Huu ndiyo muda wa kumjadili,'kumsema' na kumkosoa Dr. John Pombe Magufuli

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,068
2,000
Amechukua fomu za kuomba kugombea tena Urais kupitia CCM. Ameingia tena kwenye mchakato wa ndani ya CCM wa kumpata Mgombea wetu na baadaye kupeperusha bendera ya CCM kwa ngazi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, kama atapitishwa.

Huu ndiyo muda muafaka wa kumjadili, kumsema na kumkosoa Dr. Magufuli. Huu ndiyo muda wa kumjadili, kumsema na kumkosoa Mgombea wetu mtarajiwa.

Pamoja na filamu kalikali zilizotapakaa kilamahali nchini kuwa Dr. Magufuli anapendwa na kila Mtanzania, hali huku 'site' iko tofauti. Wapo waliorudishwa nyuma kimaisha kutokana na uongozi wa Rais Magufuli.

Wapo waliosonga mbele na kuneemeka kwenye uchaguzi huu. Wapo waliobaki vilevile na yaleyale waliyokuwa nayo tangu kwa Kikwete. Wapo wanaoufurahia utawala huu na wapo wanaouponda na kuuchukia. Mjadala unaanzia hapo.

Kama mgombea wetu chamani na uchaguzini, tuna haki na wajibu wa kumkosoa na kumjadili. Kwa mema na mabaya. Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya vyema kwenye nidhamu katika utumishi wa umma na ujenzi wa miundombinu. Amefanya pia vyema kwenye sera za kulinda malighafi na maliasili za nchi hii kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.

Hakufanya vyema kwenye masuala ya utawala wa kisheria na demokrasia. Pia, hakufanya vyema kwenye kuhodhi mfuko mkuu wa taifa na yeye kubaki ndiye mtoaji/ mgawaji wa pesa za kinchi pekee.

Nitampima chamani kwa mambo hayo. Nitampima uchaguzi kwa mambo hayo. Kura ni haki yangu, nitaitumia bila kusita.

Membe hakufukuzwa CCM kisheria na kihalali, kwanini asipewe fomu ya Urais?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma
 
Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
4,549
2,000
Tangu ulipobainika kuwa kuwa wewe ni mchumia tumbo posts zake watu wanazidharau sana

Mkuu tujikite kwenye hoja iliyopo mezani. Kumshambulia mtoa mada haiwezi kumsaidia mgombea wetu.

Nikija kwenye mada, naweza kusema Rais amejitahidi kufanya vizuri kwenye ujenzi wa miradi mikubwa kama SGR, mradi mkubwa wa umeme wa mto Rufiji, kupunguza mgao wa umeme kwa kiwango kikubwa, kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto kwenye sekta ya madini, nk.

Mapungufu ni kwenye suala la ajira kwa wahitimu wa vyuo, kuongeza 15% ya makato kwenye bodi ya mikopo, kushindwa kuboresha maisha ya wafanyakazi tangu alipoingia madarakani, kupenda sana kusifiwa na kutukuzwa, kuudhoofisha mzunguko wa pesa mtaani, kuminya demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, nk.
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,666
2,000
Amechukua fomu za kuomba kugombea tena Urais kupitia CCM. Ameingia tena kwenye mchakato wa ndani ya CCM wa kumpata mgombea wetu na baadaye kupeperusha bendera ya CCM kwa ngazi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, kama atapitishwa.

Huu ndiyo muda muafaka wa kumjadili, kumsema na kumkosoa Dr. Magufuli. Huu ndiyo muda wa kumjadili, kumsema na kumkosoa mgombea wetu mtarajiwa.

Pamoja na filamu kalikali zilizotapakaa kilamahali nchini kuwa Dr. Magufuli anapendwa na kila mtanzania, hali huku 'site' iko tofauti. Wapo waliorudishwa nyuma kimaisha kutokana na uongozi wa Rais Magufuli.

