Huwezi amini lakini ukweli bila NATO, Marekani anaiogopa Sana Urusi

Unaichuliaje Russia mkuu?
Tambua kwamba ni Russia pekee anayeweza kushambulia target iliyopo popote duniani kwa kutumia Intercontinental Ballistic Missiles ( ICBMs).

Ana nuclear power kuliko taifa lolote duniani ana vifaru imara na vingi kuliko taifa lolote.
Nuclear inatumika moja tu ndani miezi 12 dunia nzima tutakua tushakiona cha moto... usidanganywe na nchi kumiliki 1000000000 Nuclear bombs haisaidiii labda lolote

Mfano hata wasipo pigana ikatokea Mr kiduku akatuma kitukizito Antarctica tumeisha

Dunia inahatari hiii
 
Kipindi LITHUANIA na ESTONIA wanajiunga na NATO mwaka 2004 URUS sio tu alitishia Bali alipeleka Makombora ya ISKANDER Beralus na Karzakhstan. Alitia Pessure kubwa Sana eti zisijuinge na NATO kwasababu ziko Mpakani na URUS lakini yako wapi mpaka Leo?

This time URUS hatavamia Ukraine direct,atatumia mbinu nyingine. Consequences ya Urusi Kuvamia ni kubwa sana. Ujeruman ilikataa kusitisha NORD STRING 2 Lakini imeapa kusitisha Ujenzi wa Bomba Hilo endapo Urus itaivamia Ukraine.
Ukraine hali ni tofauti sana. Hiyo nchi inachukuliwa too serious tofauti na hizo ulizotaja na ndio maana tumeshuhudia umegwaji wa eneo la Crimea toka Ukraine.
 
Tatizo watu wa JF mnasikiliza Sana vyombo vya habari vya kimagharibi ......huwa havitoi Sana uwezo mkubwa wa kijeshi wa RUSSIA

ila Russia ni nchi inayomiliki silaha Kali zaidi kuliko nchi yoyote duniani that's y NATO wanajitahidi kukaa pamoja kumdhibiti coz Russia anamiliki hadi Robot za kivita ......ukiachana na ICBM ambazo zinaweza kukufikia popote pale duniani

Kama unabisha kuhusu USA kumuogopa RUSSIA rejea CUBAN NUCLEAR MISSILES. ......coz pale USA ilikaa na rais JF Kennedy wa USA aliomba yaishe wakae chin kusuruhisha hii Mambo

Na Russia kuzuia Ukraine kujiunga na NATO yuko sahihi coz ....baada ya kukaa chin walifanya agreement ya majeshi ya hiz nchi yasije kukaribiana .....kamwe ....

So USA kujiingiza Ukraine anataka kumu overtake mrussia
 
Alafu na ile ishu ya Nord String 2 ya Germany. Kuna watu mna madini umu hatari sana
Mradi una manufaa pande zote mbili. Ulaya wanautaka sana uwe active haraka iwezekanavyo sema ndio hivyo kuna figisu za Mmarekani ndio zinakwamisha huo mradi.

But at the end of the day Europe ndio inaumia kwa kupanda bei ya gas inayopitishwa Ukraine.
 
Ila dunia inaenda kasi sana ...Sio dunia ya miaka 90 na mwanzoni mwa miaka 2000...
Tunakoelekea inaonyesha ni ngumu sana kudhibiti ( Monopoly) technology kama zamani....Ona uwezo wa silaha wa Nchi zinazonyanyuka kama KOREA KZ,. IRAN, TURKEY, India nk....
Itafika mahali kumiliki silaha fulani haitoshi wewe kuweza kuishambulia tu nchi bila ya wewe kupata madhara..
Hata Russia anawaza mara 2 kuushambulia UKRAINE...
Issue sio tu kushinda bali damages baada ya vita....Hilo ndio maana US anahangaika na ': Nuclear deal"' na IRAN
Ndo maana Israel anaumiza kichwa kwa IRAN, vivyo hivyo IRAN kwa ISRAEL..
Korea kz ana test silaha kila siku watu wanaangalia tu.
Zile zama za WEST na US kutamba pekee zinayoyoma...Silaha pekee wanayotegemea ni UCHUMI,. kitu ambacho Mchina anakuja ku- ibalance dunia Ktk kutegemea West na US...
Nawaza miaka 30 ijayo Geo politic itakavyokuwa . Je US ataendelea kumudu kuilinda Taiwan, UKRAINE , Israel nk...au zitasimama zenyewe?...Je kwa utawandawazi ulivyo na usiri wa technology nchi ngapi zitainuka Ktk ujuzi wa vitu mbalimbali ikiwemo silaha..?
Jambo la kusikitisha , katika maelezo yako, haujataja nchi hata moja ya Afrika. Tafsiri yake ni kwamba waafrika wamebaki kama mashabiki na watazamaji tu wa mambo yanayofanyika kwenye mabara ya watu wenye akili timamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
S.A kwenye hayo mambo ni sawa na Simba wa maonesho, hana impact yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aliachana na hayo mambo kitambo baada ya mkataba wa kuacha kutengeneza silaha za nyuklia aliteketeza silaha zake. Ilikuwa bado serikali ya weupe.
Angekaza naye angekuwa anasumbua kama Pakstan wameweza kumiliki nukes naye angeweza tu.
 
