Huu ni uonevu, haki iko wapi ? Tukianza hivi je, tutafika ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu ni uonevu, haki iko wapi ? Tukianza hivi je, tutafika ?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mag3, Nov 5, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Washtakiwa kwa kumdhalilisha Kikwete - nipashe

  Mwalimu na mwanafunzi wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, mkoani Kilimanjaro wakikabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi na kuchapisha matoleo ya aibu kwenye Mtandao wa Facebook dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.
  Kesi hiyo namba 677/2010 inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Simon Kobelo, ambapo washtakiwa hao walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu John Nkwabi kutokana na Hakimu Kobelo kutokuwepo mahakamani.
  Washtakiwa hao ni Mwalimu Frednand Urio (25) ambaye ni mwalimu wa eneo la Marangu Komelo na mwanafunzi Daniel Mataji au RobinDaniel ni mkazi wa KDC Kiborlon.
  Wakili Mwandamizi wa Serikali,Veritas Mlay, akiwasomea washtakiwa hao mashtaka hayo, alidai shtaka la kwanza la Urio ni kuchapisha matoleo ya aibu dhidi ya Rais Kikwete kinyume na kifungu namba 175(1) (a) ya Kanuni ya Adhabu kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
  Alidai kuwa Urio kati ya Machi Mosi na Septemba mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete.
  Mlay alidai kuwa mshtakiwa huyo pia anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu namba 32 (1) cha sheria ya Magazeti namba 229.
  Alidai kuwa kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu katika Manispaa ya Moshi, mshtakiwa huyo alisambaza picha zakumdhalilisha Rais Kikwete.
  Katika shtaka la tatu alidai kuwa mshtakiwa Daniel ambaye ni mwanafunzi anakabiliwa na kosa la uchochezi kinyume na kifungu hichohicho cha Sheria ya Magazeti.
  Alidai mshtakiwa huyo kati ya Machi Mosi na Septemba 30 mwaka huu, alichapisha picha za kumdhalilisha Rais Kikwete kwenye mtandao wa Facebook.
  Washtakiwa hao walikana mashtaka hayo na ambapo Hakimu Nkwabi aliwaelezamasharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili na Sh.million mbili.
  Washtakiwa hao walishindwa kukidhi masharti ya dhamana na hivyo kwenda mahabusu hadi Novemba 17, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.


  Kwa nini serikali inawashtaki, kwani ndiyo mlalamikaji ?
   
 2. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini ameruhusu mashtaka hayo yaendelee kwa kuwa aliyedhalilishwa sio 'Jakaya Kikwete' bali ni Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na hivyo ni kuwadhalilisha Watanzania.
   
 3. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,716
  Likes Received: 3,126
  Trophy Points: 280
  Kama kudhalilishwa amedhalilishwa jk inatuhusu nini sisi kama watanzania.Eti amewadhalilisha watanzania Kwani watanzania wote wanaitwa jk??
   
 4. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sitosita kukuelimisha Ndugu yangu. Iwapo unamchukia JK, hio ni haki yako; yeye ni Public Figure na it is obvious kuwa hatopendwa na kila MTU. Kinachopaswa kueleweka hapa, ni kwamba Jakaya Kikwete ni MTU na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni TAASISI. Ieleweke kuwa Jamhuri imechukua hatua hizo kwa kuzingatia kuwa TAASISI ndio iliyodhalilishwa na kitendo hicho kimewadhalilisha WATANZANIA wanaoongozwa na TAASISI hiyo.

  PILI, hakuna mahakama itakayoendekeza mashitaka yasiyo na mashikio; yangetupiliwa mbali.

  TATU, wala mashitaka hayo yasingefika mahakamani, kwani Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini asingeliruhusu mashitaka hayo yawasilishwa mahakamani.


  NAWASILISHA
   
 5. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kwa taarifa ya vilaza wa Tanzania serikali itashindwa kesi hiyo na kulipa pesa nyingi kwa wahusika.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo ulaya wale wanaowachora chora kina Bush ,Clinton,Tony B wote wangekuwa ndani
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Freedom of Speech is violated Here..
  hawa wamechangia kuhamasisha upinzani kwa CCM mkoa wa kilimanjaro,hivyo wanapata Adhabu na kuwa kama mfano kwa wengine.
  Kipindi hichi ni kipindi cha Kampeni,na mashtaka yao yako related na Kampeni za uchaguzi zilizopo,hivyo basi Mwendesha mashtaka,Hakimu wangetakiwa kutumia busara ,na kuliondoa shauri hili mahakamani,kwani halituwakilishi watanzania-wana wa Nchi hii.
  kinachotakiwa wapewe onyo,wafanye kazi za Jamii-comunity service Full stop
  Shauri likiendelea ingefaa lipelekwe kwa Int.Human Rights Lawyers walitazame
   
 8. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  :smile-big: First Lady tafadhali sana naomba uondoe hilo neno. Hapo unafananisha mguu kwa kidole:wink2:
   
 9. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kinacho hitajika hapa ni busara tu na si kashfa,kwa maelezo ya baadhi ya watu hapo juu,ina maana kila mtu anaruhusiwa kutukana tuu kisa ni chombo cha habari?hapana hapa katukanwa raisi wa nchi ambaye ni sawa na mtu mwingine yeyote yule ambaye anatakiwa alindwe na sheria za nchi.kwa hiyo tuache kutoa hukumu kabla ya hukumu,
   
Loading...