Wapo waliosonga mbele na kuneemeka kwenye uchaguzi huu. Wapo waliobaki vilevile na yaleyale waliyokuwa nayo tangu kwa Kikwete. Wapo wanaoufurahia utawala huu na wapo wanaouponda na kuuchukia. Mjadala unaanzia hapo.

Kama mgombea wetu chamani na uchaguzini, tuna haki na wajibu wa kumkosoa na kumjadili. Kwa mema na mabaya. Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya vyema kwenye nidhamu katika utumishi wa umma na ujenzi wa miundombinu. Amefanya pia vyema kwenye sera za kulinda malighafi na maliasili za nchi hii kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.

Hakufanya vyema kwenye masuala ya utawala wa kisheria na demokrasia. Pia, hakufanya vyema kwenye kuhodhi mfuko mkuu wa taifa na yeye kubaki ndiye mtoaji/mgawaji wa pesa za kinchi pekee.

Nitampima chamani kwa mambo hayo. Nitampima uchaguzi kwa mambo hayo. Kura ni haki yangu, nitaitumia bila kusita.

Membe hakufukuzwa CCM kisheria na kihalali, kwanini asipewe fomu ya Urais?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma
Mzee VUTA-NKUVUTE hiyo miundombinu aliyofanya vyema imejengwa kwenye ardhi ya Tanzania?juzi nimeuliza hapa njamvini mtu anisaidie kutaja angalau barabara moja aliyojenga Magufuli from the word go yenye kilometer 100 sikutajiwa badala yake nikaambiwa nikasome hutuba,je hiyo miundombinu imejengwe kwenye hutuba? Kuhusu raslimali zaidi ya maigizo na mehemko na kutunga sheria zinazojichanganya Kuna Nini Cha maana kimefanyika huko?
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,666
2,000
Mkuu tujikite kwenye hoja iliyopo mezani. Kumshambulia mtoa mada haiwezi kumsaidia mgombea wetu.

Nikija kwenye mada, naweza kusema Rais amejitahidi kufanya vizuri kwenye ujenzi wa miradi mikubwa kama SGR, mradi mkubwa wa umeme wa mto Rufiji, kupunguza mgao wa umeme kwa kiwango kikubwa, kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto kwenye sekta ya madini, nk.

Mapungufu ni kwenye suala la ajira kwa wahitimu wa vyuo, kuongeza 15% ya makato kwenye bodi ya mikopo, kushindwa kuboresha maisha ya wafanyakazi tangu alipoingia madarakani, kupenda sana kusifiwa na kutukuzwa, kuudhoofisha mzunguko wa pesa mtaani, kuminya demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, nk.
Hivi hiyo reli ya SGR iliyojengwa na magufuli ipo hii nchi ya Tanzania? Umefika wapi sasa after 5 good years?
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
34,460
2,000
Amechukua fomu za kuomba kugombea tena Urais kupitia CCM. Ameingia tena kwenye mchakato wa ndani ya CCM wa kumpata mgombea wetu na baadaye kupeperusha bendera ya CCM kwa ngazi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, kama atapitishwa.

Huu ndiyo muda muafaka wa kumjadili, kumsema na kumkosoa Dr. Magufuli. Huu ndiyo muda wa kumjadili, kumsema na kumkosoa mgombea wetu mtarajiwa.

Pamoja na filamu kalikali zilizotapakaa kilamahali nchini kuwa Dr. Magufuli anapendwa na kila mtanzania, hali huku 'site' iko tofauti. Wapo waliorudishwa nyuma kimaisha kutokana na uongozi wa Rais Magufuli.

Wapo waliosonga mbele na kuneemeka kwenye uchaguzi huu. Wapo waliobaki vilevile na yaleyale waliyokuwa nayo tangu kwa Kikwete. Wapo wanaoufurahia utawala huu na wapo wanaouponda na kuuchukia. Mjadala unaanzia hapo.

