Kwa wale wasiogopa majini angalieni hizi picha za majini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
165064_492159844170258_510225546_n.jpg



190776_488280031224906_1654855159_n.jpg

Usijali mimi JINI nakutakia kila lam kheri


734903_487348407984735_1872153898_n.png

540269_482083241844585_1203274767_n.jpg

JINI WA KULETA PEA HUYOOOOOOOOOO

Majini ni nini?
Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa Moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita.
Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;

Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.

Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vile

vile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.

Taifa la Majini limegawanyika katika makabila Milioni Sabini na mbili (72,000,000) na wana uwezo wa kujifunza lugha yeyote wanaoitaka.

Idadi ya Majini ni kila Binadamu mmoja kuna Majini 300 na wanaishi katika Majumba yetu, kwenye Miti, Majangwani, Kwenye Mapango na Sehemu zenye Misitu Mikubwa.


Majini wako katika aina Mbili (2); Maruhani na Mashetani.

Maruhani ni Majini wema ambao wanamtii Mwenyezi Mungu na wanawasaidia Binadamu katika mambo mengi.
Mashetani ni Majini Waovu ambao ni wakorofi na wanawaletea Watu madhara na Matatizo mara kwa mara.
Baba wa Majini anaitwa JANN ambaye kimaumbile yeye ana tofauti ndogo na wenzie kwamba yeye ameumbwa kwa ulimi wa Moto.

Pamoja na mambo mengi wanayoyafanya Majini na kujihusisha na binadamu, Majini vilevile wanafanya kazi za Malaika hasa zile za mambo ya kupeleka Habari na kuwalinda Binadamu, mambo ya doria za Angani. Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda kuiga mambo basi huiga hata kazi ambazo siyo zao.


Majini na Binadamu wana sifa zinazofanana kwani wote wana akili na wote watahesabiwa siku ya Kiama na watazawadiwa kwa mema yao na maovu yao, wote wanakula na kuzaa.

Kama ilivyo, kuna wataalamu wa Kijini wenye fani sawa na Wataalamu wa Kibinadamu wenye kufanya kazi zinazofanana.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya Majini na Binadamu ni kwamba; Majini hawana maumbile maalum na wana uwezo wa kujibadilisha katika maumbile mbalimbali ingawa wengi wa Majini wapo katika maumbile ya paka, nyoka na ndege.

Binadamu wao wana umbile maalum ambalo halibadiliki.
Majini wana uwezo wa kuwaingia Binadamu wakati Binadamu hawana uwezo wa kuwaona Majini isipokuwa kwa ufundi maalum.

Namna Majini wanavyowaingia Binadamu iko katika njia tatu:-



  1. [*]Njia ya kwanza (1): ni kama Remote Control; Hii inamfanya yule aliyedhibitiwa kuweza kuelewa au kuwa na fahamu zake lakini anakuwa hawezi yeye mwenyewe kuudhibiti mwili wake na anasema yale anayotaka yule Jini.
  2. Njia ya Pili (2); Jini humwingia Binadamu ndani ya utosi na kuingia katika Mfumo wa Damu. Hii inamfanya yule Binadamu kupoteza fahamu na anakuwa haelewi kabisa kinachoendlea na anafanya yote anayotaka yule Jini.
  3. Njia ya Tatu (3) ni ile ya Jini kukaa nyuma ya Binadamu. Njia hii humfanya yule Binadamu anakuwa hapotezi fahamu ila anakuwa hawezi kufanya lolote na mwili wake.
{mospagebreak}

Majini vilevile wana uwezo wa Kusafiri kwa kasi ya upepo bila kutumia chombo chochote; Binadamu hana uwezo huo isipokuwa kwa msaada wa Majini.


Hiyo ni kusema kwamba mambo yote yanayofanywa na Wachawi na Wanga hayawezekani isipokuwa kwa msaada wa Kijini.


Jambo la muhimu ni kwamba pamoja na uwezo mkubwa walionao Majini, Wanadamu wana uwezo wa Kumtawala na Kumdhibiti Jini na vivyo hivyo Majini nao wanaweza kumtawala na kumdhibiti Binadamu wote kwa kutumia utaalamu maalum.

Wako Majini wa kila Dini na kila Kabila, na kuna watu wanaofuga Majini kwa kujikinga, na kwa kuboresha kazi zao au kujipatia utajiri. Pia kuna watu wanaofunga ndoa na Majini kwa kutumia utaalamu au kwa hiari za Majini hao.

Wabaya wa Majini ni Mashetani ambao wengi hawana Dini na ndio wanaoharibu mimba za Wazazi na kufanya mapenzi na watu usingizini bila hiari zao.

Kuepuka usichafuliwe kimapenzi, kabla ya kulala piga Bismillahi kwa Muislamu au taja jina la Yesu mara tatu kwa Mkristo.

MAUMBILE YAO YAKOJE?



  • [*]Majini wana maumbile makuu manne (4);
    [*]Wanakuwa katika maumbile ya Nyoka.
    [*]Wanakuwa katika maumbile ya Nge.
    [*]Wanakuwa katika maumbile ya Mbwa.
  • Wanakuwa katika maumbile ya Paka (Mweusi).
  • Kuna Majini wengine hawana maumbile yeyote na hawa shughuli yao ni kuruka hewani kuzunguka huku na kule na husafiri mbali kwa mara moja yaani kufumba na kufumbua.

SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:


Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama Matunda ya Mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.

Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama Jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.

Fitna na Maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki.

Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu Majini wanapenda Rangi Nyeusi kwa sababu ya kiza.

WANAKULA NINI?


Majini wao wanakula mifupa na mavi ya farasi. Hivyo ni vyaluka vyao vikuu pamoja na kwamba wengine wanakula Moshi (Ubani) na wengine wanapenda kunywa damu.


Wanapokula au kunywa, wao hutumia mkono wa kushoto na Majini wazuri ndio ambao wanakula mifupa mizuri na kuwaachia mifupa mibaya na uchafu Majini wabaya au Mashetani.


JE MAJINI WANAZAA?


Majini wanaoa na kuongezeka kama tulivyo Binadamu na huzaana kwa wingi sana.

Katika wao kuna wale wanaokula na kuoana na kuna wale ambao hawafanyi hayo.

Binadamu Mwanamume ana uwezo wa kumuoa Jini Mwanamke na Jini wa Kiume ana uwezo wa kumuoa Binadamu Mwanamke pamoja na kwamba ndoa inayotambulika na Mwenyezi Mungu ni ya kiumbe kwa kiumbe yaani Binadamu kwa Binadamu na Jini kwa Jini.


Haya ni baadhi ya maelezo kuhusu Majini, zidi kutembelea tovuti hii mara kwa mara kwani hii ni mwanzo tu na tutazidi kuwaletea habari za ndani kuhusu majini na tabia zao, jinsi ya kujikinga nao au kushirikiana nao.





JE UNAWEZA KUWAONA MAJINI?

Majini hawawezi kuonekana kwa macho ya kawaida ila kwa Utaalam Maalum, ingawa Mtu yeyote unaweza Kumuita, Kumuona na hata Kumtuma Jini akufanyie au akuletee kitu chochote kile Naye akafanya vivyo hivyo kama

ulivyomuagiza; katika njia Rahisi kabisa kama inavyoelezwa hapo chini. Wao wana uwezo wa kutuona sisi.

Viumbe ambao wana uwezo wa kuwaona Majini au Mashetani kwa macho yao ni Mbwa na Punda

Ukimsikia Mbwa anabweka bila sababu yeyote basi atakuwa amemuona Jini au Shetani yuko karibu au anapita. Maelezo haya yamethibitishwa na Wanazuoni kuhusu kuonekana vile vitu ambavyo sisi hatuvioni.


Mfano mwingine ni kwamba Sisimizi ana uwezo wa kuona miale ya mwangaza yenye rangi ya urujuani na kwa hiyo kuona Jua litokeapo kwenye mawingu na Popo nae ana uwezo wa kumuona Panya kwenye giza nene.


KUMUONA JINI:


Iwapo unataka kwa haraka kuona Majini na kuwatumia; tamka Majina haya MARA 1,000;



  • [*]1. Salsal, Salsal ........................x 1,000.
  • 2. Akmash, Akmash..................x 1,000.
  • 3. Laash, Laash..........................x 1,000.

Tamka majina hayo hapo juu, huku ukiwa unafukiza Ubani Maka, Kuzbara na Majani ya Mnazi wa Kipemba au majani ya Mtende au majani ya Mchikichi.

Ukiwa sawa (yaani uwe msafi, mahali safi na nguo safi); atakutokea Paka mweusi au Taa kuzimika au kutokea Moshi mweusi.

Ndio huyo – Muagize lolote lile ulitakalo; akuitie Mpenzi, Pesa, cheo au Ushindi.

Ni vizuri pia ujue ni wakati gani au ni Sayari gani inayotawala ili ujue ni Jini yupi atakaekuja.

Unashauriwa;


  • Uwe na nia ya kweli na wala si mchezo au kufanya majaribio.
  • Usiwe muoga, kwani iwapo utakuwa muoga anaweza kukudhuru.


Kuwatumia au Kujikinga na Majini

JE MAJINI WANAWEZA KUTUMIKA?

Majini wanaweza kutumika kwa kazi mbalimbali ambazo Binadamu anaweza kumtuma.

Mwenyezi Mungu aliwaamuru Majini wamtumikie Mfalme Suleimani na wakawa wanamfanyia Kazi kadri anavyotaka yeye.

Katika Biblia 1 Wafalme 5: (13-17).


