Jana ilitokea nikawa naangalia kipindi cha 'take one' cha Zamaradi. Kuna binti ambay kwa umri anaonekana yuko chini ya miaka kumi na minane. Binti huyo anasema alikuja Dar Es Salaam kwa ajili ya kufuata ndoto yake ya kuwa mcheza sinema uki akimwacha mama yake anayeugua maradhi yanayoyokana na kukosa kinga za mwili. Aliendelea kufunguka kuwa mtu wa mfano kwake ni Lulu. Binti huyu aliingia Dar Es Salaam kwa maneno yako akiwa hajawahi kumjua mwanamume yoyote.
Habari ya dada huyu inasikitisha kwani anasema alikuja Dar Es Salaam akiwa na shilingi elfu thelathini tu mkononi. Akiwa Dodoma aliambiwa kwamba wasanii wengi wanapatikana maeneo ya Ilala. Alifika ubungo na kuelekea Ilala ambako hakukutana na msanii yoyote wa sinema. Matokeo yake akajikuta akiishi na mlinzi wa magari hapo Ilala. Mlinzi alianza kumtaka kimapenzi na ikabidi Dada akimbilie Sinza ambapo alikutana na Hemed. Hemed alimgandisha dada huyu mpaka kiza kikamkuta akiwa nje yanyumba hapo Sinza. Dada huyo katika kusubiri akakutana na wadada (sema: madada powa) ambao walichukua na kuanza kuishi naye hapo Sinza. Wadada hao walikuwa wakimfanyisha kazi za nyumbani na kumfungia ndani kama mtumwa na mwisho wakatumia ushamba wake kuanza kumletea wanaume. Binti huyu anasema kwamba mwanamume wa kwanza alikuwa anatokea Ilala na alikuwa na dalili zote za maradhi ya ukimwi. Jamaa huyu wa Ilala akutumia kinga katika kumwingilia kimwili huyu binti. Binti huyu aliendelea kusema kwamba kwa wastani alikuwa akilala na wanaume watatu kwa siku na alihishi katika nyumba hiyo kwa miezi mitatu mpaka alipofanikiwa kutoroka.
Binti huyu amepoteza matumani lakini anasema sasa hivi anataka kupima na kujua hali yake ya kiafya. Pili anaogopa hizi habari kumfikia mama yake kwani hajui kama ndoto yake ya kuwa muigizaji itatimia.
Kipindi kitaendelea wiki ijayo.
My Take:
Kwa nini Zamaradi na Wahariri wa TV Clouds hawakuilinda 'privacy' ya huyu binti ambaye ni mdogo kiumri na hajui madhara ya habari yake na picha kurushwa hewani? Maelezo yake yalikuwa 'graphical' na sijui lengo la Zamaradi lilikuwa ni nini? Kuuza kipindi ?