Huyo sijui ni samaki ama kitu gani ila yupo mfano wa huyo nilimuona ufukwe wa mbezi aliingia katika wavu wavuvi wote watoka nje ya wavu sasa sikuelewa kwanini kilinuka baharini, wakasema kuna samaki yupo ndani ya nyavu sio ni muuaji yaani huyo akikugusa tu kwanza lazma uzame na ukiibuka ushadedi.
Kingine nilichoshuhudia walifanikiwa kuzivuta zile nyav mpaka ufukweni na nilimuona samaki kama huyo apo, sasa haikupita dakika tatu akaanza kubadilika akawa mweusi kama mkaa ndio jamaa wakasema huyo samaki ana umeme akiwa ndani ya maji na ana sumu mbaya sana kinachombadilisha hapo na kumuua ni sumu yake mwenyewe.
Tangu ile siku nikapunguza kuogelea maji marefu maana nilikuwa na udwanzi fulani sio yaan naenda mbali kiasi mpaka ile minazi ufukweni inanipotea machoni nazuga zuga hukoo kisha narudi mdogo mdogo (kuna samaki flani wanapenda kucheza wanakuja wengi alafu wakikukaribia wanatawanyika kule katika maji mengi yanakuwa kama kioo unaona vizuri tu ndani ya maji, lakini tangu nimuone yule samaki aisee niliingiwa na uoga naogelea kwenye mchanga maji ya ugoko.