Biblia inaeleza jinsi nyumba ya Suleimani ilivyokuwa ikijengwa kimya kimya. ... "Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwishachongwa chimboni, wala nyundo wala shoka, wala chombo cha chuma chochote sauti yake haikusikika ilipokuwa ikijengwa Nyumba".


Majini vilevile wanatumiwa na watu katika kupata habari za mambo mbalimbali kwa sababu wao wana uwezo wa kupata habari angani.


Majini vilevile wanatumika katika ulinzi wa kulinda majumba au kulinda watu au Mikutano au Shughuli yeyote na vilevile wanaweza kutumika katika vita.

Wao wanajigeuza katika maumbo aidha ya Binaadamu au Mnyama na kushiriki katika vita.

Mfano Shetani mmoja alijigeuza kwa mfano wa Binaadamu mmoja aitwae Saraqa Bin Malik na kushiriki vita vya Badri na kuwaahidi Makafiri ushindi mkubwa lakini alipoona Majeshi mawili ya Malaika wanateremka kutoka Mbinguni alitimka na kutoroka.


JE TUNAWEZA KUJIKINGA NA MASHETANI?


Zipo njia nyingi za kujikinga na Mashetani lakini kubwa zaidi ni kutumia Jina la Mwenyezi Mungu na kumtaka Mungu akuepushe na Shetani mbaya Naye atakusaidia.


Shetani ana Maudhi mengi sana kwa Binadamu kwa sababu anapenda kujishirikisha na Binadamu katika kila kitu kama vile katika kula, kunywa, kufanya Mapenzi, kutembea, Kuishi ndani ya Nyumba na hupenda kufanya hayo yote pale Mwanadamu anapopotea na kumsahau Mwenyezi Mungu.


Shetani vilevile anamgusa kila Mtoto anayezaliwa katika dunia hii. Mtoto ambaye hajaguswa na Shetani ni Yesu au Issa Bin Maryam hayo ni kwa mujibu wa maelezo ya Qurani na Mtume Muhammad (SAW).


Mashetani vilevile ndio wanasababisha Ugonjwa wa Tauni (Plague – Ugonjwa unaoambukiza). Mtume Muhammad (SAW) ameeleza "Hakika kuangamia kwa Umma wangu kunatokana na kushuka Hadhi yao na Ugonjwa wa Tauni na Adui yenu Mkubwa anatokana na Jini, na Hiyo kwenu ni Shahada".


Hivyo basi ili kujiepusha na maovu ya Shetani unashauriwa kumweka mbele Mwenyeezi Mungu katika lolote unalolifanya ukiwa Nyumbani au popote pale.


Haya ni baadhi ya maelezo kuhusu Majini, zidi kutembelea tovuti hii mara kwa mara kwani hii ni mwanzo tu na tutazidi kuwaletea habari za ndani kuhusu majini na tabia zao, jinsi ya kujikinga nao au kushirikiana nao.





Marafiki na Maadui wa Majini

MARAFIKI WA MAJINI:

Majini huwa wanafanya Urafiki na Binadamu lakini Marafiki wao wakubwa ni Ngamia.

Baadhi yao wanaishi katika nyumba tunazoishi na ukitaka kuwafukuza unasoma Quran au Biblia au kumtaja Mwenyezi Mungu.

Majini hukusanyika na kuongezeka giza linapoingia au unapopatwa Mwezi, na huwa wanakimbia wanaposikia Adhana au Kengele ya kamba.

Majini wengi wanapenda kukaa baina ya kivuli na jua na siyo vizuri kukaa eneo hilo.

SURA ZA MAJINI NA MASHETANI:


Majini sura zao ni za kutisha na mfano wake ni kama Matunda ya Mti wa Zaqum ambao unatoa matunda yenye sura mbaya na yanayofanana na mawe.


Majini wanakuwa na mkutano kila siku nyakati za kuchomoza na kuzama Jua na nyakati hizo ndizo ambazo wanafanya maasi yao.


Fitna na Maasi yao mengi wanafanyia upande wa Mashariki.

Majini vilevile wanaweza kujigeuza kama mbwa mweusi au paka mweusi kwa sababu Majini wanapenda Rangi Nyeusi kwa sababu ya kiza.

UADUI WA MAJINI NA BINADAMU:


Majini na Binadamu wana Uadui wa asili tangu pale Binadamu alipoumbwa na kabla Mwenyezi Mungu hajampulizia Roho; Shetani akawa anauzunguka mwili wa binaadam na kusema "Nikipewa Uongozi juu yako basi nitakufanya uwe Aaswi (Usimsikilize Mola wako) na ikiwa utapewa wewe Uongozi basi nitakuangamiza".

Mungu alipompulizia Roho Adamu aliwaamrisha Ibilisi na Malaika wamsujudie lakini Ibilisi alikataa kwa kusema kwamba Yeye ni bora kuliko Binadamu.

JE MAJINI WANAKUFA?

Majini na Mashetani nao wanakufa isipokuwa wao wanaishi miaka mingi kuliko Binadamu kwa sababu hawana maumbo maalum.

TUNAWEZA KUWAUA MAJINI?


Majini tunaoishi nao nyumbani mwetu tunaweza kuwaua kwa kutumia utaalamu Maalum. Lakini kabla ya kufanya hivyo unatakiwa umuadhinie mara tatu Kidini yako au Umtaje Mwenyezi Mungu mara tatu; asipobadilika au

kuchukua mfano mwingine muache, lakini akibadilika muuwe huyo atakuwa Shetani.

Shetani anapohisi Binadamu anataka kumdhuru basi hukimbia kama vile damu inavyokimbia kwenye mishipa ya damu.




Uchawi Makaburini

Ifuatayo ni sehemu ya Vipindi mbalimbali vya Television vya Nyota Zenu kama jinsi ambavyo vimerushwa katika TV ya Channel 10 na hapa ni sehemu ya Vipindi hivyo.
Sehemu ya Video inayoonyesha namna watu wanavyofanya Uchawi Makaburini.





MAUMBO NA SURA ZA MAJINI KULINGANA NA SAYARI ZAO
1. Majini wa Saturn (Zohal) - Majini wa Jumamosi

Majini hawa huwa ni warefu, wembamba na wenye sura ya ukatili na kutisha, wana nyuso nne ambazo kila moja iko kila upande wa kichwa, yaani kwa mbele na nyuma sura inakua na midomo kama ya ndege.



  • [*]Pia wana sura nyeusi inayon'gaa katika kila goti. Mwendo wao ni kama mwendo wa upepo ambao huambatana na radi.
    [*]Alama yao ni ardhi nyeupe kuliko theluji.
    [*]Umbo lao maalum ni kama Mfalme mwenye ndevu anaemuendesha DRAGON.
    [*]Umbo lingine ni la mtu mzee mwenye ndevu
    [*]Umbo lingine ni la Bibi kizee ambae anaegemea kitu
    [*]Umbo lingine ni la Mvulana
    [*]Umbo lingine ni la Dragon
    [*]Umbo lingine ni la Bundi (Owl)
    [*]Umbo lingine ni la Nguo nyeusi isiyo na mwili
  • Umbo lingine ni la Ndoano au Mundu
  • Umbo lingine ni la mti wa Mreteni

2. Majini wa Jupiter (Mushtara) - Majini wa Alhamisi


Majini wa sayari hii wanakuwa na mwili mwekundu na umbo la kati siyo wakubwa wala siyo wadogo, mwendo wao na mwondoko wao ni wa kutisha na wa kuogopesha lakini na wapole na wanao ongea taratibu.


Wana rangi ya chuma ambayo inawaunganisha wao na Sayari ya Mars (Mariikh). Mwendo wao ni ule wa umeme ukiambatana na ngurumo za radi.



  • [*]Alama yao ni ya mizuka ya watu ambao miili yao ni kama iliyojeruhiwa na Simba.
    [*]Umbo lao maalum ni la Mfalme mwenye Upanga akiwa mgongoni mwa Simba akimwendesha.
    [*]Umbo lingine ni la Mtu aliyevalia rasmi Nguo za Chuma za Kivita.
    [*]Umbo lingine ni la Kijakazi aliyevaa Taji lililopambwa kwa Maua.
    [*]Umbo lingine ni la Ng'ombe Dume.
    [*]Umbo lingine ni la Paa dume
    [*]Umbo lingine ni la Tausi
    [*]Umbo lingine ni la Nguo ya rangi ya bluu isiyokua na mwili.
  • Umbo lingine ni la Upanga.
  • Umbo lingine ni la Mti wa Mbuyu.
{mospagebreak}

3. Majini wa Mars (Mariikh) - Majini wa Jumanne


Majini wa Mars (Mariikh) wanakuwa na Umbo refu, Mwili Mwekundu, mchafu na hutoa harufu yenye kutia kinyaa. Huwa wanajitokeza pia katika mwili wenye rangi Nyekundu, Kahawia au Nyeusi. Wana mapembe kama ya mnyama aitwaye Ayala (Hart), kucha kama za Simba, Wanatoa sauti kama za Nyati (Mbogo).



  • [*]Mwendo wao ni kama mwendo wa moto unaowaka na Alama yao ni radi na umeme unaowaka kwa katikati.
    [*]Umbo lao maalum ni la Mfalme aliyevalia kivita akiwa amempanda Mbweha (Mbwa mwitu).
    [*]Umbo lao lingine ni la Mwanamme aliye na silaha.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliyeshikilia Ngao kwenye mapaja yake.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mbuzi Jike.
    [*]Umbo lao lingine ni la Farasi.
    [*]Umbo lao lingine ni la Paa.
  • Umbo lao lingine ni la Nguo Nyekundu isiyokuwa na mwili.
  • Umbo lao lingine ni la Sufi.

4. Majini wa Sayari ya Jua (Shams) - Majini wa Jumapili


Majini wa Sayari ya Jua (Shams) wana viungo na umbo la kati, wasiovutia na dhalimu, wana Sura nyekundu na rangi ya dhahabu iliyochanganyikana na Damu.


Mwendo wao ni mfano wa Umeme na Alama yao kubwa ni kusababisha mwenye kumuita kutokwa na jasho jingi (ambapo hii ni kawaida kwa Viumbe hivi ambavyo ni vigumu kuelezeka).



  • [*]Umbo lao maalum ni la Mfalme aliyebeba fimbo ya kifalme huku akiwa amempanda Simba.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mfalme aliyevikwa Taji.
    [*]Umbo lao lingine ni la Malkia mwenye Fimbo ya Kifalme.
    [*]Umbo lao lingine ni la Ndege wa aina yeyote isipokuwa wale ndege ambao wanawakilisha peponi.
    [*]Umbo lao lingine ni la Simba.
    [*]Umbo lao lingine ni la Jogoo.
    [*]Umbo lao lingine ni la Nguo ya Dhahabu isiyokuwa na mwili.
  • Umbo lao lingine ni la Fimbo ya Kifalme.
  • Umbo lao lingine la mwisho ambalo kwa kweli ni la kutisha sana; ni lile la Kiumbe ambaye haeleweki eleweki vizuri na ni vigumu kumuelezea ila ana mkia.

5. Majini wa Sayari ya Venus (Zuhura) - Majini wa Ijumaa


Majini wa Sayari ya Venus wana Umbo la kati na ambalo ni zuri kwa kuliangalia ambapo sehemu yao ya juu ni ya dhahabu na sehemu yao ya chini katika mwili ni ya rangi nyeupe au kijani.


Mwendo wao ni kama wa mwendo wa Nyota inayong'aa. Alama yao ni ile inayofanana na Wanawake wanaocheza katikati ya Mduara, huku wakimshawishi na kumtamanisha Mwanamazingaombwe ajiunge nao.

{mospagebreak}

Umbo lao maalum ni:-



  • [*]Ni la Mfalme aliyebeba Fimbo ya Kifalme huku akiwa anamwendesha Ngamia.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliye Uchi.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mbuzi Mwanamke.
    [*]Umbo lao lingine ni la Ngamia; ambaye huwakilisha Shetani mbaya aitwae Cazote.
    [*]Umbo lao lingine ni la Njiwa.
  • Umbo lao lingine ni la Nguo isiyokuwa na mwili ya rangi Nyeupe au Kijani.
  • Umbo lao lingine ni la Mmea uitwao "Savine".

6. Majini wa Sayari ya Mercury (Attwarid) - Majini wa Jumatano


Majini wa Sayari ya Mercury (Attwarid) mara nyingi hutokea na mwili wa Kati, Baridi, Majimaji, Unyevu nyevu. Kwa ujumla maana yake ni kusema kuwa Majini hawa wa Sayari ya Mercury wanafanana na maumbile ya Mercury (Zebaki).


Muonekano wa Majini hawa ni wa kuridhisha, ni Wachangamfu katika maongezi, wana Umbo la Kibinadamu, na wanaonekana kama Shujaa aliye na silaha.



  • [*]Mwendo wao ni kama wa Mawingu ya rangi ya Fedha. Alama yao ni kuwa wanasababisha Vitisho, Hofu na Woga kwa mwenye kuwaita.
    [*]Umbo lao Maalum ni la Mfalme anaemuendesha Dubu.
    [*]Umbo lao lingine ni la Kijana Mzuri wa Kuvutia.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mwanamke aliyebeba Kijiti cha kukunjia Uzi chenye bonge la uzi.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mbwa.
    [*]Umbo lao lingine ni la Dubu Jike.
    [*]Umbo lao lingine ni la Kunguru; Kunguru hawa hutumwa kwenda kusaidia katika Kazi za Kichawi na Kijini kwa Kuchukua Nguo za Ndani za Watu, Soksi, Vijiko, na vitu vingine vidogo dogo kama hivyo. Ndio maana katika aina nyingi za Ndege, Kunguru mara nyingi ndio huchukua vitu vya ajabu ajabu ambavyo ndege wengine hawawezi kuvichukua.
  • Umbo lao lingine ni la Nguo isiyo na mwili yenye kubadilika badilika rangi.
  • Umbo lao lingine ni la Fimbo, Rungu, Bakora au Gongo dogo.

7. Majini wa Sayari ya Moon (Qamar) - Majini wa Jumatatu


Majini wa Sayari ya Moon – Mwezi (Qamar) wana Maumbo makubwa, Laini, Tulivu na rangi yao ni kama wingu jeusi.

Muenekano wao ni umbo lililotuna, Vichwa vyao vina upara, Macho yao ni Mekundu na yanatoa Majimaji, Meno yao ni kama ya Nguruwe Mwitu.


  • [*]Mwendo wao ni kama Dhoruba kubwa Baharini. Alama yao ni ni Mvua kubwa inayonyesha katika Mduara.
    [*]Umbo lao Maalum ni:-
    [*]Ni la Mtu kama Mfalme anayerusha Mishale huku akiwa anamuendesha Swala Jike.
    [*]Umbo lao lingine ni la Kijana Mdogo wa Kiume.
    [*]Umbo lao lingine ni la Mwindaji wa Kike mwenye Upinde na Mishale.
    [*]Umbo lao lingine ni la Ng'ombe.
    [*]Umbo lao lingine ni la Swala Mdogo.
    [*]Umbo lao lingine ni la Bata.
    [*]Umbo lao lingine ni la Nguo isiyokuwa na Mwili yenye rangi ya Kijani au Fedha.
  • Umbo lao lingine ni la Mshale.
  • Umbo lao lingine ni la Kiumbe mwenye Miguu Mingi mfano wa Tandu.





SERIKALI YA MAJINI
Majini wana Utawala wao ambao ni Majini Wakuu na Majini wa Kawaida wanaopewa Kazi za kufanya na Wakuu wao, Katika Serikali yao kuna Wakuu wa Serikali, Wakuu wa Majeshi, Wakuu wa Mahakama na wengineo wengi.

Utawala katika Serikali yao umegawanyika katika sehemu Kuu mbili (2);


  1. Utawala katika Ulimwengu wa Kijini.
  2. Utawala katika Ulimwengu huu wetu wa Kibinadamu.

Majini Wakuu kabisa wapo Watatu (3) ambao Majina yao ni;



  1. [*]Lucifer.................ambae ndio Mfalme wao (Emperor),
  2. Beelzebuth.......... ambae ni Mtoto wa Mfalme (Prince),
  3. Astaroth ..............ambae ni Mtawala Mkuu wa Majimbo (Grand Duke).

Hawa Watawala Wakuu kabisa watatu, iwapo Binadamu anataka kuwaita na kuwatumia inambidi atumie njia Maalum;


Mtu anayewaita anatakiwa achore alama zao kwa kutumia Damu yake mwenyewe, au anaweza pia kutumia Damu ya Kobe wa Baharini (Kasa) katika kuandikia.

Iwapo atashindwa haya yote basi anaweza pia kuwaita kwa kuchora alama za Majini hao kwenye Kito cha Ruby au

Emarald; kwani vito hivi vinaendana sana na Majini hasa wale wa Ukoo wa Jua, ambao huwa na Busara, wazuri na Marafiki zaidi kuliko aina nyingine ya Majini.


Alama hizi za Majini zinatakiwa zivaliwe na Mtu ambae anataka kuwaita. Ikiwa muitaji ni Mwanamme, anatakiwa aiweke kwenye Mfuko wake wa Kulia na iwapo ni Mwanamke, anatakiwa aiweke katikati ya Matiti yake ikielekea upande wa Kushoto.


Alama hizi zinatakiwa ziandikwe katika siku ya Jumanne saa Kumi na mbili (12) mpaka saa moja asubuhi au saa saba mchana mpaka saa nane kwa majini wote.


Majini hawa watatu wana uwezo wa kufanya mambo yote, na kwa Mtu ambae anawaita hawa anatakiwa aheshimu wale tu ambao watamheshimu kwani Majini hawa Wakuu wanawaheshimu wale tu ambao ni Marafiki wao Wakuu na wa karibu, hivyo mtu anaeamua kuwaita anatakiwa ajihadhari kwa lolote ambalo linaweza kutokea.


Utawala wa hawa umegawanyika baina yao wote kwani kila mmoja ana Wasaidizi wake wakuu Wawili ambao nao huwa wanawatuma Majini wengine kuhusu mambo ambayo Mfalme wao Lucifa ameagiza yafanyike Duniani kote.


Wasaidizi walio chini ya Lucifa ni;

Put Satanachia na
Agaliarept;.............Ambao wanaishi Bara la ULAYA na ASIA.
Wasaidizi walio chini ya Beelzebuth ni;
Tarchimache na
Fleurety...................Ambao wanaishi Bara la AFRIKA.
Wasaidizi walio chini ya Astaroth ni;
Sargatanas na
Nebiros.............Ambao wanaishi Bara la AMERIKA.
{mospagebreak}

Majini katika Serikali yao kulingana na Kazi zao ni kama ifuatavyo;



  1. [*]LUCIFUGE ROFOCALE....ambae ni Waziri Mkuu (Prime Minister)
    [*]SATANACHIA.........ambae ni Amiri Jeshi Mkuu (Commander-in-Chief)
    [*]AGALIAREPT......ambae ni Kamanda wa Majeshi
    [*]FLEURETY.........ambae ni Luteni Jenerali (Lieutenant-General).
  2. SARGATANAS.....ambae ni Brigedia Meja (Brigadier-Major)
  3. NEBIROS....ambae ni Jemedari Mkuu na ni Inspekta Jenerali (Field-Marshal and Inspector-General).

Kama jinsi ilivyoonekana hapa ya kuwa Utawala wao katika Ulimwengu wao wa Kijini umekaa KIJESHI lakini Utawala wao hapa Duniani sio wa Kijeshi kwani;


1. LUCIFUGE ROFOCALE;
ana Mamlaka ambayo amepewa na LUCIFA ya kudhibiti Mali na Hazina zote za hapa Duniani.
Wasaidizi wake ni Baal, Agares na Marbas.

2. SATANACHIA
ana Mamlaka juu ya Wake, Wanawake, na Wasichana wote ambapo ana uwezo wa kuwafanyia kama jinsi atakavyopenda yeye.
Wasaidizi wake ni Pruslas, Aamon na Barbatos.

3. AGALIAREPT

Ana Mamlaka na Uwezo wa kugundua Siri zote zilizopo katika Mabaraza na Mahakama zote hapa Duniani.
Anavumbua Siri za hali ya juu sana.
Anaamuru Kikosi cha Pili cha Majini wasiopungua 3,000).
Wasaidizi wake ni Buer, Gusoyn, na Botis.

4. FLEURETY

Ana Mamlaka na Nguvu za Kufanya Kazi yeyote Usiku na anasababisha mvua ya Mawe katika sehemu yeyote ile itakayoitajika.
Anaongoza na Kudhibiti Jeshi kubwa la Majini.
Wasaidizi wake ni Bathsin (au Bathim), Pursan, na Eligor.

5. SARGATANAS
ana Nguvu na Mamlaka ya;
Kumfanya Mtu yeyote asionekane.
Anasafirisha Mtu yeyote kwenda sehemu yeyote ile.
Kufungua Loki na Kufuli zote Duniani,
Kuonyesha na kuweka wazi mambo yote yanayofanyika ndani ya Nyumba za Watu binafsi.
Anafundisha mbinu zote za Uchungaji wa Wanyama.
Anadhibiti na Kuamuru Vikosi Kadhaa vya Majini wasiopungua 5,000 kwa kila kikosi.
Wasaidizi wake ni Zoray, Valefar na Faraii.
{mospagebreak}

6. NEBIROS
ana uwezo wa;

Kushurutisha Uovu kwa Mtu yeyote amtakaye.

Ana uwezo wa Kumletea Mtu Fahari Kuu.

Ana uwezo wa Kumuonyesha Mtu vitu Bora kama vile; Madini, Mawe, Mboga, na Wanyama.

Ana uwezo Mkubwa wa Kutabiri vitu vitakavyotokea hapo baadae; kwani Huyu ndiye Mkuu wa Utabiri katika Ulimwengu wa Kijini.

Anazunguka zunguka huko na huko kila sehemu kwa ajili ya Kuangalia, kuchunguza na Kukagua aina zote za Maangamizi.

Wasaidizi wake ni Ayperos, Naberrs na Glassyalabolas.

Kuna Mamilioni ya Majini wengine ambao nao wapo chini ya hao waliotajwa hapo juu na hutumika tu pale inapoonekana ya kuwa kuna Kazi ya kufanya kutoka kwa Wakuu wao, kwani wao hutumiwa na Wakuu wao kama Wafanyakazi au Watumwa.


Hata hivyo kuna Majini Wasaidizi Muhimu Kumi na Saba (17) ambao wao hufanya Kazi kama Mawaziri wa Wale Majini Wakuu Sita (6), Majini hao pamoja na Kazi zao ni kama ifuatavyo;


1. CLAUNECK;


Ana Nguvu na Mamlaka juu ya Vitu na Utajiri,

Anaweza Kuvumbua Hazina iliyofichwa, kwa yeyote atakayeweka Mkataba nae,
Ana uwezo wa Kumzawadia Mtu Utajiri mkubwa kwani yeye anapendwa sana na Lucifer,
Ana uwezo wa kukuletea Pesa kutoka mbali;
Mtii naye atakutii!

2. MUSISIN;

Ana Nguvu juu ya Mabwana Wakuu, anawapa Maelekezo kuhusu yale yanayotokea na kupitishwa katika Serikali zao na za Washirika wao.

3. BECHARD;

Ana Nguvu na Mamlaka juu ya Upepo, Dhoruba (Tufani), Radi, Umeme, Mvua na Mvua ya Mawe, kwa kutumia uchawi wa Chura na Vitu vingine vya namna hii.

4. FRIMOST

Ana uwezo juu ya Wake na Wanawali na ana uwezo wa kukusaidia kuwafurahia.
5. KHIL ....Husababisha Mtetemeko wa Ardhi.

6. MERSILDE: Ana uwezo wa kukusafirisha mara moja sehemu yeyote uitakayo.


7. CLISTHERET: Ana uwezo wa kukugeuzia usiku na mchana kwa kupenda kwako.

{mospagebreak}

8. SIRCHADE: Ana uwezo wa kukuonyesha wewe aina zote zile za wanyama katika umbo lolote lile walilonalo.


9. SEGAL: Ana uwezo wa kukuonyesha dhahiri miujiza yeyote iwe ya kawaida au ya kimazingaombwe.


10. HIEPATCH: Ana uwezo wa kukuletea mtu aliye mbali papo hapo.


11. HUMOTS: Ana uwezo wa kusafirisha aina zote za vitabu kwa starehe yake.


12. FRUCIESSEIERE: Ana uwezo wa kuwafufua wafu.


13. GULAND: Ana uwezo wa kusababisha aina yote ya maradhi.


14. SURGAT: Ana uwezo wa kufungua aina zote za Loki.


15. MORAIL: Ana uwezo wa kufanya vitu vyote Duniani visionekane.


16. FRUTIMIERE: Ana uwezo wa kukupa kila aina ya sherehe.


17. HUICTIIGARA: Ana uwezo wa kusababisha kutembea usingizini na kwa wengine kuwakosesha usingizi kabisa.


Satanachia na Satanisie wanawatawala majini 45 au 50 wanne katika hao ni Surgutthy, Heramael, Trimasel na

Sustugriel. Wawili wa hawa ni machifu na waliosalia hawana umuhimu wowote.


Hawa ni Majini watumikao kwa binadamu kwa urahisi na haraka lau ikiwa wanaelewana na anaemuita,


Serguthy ana uwezo juu ya wake za watu na wanawali


Heramael anafundisha elimu ya madawa na anatoa na ujuzi kamili wa magonjwa yote, tiba zake sahihi, anafundisha

aina ya mimea yote, sehemu mimea hiyo inapatikana, nyakati nzuri ya kuipata, umuhimu wa mimea hiyo na namna ya kuchanganya mimea hiyo ili kupata dawa sahihi kwa maradhi ya aina yeyote ile.


Trimasel na Sustugriel hawa wawili ni Machifu na wanatoa elimu ya kichawi kwa wale wanaowapenda.


Agalierept na Tarihimal wanamtawala Elelogap, ambae nguvu zake zipo juu ya Maji.


Nebirots Wawili wawatawala Hael na Sergulath.


Hael anatoa maelezo juu ya Usanii wa kuandika kila aina ya Barua, anampa Mtu uwezo wa kuongea mara moja kila

aina ya Lugha na anaelezea na kufumbua vitu vyote vya siri.

Sergulath ana uwezo wa Kufundisha Mtu njia mbalimbali za kuvunja pande ambazo hazielewani.

Hawa wana Wasaidizi wao Wanane (8) wenye nguvu


1. Proculo ambae ana uwezo wa kumpatia Mtu usingizi kwa muda wa masaa manane huku akiwa anafahamu yanayotokea usingizini.


2. Haristum ambae anampa Mtu uwezo wa Kupita kwenye Moto bila ya kuungua.


3. Brulefer, ambae ana uwezo wa Kumfanya Mtu apendwe na Wanawake.


4. Pentagnony, ambae anawapa Watu uwezo wa Kutokuonekana (Invisible), pia anapendwa sana na Watawala Wakuu


5. Aglasis, ana uwezo wa Kumsafirisha Mtu kwenda sehemu yeyote ile Duniani.


6. Sidragrosam, anawafanya Wanawake wacheze Uchi.


7. Minoson, ana uwezo wa Kumhakikishia Mtu kushinda katika Michezo yeyote ukiwepo wa Kamari.


8. Bucon ambae ana Uwezo wa kuanzisha Chuki na Wivu kati ya Jinsia mbili (Wanaume na Wanawake).
 
Ivi mkuu, kunatofauti gani kati ya majini aliyo yazungumzia mwenyezimngu ndani ya Quraan na haya tuambiwayo yanafugwa na watu?
 
552425_466816133371296_1456027839_n.jpg

MAJINI nao hawako nyuma katika masuala ya mapenzi kama ulifikiri vingine shauri yako..................


62229_466804463372463_539519154_n.jpg



598604_466789656707277_281136013_n.jpg


311213_466772880042288_1295111525_n.jpg

Jini Moto huyu...............


148498_466375356748707_204746185_n.png


196128_463451947041048_1608428613_n.jpg


Jini Mbwa huyu Mbwa mweusi anakuwa ni jini.

407725_463023687083874_1624318957_n.jpg
 
Back
Top Bottom