Huu ni mgao wa umeme au mabwawa yamekauka?

GwaB

JF-Expert Member
Mar 19, 2014
3,580
4,638
Dar es salaam hakuna umeme maeneo ya Chanika tangu jana na leo siku nzima hakukuwepo umeme hadi hivi niandikapo.

Je, ni halali Tanesco kupokea pesa kutoka kwa wateja wake halafu wagome kutoa huduma?

Je, kama Kuna matatizo ya kiufundi hivi si busara kuwataarifu wateja wanaotegemea umeme wa Tanesco kuendesha biashara zao juu ya katizo la umeme?

Je, tujipange sasa kutegemea umeme wa gesi kama alivyolisha matango pori na Waziri wa nishati?

Du ... Maswali ni mengi tu, Ila giza totoro kama enzi za ujima wakati Chief Hangaya akiendelea kupinga mwingi.
 
Hawataki kutangaza ila naamini kuna mgao, umeme umekatika tangu asubuhi ndio umerudishwa sasa hivi, kama ni hujuma za makusudi walaaniwe wote wanaofanya huu mchezo wa kihuni, wapo wanaojitafutia riziki zao kwa kutumia umeme wanapowakatia bila taarifa siku nzima wanataka wakale wapi?
 
Wanasema hakuna shida ya maji wala umeme ,ukiwa na hela hauwezi kufeel kama kuna mgao wa maji wala umeme.

Umeset Generator Auto Mode kwenye ChangeOverSwitch -Umeme ukikatika Generator inapick load then Una reservoir yenye capacity ya litre elfu 50 sasa sijui kama utafeel migao yao.
 
Arusha giza tororo....
 
Najiuliza matengenezo gani ya usiku maana umeme unakata mpaka usiku.
 
Dar es salaam hakuna umeme maeneo ya Chanika tangu jana na leo siku nzima hakukuwepo umeme hadi hivi niandikapo.

Je, ni halali Tanesco kupokea pesa kutoka kwa wateja wake halafu wagome kutoa huduma?...
 
Wanasema hakuna shida ya maji wala umeme ,ukiwa na hela hauwezi kufeel kama kuna mgao wa maji wala umeme.

Umeset Generator Auto Mode kwenye ChangeOverSwitch -Umeme ukikatika Generator inapick load then Una reservoir yenye capacity ya litre elfu 50 sasa sijui kama utafeel migao yao.
Kweli mambo ni zamu kwa zamu, zama hizi ni zamu ya masikini kuishi kama mashetwani…

Hata hivyo imeandikwa amelaaniwa yule amtegemeae mwanadamu, serikali ikiwemo maana ndio wanadamu wenyewe.
 
Back
Top Bottom