Mi nakuja na ushauri mwingine isitoshe skendo kama inayo karibia na kufanana na hiyo imenitokea hivi majizi. Japokuwa nilitaka mwenyewe.
Mi naona anaweza kuwa alikosea namba, lakini haamini kuwa si we, au amejua si wewe lakini ameona akunga'nganie.
Kisa changu kilikuwa hivi.
Ilikuwa asubuhi njema ya tarehe 3/09/12. nilifika katika stendi ya mabasi yaendayo arusha kwa ajili ya safari ya kurudi huku kazini kwangu (vichakani) Nikiwa katika stendi hiyo ya wilaya (jina kapuni) nilimuona binti mrembo ambae kwa dhalula nilijikuta nampenda, aroo alikuwa na umbo balaa, alikuwa na sifa za umbo na muonekano ambao nataka my ideal woman awe nao.
baada ya dakiaka kadha nilijisogeza kwa binti huyo, mara nikaanza kumchukua maelzo Binti huyo aliniambia kuwa anitwa Neema ( Surname kapuni) na ni mwalimu wa shule ya msingi wilayani humo kijiji kimoja hivi. Wakati zoezi la kumchukua maelezo likiendela mara basi likatokea tukapanda.
Baada ya kumchukua maelezo nilimuomba namba ya simu, lakini akachomoa. sikujali kwani nilijua kuwa namba yake naweza ipata ndani ya masaa machache hata kabla sijafika ninapoelekea.
Nilipofika mahali pa kushukia niliteremka, na abiria wengine waliteremka kwa ajili ya kupata lunch. awakati wanapata lunch Dereva aliekuja nifata alifika, basi nilichukua jukumu la kumwambia huyo dada nitampigia nikipata namba yake, hivyo nilimuomba apokee endapo ntampigia.
Waliendelea na safari yao ya kuelekea Arusha na mimi nikaelekea kazini kwangu.
Picha linaanzia hapa
Nilichukua hiyo namba na kuipiga, ilipokelewa na mdada mbae nilimkumbusha jinsi tulivyo kutana, basi niliendelea kumwaga swaga zangu mpaka huyo mdada akakubali. Tulipanga siku ya kukutana na siku yenyewe ilikuwa ni tarehe 17/10/12.
Nilichukua kijilikizob cha siku 14. Ilipifika tarehe 17 nilifunga safari ya kuelekea wilayani huko tuliko kutana. Nilipofika nilifikia sehemu moja ambayo tulikubaliana kuwa atakuja nichukua twende kwake
Huwezi mtu alie kuja nilikuwa sijawahi kumuona wala simufahamu. Kwa ustarabu nilimukalisha chini nikajaribu kumuuliza kama tushawahi kuonana, badala ya yeye kusema ukweli akaanza kulia akida kwmba ninavyomfanyia sio vizuri. Kutokana na urembo aliokkuwanoa huyo mdada ilibidi nimkubalie.
Tulienda kwake nakaka kama siku 5 alafu nikasepa. Lakini ukweli unabaki palepele kuwa huyo dada simjui na sikuwahi kumuona kabla ya siku hiyo laki I yeye anadai kuwa tulikuta. Hivi punde name ntaomba msaada kwa wana JF ili wanishauri jinsi ya kuachana nae kwani sina feelings nae hata kidogo lakini yeye kafa kaoza.
Hivyo basi hata wewe inaonekana huyo mtu anekuita john kachanganya namba kama mimi nilivyopewa namba feki nikajukuta nakutana na mtu nisie mjua.