Kama mgombea wetu chamani na uchaguzini, tuna haki na wajibu wa kumkosoa na kumjadili. Kwa mema na mabaya. Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya vyema kwenye nidhamu katika utumishi wa umma na ujenzi wa miundombinu. Amefanya pia vyema kwenye sera za kulinda malighafi na maliasili za nchi hii kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.

Hakufanya vyema kwenye masuala ya utawala wa kisheria na demokrasia. Pia, hakufanya vyema kwenye kuhodhi mfuko mkuu wa taifa na yeye kubaki ndiye mtoaji/mgawaji wa pesa za kinchi pekee.

Nitampima chamani kwa mambo hayo. Nitampima uchaguzi kwa mambo hayo. Kura ni haki yangu, nitaitumia bila kusita.

Membe hakufukuzwa CCM kisheria na kihalali, kwanini asipewe fomu ya Urais?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma

Hakuna mahali popote pale unaweza kumjadili huyo mwenyekiti wenu kwa uwazi nje ya mitandao, hasa utakopajadili sehemu negative kuhusu yeye, na serikali yake. Ukithubutu kumjadili nje ya mitandao, tena kwa fake I'd, jiandae kuwa shakani, maana lile kundi la watu wasiojulikana bado halijafunga operation zake hapa nchini.
 
NTWA MWIKEMO

JF-Expert Member
Oct 7, 2014
734
500
Maadama hakuna uwazi awamu hii,nakushauri usiamini kwa asilimia 100 kuwa amelinda maliasili za nchi hii.

Kuhusu utumishi wa umma,hakuna nidhamu yoyote iliyojengwa zaidi ya watu kujaa hofu(nidhamu ya woga).
Nidhamu ya uoga ni ipi na ya kweli ni Ipi. Au unataka watumishi wawe wanakula Faru John muda wa kazi
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
4,314
2,000
Mgombea wako na nani ? Acha kujioendekeza kwangu sikujui
Mkuu tujikite kwenye hoja iliyopo mezani. Kumshambulia mtoa mada haiwezi kumsaidia mgombea wetu.

Nikija kwenye mada, naweza kusema Rais amejitahidi kufanya vizuri kwenye ujenzi wa miradi mikubwa kama SGR, mradi mkubwa wa umeme wa mto Rufiji, kupunguza mgao wa umeme kwa kiwango kikubwa, kuzifanyia kazi baadhi ya changamoto kwenye sekta ya madini, nk.

Mapungufu ni kwenye suala la ajira kwa wahitimu wa vyuo, kuongeza 15% ya makato kwenye bodi ya mikopo, kushindwa kuboresha maisha ya wafanyakazi tangu alipoingia madarakani, kupenda sana kusifiwa na kutukuzwa, kuudhoofisha mzunguko wa pesa mtaani, kuminya demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari, nk.
 
Hercule Poirot

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
1,507
2,000
Mnapoteza muda kumjadili, fomu ni moja itapitishwa iwe kwa jembe au nyundo.

Tutamkata vipi wakati yeye ndiye pekee, tukimkata maana yake hatuna mgombea uchaguzini.

Basi, lililopo ni kumpitisha kwa kishindo akatushindilie maendeleo
 
Sijijui

JF-Expert Member
Jan 14, 2018
7,666
2,000
Na yenyewe imefikia sijui 38% vile! Ufupi na kwenyewe anasuasua tu. Tambo ndiyo nyingi kuliko uhalisia
Hiyo asilimia 38 ni ya Dar Isaka au hiki kipande Cha Dar moro ambapo eneo kubwa kilichofanyika ni kusafisha njia tu ya reli?
 
Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
148,164
2,000
Tangu ulipobainika kuwa kuwa wewe ni mchumia tumbo posts zake watu wanazidharau sana
Hapa umewasema watu wawili tofauti.. Mtoa mada na huyo kwenye mada.. Automatically mtoa mada ndio ulimaanisha kwenye sentence ya kwanza na sentence ya pili ikaenda kwa mjadiliwa.. Unaweza kusema ni typing error lakini kiroho ndio uhalisia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom