Huwa siwaelewi kabisa wazee wa michepuko

raia_mwema

JF-Expert Member
Oct 10, 2012
481
250
Heshima zenu wakuu!!!

Jamani kama kuna watu ambao siwaelewi ni hawa wanaoendekeza michepuko.

Utakuta mwanaume ana ndoa halali lakini huwachukua binti aliyeko single na kumpangishia kisha kumhudumia. Mzee mtu mzima ana kabinti ka 20's amekapangishia na anakahudumia, mwishowe wanazaa mtoto, hapa utamkuta binti anajidanganya eti wazee hawawapi presha bila kujua kuwa kuna mke halali wa ndoa ambaye anapata presha huko alipo.

Jaribu pia kufikiria future ya huyo mtoto pia, atapataje elimu na huduma nyinginezo za kijamii? Watoto wanaishia kunyanyasika na kuishi maisha ya shida, jiulize utakuwa mchepuko hadi lini? wenzako wanafamilia wewe mchepuko, halafu huku wazee hawanipi presha kwa hiyo siwataki vijana. una tofauti gani na kahaba anayejiuza? Maana na wewe pia unajiuza.

Mwishowe unajikuta ndio single mother unalalamika umetelekezwa. Hautaweza kutambulishwa popote wala hakuna yeyote atakayetambua mahusiano hayo ya nyumba ndogo.

Wewe unayeendekeza kuchepuka labda nikwambie tu mtu mwenye malengo na mipangilio mizuri ya kimaisha haendekezi kuchepuka wala haendeshwi na tamaa za ngono, Tambua kuwa maisha ni zaidi ya ngono. Binti kama unajitambua, unajiheshimu na kujithamini hautayumbishwa na vitamaa vya mali wala kukubali kuwekwa kinyumba na kutumika kingono.

Wanaume wenzangu tupunguze kuendeshwa na tamaa za kimwili. Hautakaa utunukiwe cheti cha kufuzu katika ubingwa wa kuchepuka au ngono. Tufikirie maisha na zaidi kuwa na upendo na wake zetu na watoto zetu zaidi. Chukua muda kujenga upendo na ukaribu na familia kuliko kukimbilia kwa michepuko.

Tusiendekeze zinaaa jamani wakuu

Ni hayo tu naomba kuwasilisha
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,741
2,000
Rais ameshauriwa na Mwinyi aongeze mke ili asizeeke. Maana yake nini....?? Jiulize.
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,169

Umemaliza?
 
logolie

Member
Oct 2, 2016
96
125
Mchepuko kawaida na ili mwanandoa wakike ajitume lazima aone vi SMS za mademu wengine kwenye simu ili kumhamasishe asizubae. Wanawake wetu akijua ndio yeye pekee nyodo zinakuwa nyingi hajali tena kivile..ila kukiwa na more than one ukorofi unapungua..anakuwa na adabu sana. Hongera mchepuko.
 
Ncherry1

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
1,973
2,000
Hahahah... I never thought kila anaechepuka n muhun bt cyo wote coz i hav experienced that issue and i hv come to realiz its nt bad at all acha wachepuke tu afu nkwambie kitu ukiwa hujawai fanya unaona wenzio wana dhamb cku ukifanya unatuliaa tuli wala umsem mtu... Cyo mbaya kuchepuka na mtu ambae ana heahim familia yako na anajali future yako and cyo kila mtu anatakiwa aolewe wanaume hawatosh and mwngne ameolewa n mateso tu bora upate zako mbaba anakuhandle naanakushaur to be somebody... I rather date a married man than mkaka ambae anntumia for sex nikimwambia twende kwetu hatak nkimnyima mgegedo ugomv sasa vya nn kujipa karaha akat hata mia mbovu ukipata shda akusaidii..... Life is full of mysterious things! I just said ts nt me!
 
msmimi30

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
913
1,000
mi kutambulishwa sijui kufahamika inanisaidia nini muhimu huduma nnazo hitaji napata na mwanangu namsetia maisha yake mapemaa siwezi kubweteka kusubiri kugombea urithi na kweli wazee hawana presha maisha ya michepuko inaendelea wakati nyie wa ndoani mnakufa na presha kuwaza michepuko ya waume zenu. kingine wanaume ni wachache na katika uchache wao kuna wasoweza kazi na kina james lazima kugawana aisee
 
Jephta2003

JF-Expert Member
Feb 27, 2008
5,311
2,000
Heshima zenu wakuu!!!

