Huu ni ukweli kuhusu samaki aitwaye chunusi

BigBaba

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
1,909
9,038
Tumezoea kumuita chunusi ila kwa jina lingine anaitwa electric eel. Anafanana na kambale. Anatoa umeme aina ya umeme tuli (static electricity) hadi vilt 850v.

Kiwango hicho cha umeme kinatosha vizuri kuua binaadamu na damu kuganda ndio maana utasikia wanasema jini chunusi ananyonya damu.

Ni vigumu kumvua kutokana na maumbile yake na umeme autoao. Wengi hawajawahi kumuona ndiyo maana inabaki kuwa tu ni jini wa kwenye maji.

La Voice muafrica wa kwanza kugundua kuwa chunusi sio jini bali ni electric eel.

Share wapate habari marafiki.

FB_IMG_1578865931543.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo sijui ni samaki ama kitu gani ila yupo mfano wa huyo nilimuona ufukwe wa mbezi aliingia katika wavu wavuvi wote watoka nje ya wavu sasa sikuelewa kwanini kilinuka baharini, wakasema kuna samaki yupo ndani ya nyavu sio ni muuaji yaani huyo akikugusa tu kwanza lazma uzame na ukiibuka ushadedi.

Kingine nilichoshuhudia walifanikiwa kuzivuta zile nyav mpaka ufukweni na nilimuona samaki kama huyo apo, sasa haikupita dakika tatu akaanza kubadilika akawa mweusi kama mkaa ndio jamaa wakasema huyo samaki ana umeme akiwa ndani ya maji na ana sumu mbaya sana kinachombadilisha hapo na kumuua ni sumu yake mwenyewe.

Tangu ile siku nikapunguza kuogelea maji marefu maana nilikuwa na udwanzi fulani sio yaan naenda mbali kiasi mpaka ile minazi ufukweni inanipotea machoni nazuga zuga hukoo kisha narudi mdogo mdogo (kuna samaki flani wanapenda kucheza wanakuja wengi alafu wakikukaribia wanatawanyika kule katika maji mengi yanakuwa kama kioo unaona vizuri tu ndani ya maji, lakini tangu nimuone yule samaki aisee niliingiwa na uoga naogelea kwenye mchanga maji ya ugoko.
 
huyo sijui ni samaki ama kitu gani ila yupo mfano wa huyo nilimuona ufukwe wa mbezi aliingia katika wavu wavuvi wote watoka nje ya wavu sasa sikuelewa kwanini kilinuka baharini, wakasema kuna samaki yupo ndani ya nyavu sio ni muuaji yaani huyo akikugusa tu kwanza lazma uzame na ukiibuka ushadedi.

kingine nilichoshuhudia walifanikiwa kuzivuta zile nyav mpaka ufukweni na nilimuona samaki kama huyo apo, sasa haikupita dakika tatu akaanza kubadilika akawa mweusi kama mkaa ndio jamaa wakasema huyo samaki ana umeme akiwa ndani ya maji na ana sumu mbaya sana kinachombadilisha hapo na kumuua ni sumu yake mwenyewe.

Tangu ile siku nikapunguza kuogelea maji marefu maana nilikuwa na udwanzi fulani sio yaan naenda mbali kiasi mpaka ile minazi ufukweni inanipotea machoni nazuga zuga hukoo kisha narudi mdogo mdogo (kuna samaki flani wanapenda kucheza wanakuja wengi alafu wakikukaribia wanatawanyika kule katika maji mengi yanakuwa kama kioo unaona vizuri tu ndani ya maji, lakini tangu nimuone yule samaki aisee niliingiwa na uoga naogelea kwenye mchanga maji ya ugoko.
Mkuu, hii ni chai. Uogelee kavu mpaka minazi ipotee? Wewe Zanzibar unaenda kwa miguu bila shaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliambiwa ni jini wakati tunaogelea mtoni, kabla hatujaogolea tunarusha mchanga huku tunasema shetani toka Mungu ingia...tunaambiwa msiogelee pale ambapo maji kama yamesimama, chunusi yuko!

Au ajali zikiwa zinatokea sana madarajani fln, walikua wanadai chunusi yuko hapo anataka damu za watu!
 
Tangu ile siku nikapunguza kuogelea maji marefu maana nilikuwa na udwanzi fulani sio yaan naenda mbali kiasi mpaka ile minazi ufukweni inanipotea machoni nazuga zuga hukoo kisha narudi mdogo mdogo
Aisee, unahatari sana wewe, umbali huo ni sawa na km 19 kutoka ufukweni. Kweli ulienda kote huko kwa kuogelea?
(kuna samaki flani wanapenda kucheza wanakuja wengi alafu wakikukaribia wanatawanyika kule katika maji mengi yanakuwa kama kioo unaona vizuri tu ndani ya maji, lakini tangu nimuone yule samaki aisee niliingiwa na uoga naogelea kwenye mchanga maji ya ugoko.
Kuna uwezekano mkubwa hao samaki wadogo waliokuzunguka walikuja kukulinda na hatari ambayo wewe hukuiona.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom