VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,800
Amechukua fomu za kuomba kugombea tena Urais kupitia CCM. Ameingia tena kwenye mchakato wa ndani ya CCM wa kumpata Mgombea wetu na baadaye kupeperusha bendera ya CCM kwa ngazi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba, kama atapitishwa.
Huu ndiyo muda muafaka wa kumjadili, kumsema na kumkosoa Dr. Magufuli. Huu ndiyo muda wa kumjadili, kumsema na kumkosoa Mgombea wetu mtarajiwa.
Pamoja na filamu kalikali zilizotapakaa kilamahali nchini kuwa Dr. Magufuli anapendwa na kila Mtanzania, hali huku 'site' iko tofauti. Wapo waliorudishwa nyuma kimaisha kutokana na uongozi wa Rais Magufuli.
Wapo waliosonga mbele na kuneemeka kwenye uchaguzi huu. Wapo waliobaki vilevile na yaleyale waliyokuwa nayo tangu kwa Kikwete. Wapo wanaoufurahia utawala huu na wapo wanaouponda na kuuchukia. Mjadala unaanzia hapo.
Kama mgombea wetu chamani na uchaguzini, tuna haki na wajibu wa kumkosoa na kumjadili. Kwa mema na mabaya. Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya vyema kwenye nidhamu katika utumishi wa umma na ujenzi wa miundombinu. Amefanya pia vyema kwenye sera za kulinda malighafi na maliasili za nchi hii kwa ajili ya manufaa ya nchi yetu.
Hakufanya vyema kwenye masuala ya utawala wa kisheria na demokrasia. Pia, hakufanya vyema kwenye kuhodhi mfuko mkuu wa taifa na yeye kubaki ndiye mtoaji/ mgawaji wa pesa za kinchi pekee.
Nitampima chamani kwa mambo hayo. Nitampima uchaguzi kwa mambo hayo. Kura ni haki yangu, nitaitumia bila kusita.
Membe hakufukuzwa CCM kisheria na kihalali, kwanini asipewe fomu ya Urais?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dodoma