kurudi kwangu, siku moja tukakaa tukayaongea, penzi likarudi na akaahidi ya kuwa ataachana na huyo kijana. Kidume nikatulia nikahisi nimekuwa mkubwa nahitaji kuoa huyu mwanamke, tukaweka mipango ya kutambulishana Kwa wazazi liwe jambo official.

Kabla ya hayo kutimia kumbe mwenzangu bado hajatulia kila kukicha magomvi akawa halali nyumbani siku nyingine anaenda kulala kwa wanaume wake,Kuna siku nimekuta SMS za huyo kijana wa saloon Wakiitana mume na mke na siku chache nyuma aliniambia kuwa ana mimba. Ile mimba ikazua mzozo akaitoa mwenyewe.

Tumeendelea kuishi majuzi nikakuta video wamejirecord wakiwa kitandani na huyo Kijana wa saloon. Nilimpiga na simu yake kichwani.
Yeye na mama yake wakanifungulia shitaka la shambulio, na bila kuwa na uoga akaniambia hanitaki ana mpenda yule kijana wa saloon. Kihistoria mama yake ana watoto saba kila mmoja na baba yake.

Tumeshaachana week tatu sasa ila changamoto ipo kwenye malezi ya mtoto.

Nawasilisha.
 
1. Ulikuwa unamhudumia ila hukuweza kutimiza mahitaji yake.......

2. Kijana wa saluni.....

Kaka unamlaumu bure huyo binti.... kosa lako, umejiwekeza sehemu kuna red flags kibao!!!
 
1. Kipindi nikiwa chuo nlikuwa nikitimiza mahitaji yake kwa uchache maana nlitegemea pesa ya wazazi na boom la chuo.
2. Baada ya kumaliza chuo nakupata kibarua nikaweza kumtimizia mahitaji yake yote ya msingi bado hakuweza kutulia.

Kama ulivyosema ni kweli mimi ndio mkosaji,hata kwenye mada nieleza kuwa nilipungukiwa na akili nilitaka kubadili tabia ya mwanamke kumbe ni jambo ambalo haliwezekani😅😅.
 
Salute wakuu!

Mimi ni kijana wa miaka 27,kipindi na soma chuo niliwahi kutongonzwa na binti ambaye alikuwa tayari ana mtoto sikuona kuwa ni shida maana kila nlipo kuwa na hamu nae alinipa bila usumbufu wowote.

Kwa mwanzo nlikuwa sijajua maisha yake taratibu nikaanza kumjua, kumbe ni binti ambaye alikuwa hana kazi Maalumu alikuwa anawapenzi wengi ambao ndio walikuwa wakimuweka mjini ubaya nlikuwa tayari nimesha mpenda.

Kwa kupungukiwa akili nikasema wacha nimbadilishe nilijua shida yake inayo msumbua ni pesa nikawa na muhudimia japo sikuweza kutimiza mahitaji yake yote,kwahyo tabia ya kuruka na wanaume ikaendelea japo kwa uchache.

Kabla sijamaliza chuo alinetegeshea mimba nyumbani wakajua ila wakanishauri nisitishe mawasiliano na huyo binti Mpaka ntakapo maliza chuo, ila tutaendelea kumuhudumia huyo binti na ikawa hvyo.
Baada ya yeye kujifungua akapata Mpenzi alikuwa kinyozi wa saloon, meanwhile huduma zote mimi ndio nlikuwa natoa pale anapoishi,sikuona kama ni shida yeye kuwa na mahusiano mengine.

Siku zikapita nikamaliza chuo nikawa nikienda kumona mtoto na kurudi kwangu, siku moja tukakaa tukayaongea penzi likarudi na akaahidi ya kuwa ataachana na huyo kijana. Kidume nikatulia nikahisi nimekuwa mkubwa nahitaji kuoa huyu mwanamke, tukawepaka mipango ya kutambulishana Kwa wazazi liwe jambo official.

Kabla ya hayo kutimia kumbe mwenzangu bado hajatulia kila kukicha magomvi akawa halali nyumbani siku nyingine anaenda kulala kwa wanaume wake,Kuna siku nimekuta SMS za huyo kijana wa saloon Wakiitana mume na mke na siku chache nyuma aliniambia kuwa ana mimba. Ile mimba ikazua mzozo akaitoa mwenyewe.

Tumeendelea kuishi majuzi nikakuta video wamejirecord wakiwa na huyo Kijana wa saloon. Nilimpiga na simu yake kichwani.
Yeye na mama yake wakanifungulia shitaka la shambulio, na bila kuwa na uoga akaniambia hanitaki ana mpenda yule kijana wa saloon.

Tumeshaachana week tatu sasa ila changamoto ipo kwenye malezi ya mtoto.

Nawasilisha.
Wewe falaaa nini....nani anaoa single maza? Hao ni wakugegeda tuu.
 
Ha haaa...
Mambo yao (Kinyozi na Binti) waachie wenyewe..

Sema nini mkuu huyo binti atarudi kwako tena and guess what mtaendelea na penzi
Kurudi kwangu ni jambo ambalo halitowezekana kamwe. Maana nimeshajua ni kiumbe wa aina gani.
 
Kuzaa namtu sio dhambi ,maranyingi snaa tumezaa nawatu tusiowajua Sana kiundani mtoto akishazaliwa inabaki Kua baraka kwenu,inshu IPO ktk kuhimili mikiki yamalezi namtu ambae ushajua fika Kua hamuwezi kupikika chungu kimoja tena,nikipengele!
 
Kwa maana nyengine awe gaidi si ndivyo..?
Akiwa hivyo stori Kama hizi tutatolea wapi. Bando zetu tutazitumiaje sasa..?

Mkuu acha apende tena huko atuletee mrejesho..
wenzako wamekua wengi siku hizi humu ndani lol. Hebu mpe uzoefu huyu mtu. Hahahah
 
Kijana wa chuo una haha na mapenzi tena Yale ya dhati kabisaa, hivi huo muda mnapata wapi kwani? poleeeeeh sana lol
 
1. Kipindi nikiwa chuo nlikuwa nikitimiza mahitaji yake kwa uchache maana nlitegemea pesa ya wazazi na boom la chuo.
2. Baada ya kumaliza chuo nakupata kibarua nikaweza kumtimizia mahitaji yake yote ya msingi bado hakuweza kutulia.

Kama ulivyosema ni kweli mimi ndio mkosaji,hata kwenye mada nieleza kuwa nilipungukiwa na akili nilitaka kubadili tabia ya mwanamke kumbe ni jambo ambalo haliwezekani😅😅.
Kunguru hafugiki
 
Back
Top Bottom