Unasema kwamba, Marekani haiwezi kuikabili Urusi bila NATO, hapohapo unasema inaweza kuikabili Urusi kwa vikwazo! Sijakuelewa!
Ok namaanisha Kijeshi Marekani anaiogopa Urusi,ndio maana Kila akitaka kuinya Urusi Kijeshi huanza kuwaambia NATO wawe wamoja dhidi ya hujuma zozote za Urusi za Kijeshi.
Marekani hawezi kuinya Urusi kuwa ataikabili peke yake,Bali lazima atake kuihusisha NATO yote.
Lakini kitu pekee ambacho Marekani anaweza kumshugulikia Urusi ni kumwekea vikwazo tu.
Nadhani nimeeleweka Mkuu wangu Franc the Great.
 
Wewe sasa ndo zuzu kabisa, kuwa wa kwanza kuunda vitu haimanishi huwezi kupitwa, china ashaanza unda ndege za abiria ila mpaka upewe kibali cha kuanza kuziuza kwa ajili ya usafirishaji kuna mchakato unapita, na unachukua miaka.
Ndehe za kivita ndo sasa katoa generation ya ndege zake ambazo wanasema ni superior kuliko hata ndege za kirusi.
China ndiyo nchi pekee duniani inayomiliki space station.
Ukitoa Marekani, na Urusi, China ndiyo one man show aliyeshusha vifaa mars. Hizo nchi za ulaya wana agency ya anga moja wanashirikiana.
Space station nyingine wanashirikiana russia, US, na nchi za ulaya.
Kwa roho mbaya ya marekani akataka wasimpe ruhusa china kuitumia hiyo space station, mchina akaona isiwe tabu ngoja nitengeneze yangu, na anayo na anazidi kuitanua iwe the biggest station huko angani.
Steve jobs aliwahi kuulizwa kwanini wanapenda kufanyia production china, jibu lake lilikuwa china ndo nchi ambayo ukitaka skilled labor ya watu wanaojua kitu flani, watajaa stadium, wakati US hawajai hata meza.
Speed ya China ya mabadiliko katika muda mfupi inatisha ni mabadiliko ya muda mfupi sana.
China ndiye mwenye train zenye speed kuliko train ya nchi yoyote, nadhan unajua kuhusu maglev technology, train inayoelea kwenye reli na kukimbia speed ya bullet.
US sasa anaigopa china ndo maana anahangaika na vikwazo kuipunguza speed navyo vina matokeo ya muda mfupi.
Huawei baada ya kuwekewa vikwazo, soon wanataka kuanza kuzalisha vifaa wenyewe kwa ajili ya electronics.
Kuna kampuni inadeal na mambo ya quantum computing mwaka jana imepata breakthrough, US kwa uoga kuwa ikifanikiwa inaweza hack na kubreak security zake kaipga vikwazo wakati ana makampuni kibao yanafanya research ya quantum computing.
Bado silaha, kala mfuatiliaji mwishoni mwa mwaka jana katest kifaa kikaenda into space kikarudi kwa speed kali sana lakini bado kikawa maneuvered kutua. Wataalam wa US wakashangaa maana hawana kifaa kama hicho, kifaa chochote kikiwa kwenye high speed from space kwenye reentry huwezi kukimaneuver kwa technology walionayo, iliwashangaza mchina kufanya hivyo. Na walikuwa hawajui ni kifaa cha kubeba wanaanga au silaha.
Baadae wanakuja kugundua ni kwa ajili ya vyote, inaweza tumika kubeba silaha au ikatumika kama rocket ya kupeleka vtu space.
Mchina anatengeneza drones, tena advanced drones za ulinzi.
It is a matter of time wale jamaa ni unstoppable.
Nawaogopa sana maana wakishakaa pale top kabisa wakatulia hii dunia itapata shida sana maana ni wanyonyaji haswa.
Lazima utakuwa muislamu wewe, huwa mnafundishwa kuichukia marekani na europe na kuishabikia china..,
 
Lazima utakuwa muislamu wewe, huwa mnafundishwa kuichukia marekani na europe na kuishabikia china..,
🤣🤣🤣🤣 Mimi siyo Mwislamu ni Mkatoliki ambaye kasahau mlango wa kanisa ulipo. Mimi arguement zangu uwa haziko based kwa misingi ya dini, bali ninasema kile ninachoona kama kilivyo.
Sina kumbukumbu kwenye ukoo wetu hata kama tuna Mwislamu.
Siichukii Europe lakini ndiyo ukweli China anakuja kwa kasi, hata ukifumba macho ukapingana ma hilo hakutabadili ukweli. 🤣🤣
Labda uniambie uliponiquote kuna uongo wowote nilioandika.
 
Sijui nikuite Punguani au Layman?

Bila NATO Urusi ataifanya Nini Marekani?

NATO ina jumla ya Wanajeshi 450,000. Kati ya hao Wanajeshi wa Marekani ni 370,000. Nchi 29 zilizobaki Zina Wanajeshi 80,000 ndani ya NATO.

NATO ina Aircraft Carrier 27. Kati ya Hizo 22 ni za Marekani. Nchi 29 zilizobaki Zina Aircraft Carrier 7 tu.

NATO ina Combat Tanks 27,000. Kati ya Hizo, 19,000 ni za Marekani. Nchi 29 zilizobaki kwa pamoja Zina Combat Tanks 8,000.

Bajeti ya NATO kwa mwaka ni $ 1,019,000,000,000.($ 1.019T). Kati ya Hizo, $ 760,000,000,000 ni za kutoka Marekani. Nchi 29 zilizobaki zinachangia Nusu ya Marekani kwa pamoja $ 300,000,000,000.

NATO ina Jumla ya Nuclear Waepons 7,200. Kati ya hizo, 6,500 ni kutoka Marekani. Nchi zingine 29 kwa pamoja Zina Nuclear Waepons 700 tu.

NATO ina Jumla ya Fighter jets 3,500. Kati ya Hizo, 2,700 ni Kutoka Marekani. Nchi zingine 29 zinachangia Jumla ya Jets 800 tu.

Huwa mnaposema sijui eti Marekani bila NATO hawezi kupigana wakati mnajua kabisa Marekani ndio NATO kwenye Kila Kitu,bila Marekani hakuna NATO.

Lengo la Marekani kwenye NATO sio kutafuta Support ya nchi za Ulaya Kijeshi bali ni Hofu ya Marekani kwamba Urus atazimeza nchi za Ulaya Mashariki tangu USSR kusambaratika. Ndio maana kwenye huu mgogoro wa URUS na UKRAINE,Mataifa madogo ya Ulaya Mashariki Kama LATVIA,LITHUANIA,ROMANIA na ESTONIA ambao ni wanachama wa NATO wameiomba Marekani iongeze Wanajeshi wake kwenye Mataifa hayo na Siraha nzito ili kuyalinda dhidi ya Urusi.

Ndio Maana Marekani imeahidi kwamba endapo Urus itaivamia Ukraine kijeshi basi Marekani haitatuma Wanajeshi wake kwasababu Ukraine sio Memba wa NATO. Lakini ikaahidi Urus itajutia kitendo chake make Marekani itaongeza idadi ya vikosi vyake na Siraha nzito kwenye Mataifa ya Ulaya Mashariki ili kuyalinda dhidi ya uvamizi wa URUS. Ndio Maana mpaka Sasa Putin kagoma Kuvamia Ukraine.
Umechangia vizuri na huu ni mjadala was kawaida tu.
Sasa kulikua na haja gani kuniita punguani.
Mimi nimetoa maoni yangu,nawe umetoa yako Tena vizuri tu.ulichoharibu ni kuniita punguani.asante kwa hilo pia Asante kwa maoni yako mazuri yenye data.
 
Wadau kumbuka unapomsema USA ni kusema Israeli ,urusi alishaambiwa akijaribu kuivamia ukraine atapata madhara makubwa sana na kujutia, kashaambiwa diplomasia itumike kumaliza mgogoro huo ,yaani Israeli+uingereza+german+ufaransa+US A kiukweli amesisitiziwa ajaribu aone na wao wametega kujiona wapole ila wadau USA na washirika wake wameshajiandaa anasubiri tyu avamie,MUNGU mwenyewe hawezi ruhusu hii sayari ije kuongozwa na madikteta china na urusi,kushindwa kwa marekani na israeli niifanya dunia iongozwe na madikteta urusi na china ,pata picha hii sayari ya dunia itakuaje,dunia lazima iongozwe kwa njia ya kidemokrasia sio kidikteta ili kila mtu afanye anachotaka pasipo kuingilia uhuru wa mtu.
Kwa komenti hi ndio umeniunga mkono kabisaaaa kwamba Israel,USA,Ukraine,German na France wanamsubiri Urusi ajaribu kuivamia Ukraine.aisee kumbe Urusi ni jeshi la nchi moja dhidi ya mataifa tajiri zaidi duniani.
 
Aliachana na hayo mambo kitambo baada ya mkataba wa kuacha kutengeneza silaha za nyuklia aliteketeza silaha zake. Ilikuwa bado serikali ya weupe.
Angekaza naye angekuwa anasumbua kama Pakstan wameweza kumiliki nukes naye angeweza tu.
Nataka tujiulize, kwanini hakuna nchi hata moja ya Afrika Mashariki yenye ujuzi wa mambo hayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom