Huu sio UTU-kipindi cha TAKE ONE cha CLOUDS TV | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu sio UTU-kipindi cha TAKE ONE cha CLOUDS TV

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Shadow, Jul 25, 2012.

 1. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Jana ilitokea nikawa naangalia kipindi cha 'take one' cha Zamaradi. Kuna binti ambay kwa umri anaonekana yuko chini ya miaka kumi na minane. Binti huyo anasema alikuja Dar Es Salaam kwa ajili ya kufuata ndoto yake ya kuwa mcheza sinema uki akimwacha mama yake anayeugua maradhi yanayoyokana na kukosa kinga za mwili. Aliendelea kufunguka kuwa mtu wa mfano kwake ni Lulu. Binti huyu aliingia Dar Es Salaam kwa maneno yako akiwa hajawahi kumjua mwanamume yoyote.
  Habari ya dada huyu inasikitisha kwani anasema alikuja Dar Es Salaam akiwa na shilingi elfu thelathini tu mkononi. Akiwa Dodoma aliambiwa kwamba wasanii wengi wanapatikana maeneo ya Ilala. Alifika ubungo na kuelekea Ilala ambako hakukutana na msanii yoyote wa sinema. Matokeo yake akajikuta akiishi na mlinzi wa magari hapo Ilala. Mlinzi alianza kumtaka kimapenzi na ikabidi Dada akimbilie Sinza ambapo alikutana na Hemed. Hemed alimgandisha dada huyu mpaka kiza kikamkuta akiwa nje yanyumba hapo Sinza. Dada huyo katika kusubiri akakutana na wadada (sema: madada powa) ambao walichukua na kuanza kuishi naye hapo Sinza. Wadada hao walikuwa wakimfanyisha kazi za nyumbani na kumfungia ndani kama mtumwa na mwisho wakatumia ushamba wake kuanza kumletea wanaume. Binti huyu anasema kwamba mwanamume wa kwanza alikuwa anatokea Ilala na alikuwa na dalili zote za maradhi ya ukimwi. Jamaa huyu wa Ilala akutumia kinga katika kumwingilia kimwili huyu binti. Binti huyu aliendelea kusema kwamba kwa wastani alikuwa akilala na wanaume watatu kwa siku na alihishi katika nyumba hiyo kwa miezi mitatu mpaka alipofanikiwa kutoroka.
  Binti huyu amepoteza matumani lakini anasema sasa hivi anataka kupima na kujua hali yake ya kiafya. Pili anaogopa hizi habari kumfikia mama yake kwani hajui kama ndoto yake ya kuwa muigizaji itatimia.
  Kipindi kitaendelea wiki ijayo.

  My Take:
  Kwa nini Zamaradi na Wahariri wa TV Clouds hawakuilinda 'privacy' ya huyu binti ambaye ni mdogo kiumri na hajui madhara ya habari yake na picha kurushwa hewani? Maelezo yake yalikuwa 'graphical' na sijui lengo la Zamaradi lilikuwa ni nini? Kuuza kipindi ?
   
 2. kwamtoro

  kwamtoro JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 4,815
  Likes Received: 770
  Trophy Points: 280
  Clouds pale vihiyoo wamejaa kila idara. Wengine mashoga, kazi kweli kweli
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Zamaradi mwenywe zinamtosha?

  Utamlindaje mwenzio kama wewe mwenyewe kujilinda hujui?

  Wengine wa kusamehe bure tu, ndo maana mie hiyo TV siangaliagi kabisa iwe take one au take 2.
   
 4. mysteryman

  mysteryman JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyo zamaradi ni kilaza tu na hao tv ya wafu ma editor wao pia ni vilaza tu.....niliona jana nilikereka sana
   
 5. s

  slym Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Zamaradi mwenyewe kazaa na bosi wao, sasa si ajilinde kwanza yeye.
   
 6. stephot

  stephot JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 5,023
  Likes Received: 2,641
  Trophy Points: 280
  Aisee,hata mie ile show yake ya jana haikunifurahisha,privacy ilikuwa kitu cha kwanza ukizingatia umri wa yule binti ni mdogo sana ku-expose mambo kama yale.
   
 7. Advocate J

  Advocate J JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: May 24, 2012
  Messages: 3,880
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Hasara za kuweka vilazaform4 d 6 tu ,uhandish wa habari,alaf watangazaj wake hawana maadil na uwez compare na tbc .
   
 8. stroke

  stroke JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 13,387
  Likes Received: 6,563
  Trophy Points: 280
  Atleast wangeficha sura yake, kutokana na udogo wa umri wake, tis was very unproffessional
   
 9. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,823
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  Hivi huy anatofauti gani na yule mama fulani jana bungeni aliesema "kuna watanzania wana maumbile makubwa" kwa hio kuvaa kanga moja sio sahihi
   
 10. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Tatizo wote hao hawana ETHICS za utangazaji sijui wanaokoteana wapi?. Kwa kujua hilo naloongea ni sahihi ni kwamba 2011 CNN Africa award hata katika Top 34 Jounalist in Africa hakuna Mtanzania alietia maguu. Can u imagine?
   
 11. Opaque

  Opaque JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 24, 2008
  Messages: 1,138
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyo Zamaradi ndio yule aliyeonyeshwa 'nyumba ya kifahari ya Wema'?
   
 12. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Duh mchungaji anakula kondoo alienona?
   
 13. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,790
  Likes Received: 6,303
  Trophy Points: 280
  Watu wametoka kuwa maMC vichochoroni straight kwenye TV - unategemea nini?
   
 14. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,131
  Likes Received: 943
  Trophy Points: 280
  Halafu yale maswali Zamaradi alokuwa akimwuliza huyo msichana! Mtumeeee! Yalikuwa ni maswali saizi ya madada poa wa kona bar!
  Naungana na wanaJF wote kwamba kipindi cha take one j4 tarehe 24/7/2012 hakikuzingatia maadili ya utangazaji.
   
 15. mtzd

  mtzd Member

  #15
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Wana JF kwa waliobahatika kuangalia kipindi cha Take One kinachorusha na kituo cha Tv cha Clouds jana tarehe 24/July kwa yale niliyoyaona nadhani kwa wenye taaluma ya uandishi wa habari watakubaliana na mimi.Kuna jambo nadhani kwa maono na fikra zangu sio la kiutu kwa kweli,kwa wale ambao hawakubahatika kuangalia naomba niwaelezee japo kwa ufupi,-Kuna msichana aliyetoka Dodoma na kuja Dar kuja kutafuta kazi na ndoto yake ilikua aje awe muugizaji,kutokana na maelezo yake aliyoyatoa alipokua akihojiwa na Zamaradi ambaye ndiye Host wa kipindi hiki,anasema alipewa nauli ya kuja dar na mama yake mzazi na alipofika dar alishukia Ilala ambapo kutokana na maelezo yake aliambiwa ndipo wanapoishi wasanii wengi aliopata kuwaona kwenye baadhi ya filamu za kitanzania,basi alipofika alipata mahali kwa mzee mmoja ambaye inasemekana kazi yake ni mlinzi,alikaa pale kwa muda na mzee alimsaidia kwa chakula,ilifika kipindi yule mzee akawa anamtaka kimapenzi hata ikafikia yule mzee kumwonyesha sehemu zake za siri,ikabidi ahame na kutafuta kazi kwa mtu.

  Baadae akawa anaishi sinza na wasichana ambao inasemekana walikua wanafanya kazi ya kujiuza.Walimshawishi naye kujiingiza kwenye biashara hii ambayo ndio ilikua inampatia riziki yake,kutokana na taarifa yake alishiriki tendo la ndoa na wanaume zaidi ya 20 na wengine bila kinga.Na anasema wale wasichana walimlazimisha,imefika kipindi sasa anataka kwenda kucheki afya yake na anasema mmoja ya wanaume aliowahi kushiriki naye tendo la ndoa ni muathirika,alielezea kwa majonzi na masikitiko kweli na alikua anasema asingependa mamake ajue hili.Msichana mwenyewe bado ni mdogo anasema ana umri wa miaka 17.

  Kilichonifanya niandike hili ni jinsi walivyomwonyesha msichana huyu ,nadhani kama mtayarishaji wa kipindi hiki alipaswa kutoonyesha sura yake,tumeona masuala kama haya ni ya kinyanyasaji kijinsia kwani walipaswa kutomwonyesha sura yake,hii inamuweka kwenye mazingira hatarishi zaidi kwani wale ambao amekua nao kwa mfano alisema alilazimisha kufanya nao mapenzi wanaweza kumdhuru na pia kimaadili sio vizuri kwani wapo watu wa umri na jinsia kama yake ambao nao inaweza kuwaadhiri.Lingine ni yeye kutotamani mamake kumwona na kujua alichofanya.

  Maskini ndoto zake iliikua aje dar kutafuta maisha kwani mama yake na mdogo wake ndio wanamtegemea yeye lakini amejikuta akiishia kwenye maisha ambayo hakutegeme.Nifundisho ndio alikua anatoa kwa wengine ambao nao labda ndoto zake ni kama zake lakini kwa jinsi ilivyoonyeshwa nadhini sio Ki UTU na KIMAADILI,Tumekua tukiona kwa mfano wale waliobakwa au kufanyiwa ukatili wa namna kama hii wakionyeshwa kwenye vyombo vya habari bila sura zao na hata majina yao kutoonyeshwa lakini kwa hii ilikua tofauti.Naomba kama kuna wahusika wa haki za binadamu na wanaojua kuhusu hili waone jinsi wanaweza kulichukulia sheria ili lisiweze kutokea tena au hata kama ni funzo walikua wanatoa waangalie jinsi ya kuwakilisha jambo kama hili kwenye jamii.
   
 16. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #16
  Jul 25, 2012
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Tunawezaje kumsaidia dada huyu na hasa kuwashtaki hao watu hao 'waliomteka' na kumfyanya mtumwa kwa manufaa yao? Kama kuna mtu anaweza kumwongoza huyu binti aweze kufika katika mashirika ya kutoa misaada ya kisheria itakuwa ni bora zaidi.

  Je, hawa Clouds wanaweza kupelekwa kwenye baraza la walaji la TCRA (Consumer Consultative Council) etc kwa kutofuata maadili ya kurusha habari?
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Jul 25, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  aiseeeee.......
   
 18. C

  Cashbonnie88 New Member

  #18
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ndio ndugu
   
 19. mtzd

  mtzd Member

  #19
  Jul 25, 2012
  Joined: Jan 29, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Kweli ilikua inasikitisha sana,Hawa Clouds siju hawajali utu,Huyu Zamardi naye sijui katumwa,imagine tena ni mwanamke mwenzake ,nadhani ndio angechukua picha yake kama mwanamke na jinsi ya kumsaidia mwanamke mwenzake,sijui nini mwisho wake .
   
 20. BASIASI

  BASIASI JF-Expert Member

  #20
  Jul 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 3,109
  Likes Received: 345
  Trophy Points: 180
  sasa haya matusi bosi kashindwa kujilinda ajilinde nini huyu na e yeye aachie tu watu tutafute hati za kudumu pale kinondoni cementry
   
Loading...