Huu utani vijana wa Kibongo!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu utani vijana wa Kibongo!!!!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by ngoshwe, Aug 7, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Huu si utani kabisa kwa vijana wa Kitanzania . Ni barua ya maombi kazi hii ambayo mtu timamu aliyefuzu amekaa chini na kupoteza muda kuandika, akanunua bahasha na stempu kisha kuituma kwa ajili ya kutafuta kazi.

  Hivi kwa nini kama lugha ni shida kijana usiombe msaada wa waungwana wengine wasaidia hilo ?. Hali hii twaweza kweli kushindana kwenye soko la Jumuiya hizi tunazozing'ang'ania? ( Afrika Mashariki, SADC etc) .

  Kazi kubwa!!!

  securedownload.jpg
   
 2. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kha...!
   
 3. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  duh kazi ipo mazee
   
 4. T

  Thadeus JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2010
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 267
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Lakini jamani si mnaona kabisa kuwa "degree" yake ni ya VETA Changombe? Inaelekea huyu ni wa Std 7 akajiendeleza. Sidhani kama kwenye "degree" ya Changombe kuna somo la Communication Skills. Tumsamehe bure.
   
 5. S

  Survivor New Member

  #5
  Aug 7, 2010
  Joined: Aug 7, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni kulingana na elimu aliyoipata inatakiwa arudi darasani.
   
 6. Mahesabu

  Mahesabu JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2010
  Joined: Jan 27, 2008
  Messages: 5,043
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  GOOOD....! BIG UP DOGO....! AMEONYESHA KUJARIBU JAMANI......TUMPE PONGEZI ZAKE ZA KUTOSHA NA KUMTIA MOYO AJIENDELEZE ZAIDI.....! kwa kiwango alichokuwa amefikia na alivyojieleza amejitahidi sana..........! ila angekuwa amemaliza pale mlimani......jumlisha hayo maelezo......kweli angekuwa bado yupo mbali sana ....BUT THE YOUNG MAN HAS DONE GREATLY!
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  Aug 8, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tuwasaidieje vijana kama hawa?
  Leteni mawazo.
  Kwa upande wangu, maoni yangu ni haya:
  Kitu ambacho tunahitaji kukisisitiza ni kuwaambia vijana kama hawa wasilazimishe lugha kama haipandi. Huenda huko anakoomba kazi wametangaza kazi kwa lugha ya kiingereza na kijana kajikamua kweli kuwapa kile wanachotaka. Kama ndivyo, kijana amejitumbukiza tu kwenye matatizo zaidi, maana hata tuseme kaitwa kwenye usaili, lugha itamwangusha tu.Njia moja wapo ni kuwahimiza vijana kama huyu kujiendeleza zaidi kielimu ikiwa ni pamoja na kunyoosha lugha.

  Vyuo kama VETA navyo vingeweza kuweka module moja ya communications skills ili kuwasaidia vijana wanaohitimu pale wasije kujikuta kwenye hali kama ya huyu ambaye hata kuandika barua ya kuomba kazi ni tatizo.
   
 8. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #8
  Aug 8, 2010
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Kiingereza si cha kukurupukia, hii lugha ni ya wakoloni, walikuja nayo ili watugawanye na kututawala! Kiukweli hiyo ndio hali halisi ya wasomi wengi ndani ya Tanzania yetu, kwa ujumla nchi nzima haipo katika kutusaidia, maana ingekuwa suala ni kudumisha ushindani nchini basi tungeboresha lugha yetu na kuhakikisha ndio itumikayo kama lugha ya ofc, km wenzetu wameweza kwa nini sisi tushindwe! Kiingereza ni utumwa!
   
 9. P

  Pokola JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  :help: TEHE, MSIMCHEKE HUYO, KAJITAHIDI SANA BANDUGU. MIMI NAFUNDISHA UDOM SOMETIMES, HUWA NAKARIBIA KULIA KWA YALE NINAYOSOMA TOKA KWA PEPA ZA WANAFUNZI WA MIAKA YA JUU KABISA!!

  TUSALI USIKU NA MCHANA, TUIOMBEE TANZANIA JAMANI!!!
  :bored:
   
 10. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  WOS, Kuna vitu muhimu vya kufundishwa shule ya msingi na huwa vinarudiwa sekondari uandishi wa barua za kiingereza na kiswahili. Sidhani kama hilo somo lipo na kama lipo halina mkazo kabisa. Tatizo lipo kubwa sana na linahitaji ufumbuzi wa haraka. Simu nazo zimeta balaa kubwa lugha inafupishwa mpaka unashindwa kusoma eg ntakuja ofcn asap, kuna prob, 2kionana nitafurahi tkx & bi bi

  Huyu umwambie aandike barua ya kazi, walahi balaa
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mi sidhani kama tatizo hapo ni lugha tatizo naloliona mimi labda ni qualification. Mbona barua inaeleweka jamani inagwa kuna matatizo ya mpangilio wa syntax .

  Na haya matatizo yote huyu kaandika barua mwenyewe. Na anaonyesha anaweza kuwasiliana kwa kingereza japo kwa makosa lakini anaeleweka.

  Kama ni short list nadhani aliachwa basi sababu ya haki ni aliachwa sababu ya vigezo vya kitaaluma sio vigezo vya lugha.

  Kazi anayoomba wala haitaji uwe na uwezo mkubwa ya fashihi au sarufi ya lugha fulani. Ni kazi ya kifundi. So nothing wrong here kwa english kwa uyu inawezekana ni third language. barua safi fupi na kajieleza vizuri. Hata uko UK wascotish na wa welsh wanachapia sanalkingereza kwa kuongea na kwa maandishi.

  Tena unaweza kushangaa unayeweza lugha anaambiwa amuandalie barua jamaa anakuja ukurasa mzima wa maombi ya kazi. kama vile ana apply kwenda mwezini.
   
 12. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,354
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Kama ningekuwa Bosi ningemtafutia kazi yoyote atayoweza kuifanya na kumsaidia kumuinua kielimu inapowezekana hata kama shule yake ni ndogo! Watu kama hawa siyo wa kuwatupa,wana akili na juhudi.
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Binafsi nadhnai mbadala ni kuandika kwa lugha ya kigeni na kama huwezi vizuri ukaombe msaada wa kuiweka vizuri au vinginevyo ni kundika lugha yetu ya KIswazi ambayo inaeleweka. Kwa kawaida, barua ya maombi ya kazi si suala la majaribio kwani inapima uelewa wako katika yale unayotakwa kwenda kufanya. ukiandika katika lugha "mmbolongo" ni ngumu kueleweka hata kama unajua taaluma husika.
   
Loading...