Jamani kama kuna watu ambao siwaelewi ni hawa wanaoendekeza michepuko.

Utakuta mwanaume ana ndoa halali lakini huwachukua binti aliyeko single na kumpangishia kisha kumhudumia. Mzee mtu mzima ana kabinti ka 20's amekapangishia na anakahudumia, mwishowe wanazaa mtoto, hapa utamkuta binti anajidanganya eti wazee hawawapi presha bila kujua kuwa kuna mke halali wa ndoa ambaye anapata presha huko alipo.

Jaribu pia kufikiria future ya huyo mtoto pia, atapataje elimu na huduma nyinginezo za kijamii? Watoto wanaishia kunyanyasika na kuishi maisha ya shida, jiulize utakuwa mchepuko hadi lini? wenzako wanafamilia wewe mchepuko, halafu huku wazee hawanipi presha kwa hiyo siwataki vijana. una tofauti gani na kahaba anayejiuza? Maana na wewe pia unajiuza.

Mwishowe unajikuta ndio single mother unalalamika umetelekezwa. Hautaweza kutambulishwa popote wala hakuna yeyote atakayetambua mahusiano hayo ya nyumba ndogo.

Wewe unayeendekeza kuchepuka labda nikwambie tu mtu mwenye malengo na mipangilio mizuri ya kimaisha haendekezi kuchepuka wala haendeshwi na tamaa za ngono, Tambua kuwa maisha ni zaidi ya ngono. Binti kama unajitambua, unajiheshimu na kujithamini hautayumbishwa na vitamaa vya mali wala kukubali kuwekwa kinyumba na kutumika kingono.

Wanaume wenzangu tupunguze kuendeshwa na tamaa za kimwili. Hautakaa utunukiwe cheti cha kufuzu katika ubingwa wa kuchepuka au ngono. Tufikirie maisha na zaidi kuwa na upendo na wake zetu na watoto zetu zaidi. Chukua muda kujenga upendo na ukaribu na familia kuliko kukimbilia kwa michepuko.

Ni hayo tu naomba kuwasilisha
Wewe uliyeta hii mada ukikua umri wa kuitwa mzee ndio utajua utamu wa wasichana wadogo,mke wangu mtu mzima,halafu nichepuke kwa mtu mzima mwenzangu?,nyumbani nimekimbia nini na huku nje nafuata nini?,halafu aliyekuambia watoto wa nyumba ndogo hawasomeshwi ni nani?,wanapata huduma zote stahiki kama wa nyumbani,mimi babu yangu alikua na wake wanne,mimi nina mke mmoja na mchepuko mmoja,sijamfikia marehemu babu yangu,tuendelezeni jadi zetu tuache uzungu uzungu
 
Jephta2003

JF-Expert Member
Feb 27, 2008
5,311
2,000
Hahahah... I never thought kila anaechepuka n muhun bt cyo wote coz i hav experienced that issue and i hv come to realiz its nt bad at all acha wachepuke tu afu nkwambie kitu ukiwa hujawai fanya unaona wenzio wana dhamb cku ukifanya unatuliaa tuli wala umsem mtu... Cyo mbaya kuchepuka na mtu ambae ana heahim familia yako na anajali future yako and cyo kila mtu anatakiwa aolewe wanaume hawatosh and mwngne ameolewa n mateso tu bora upate zako mbaba anakuhandle naanakushaur to be somebody... I rather date a married man than mkaka ambae anntumia for sex nikimwambia twende kwetu hatak nkimnyima mgegedo ugomv sasa vya nn kujipa karaha akat hata mia mbovu ukipata shda akusaidii..... Life is full of mysterious things! I just said ts nt me!
Yaaani umenifurahisha mno
 
data

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
22,741
2,000
mi kutambulishwa sijui kufahamika inanisaidia nini muhimu huduma nnazo hitaji napata na mwanangu namsetia maisha yake mapemaa siwezi kubweteka kusubiri kugombea urithi na kweli wazee hawana presha maisha ya michepuko inaendelea wakati nyie wa ndoani mnakufa na presha kuwaza michepuko ya waume zenu. kingine wanaume ni wachache na katika uchache wao kuna wasoweza kazi na kina james lazima kugawana aisee
haya sasa..... maneno toka uvungu wa moyo kwa dada huyu. Patanuka hapa...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom