Mgao wa umeme, Ikulu na Bunge wanashiriki?

Girland

JF-Expert Member
Jan 24, 2016
1,826
2,843
JE, UPUNGUFU WA UMEME unaoendelea upo IKULU? je upo BUNGENI? kwamba katika makazi rasmi ya mawaziri umeme unakatwa? Natamani kujua kama nako hali ni kama mtaani.

Jijini Mwanza, nimeshuhudia umeme ukikatika mchana na kurudi jioni saa moja kwa siku tatu mfululizo! Wilayani Magu ni hali hiyohiyo, najiuliza je huko IKULU napo umeme unakatwa??

Tujiulize maswali yafuatayo :
1) KWAMBA TANESCO wameshindwa kukabiliana na upungufu wa umeme nchini?

2) KWAMBA kuna tofauti ipi ya UPUNGUFU WA UMEME na MGAO WA UMEME,au ni lugha ya kutufariji?

3) Je TANESCO wameshindwa nini kuongeza vyanzo mbadala kwenye gridi ya Taifa ili kushugulikia huo upungufu?

4) KWAMBA serikali ya awamu ya Tano iliweza vipi kukabiliana na changamoto hii ya upungufu wa umeme?

5) KWAMBA Kama kila jengo la umma (ghorofa, Viwanja na majengo makubwa) yana jenereta, ili ikitokea hitilafu basi linawashwa mara moja, je TANESCO imefikiria kuhusu wananchi wa kawaida wanaofanya kazi saluni au wanaochomelea vyuma? Au hayawahusu?

6) KWAMBA Serikali haioni miezi sita ni muda mrefu Sana? Kuendelea na changamoto ya umeme?

7) TUKISEMA wizara ya NISHATI haifanyi kazi yake ipasavyo itakuwa sahihi?

8) Je kucheleweshwa kwa mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere kuna uhusiano wowote na "UPUNGUFU WA UMEME " unaoendelea?

Je TANESCO iko tayari kukata umeme IKULU na Bungeni ili wasikie kilio cha wananchi?

Si ajabu umesikia tamko la TANESCO wakisema Hakuna MGAO WA UMEME, badala yake kuna upungufu wa umeme wakiahidi kushughulikia tatizo,haijalishi mtaliita jina lipi lakini tatizo liko dhahiri
 
Back
Top Bottom