Huu ndio ushauri pekee aliopewa Mkapa na Mwalimu Nyerere alipokuwa akiunda serikali yake 1995

Mzalendo Uchwara

JF-Expert Member
Jan 26, 2020
3,716
11,704
Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.

Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.

Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"

Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."

Hizi zilikuwa ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
 
Sikuuliza hilo la ushauri kuwa 'valid' lini au bado uko 'valid' leo. Tafadhali nielewe.
Matumaini yapo, nafasi ya kurekebisha makosa ya 2015 ipo. Wahusika wanapaswa kuwa na ujasiri na kujitoa kwa maslahi ya nchi.
 
Kabla ya kuchukua fomu ya kugombea urais wa JMT, Ben Mkapa aliamua kwenda kumuomba ushauri/ridhaa Mwalimu Nyerere kwa kumwandikia ujumbe na kuutuma butiama, lakini pia baadae Mkapa alipokutana na Mwalimu kwenye vikao vya chama Dodoma alipata wasaa mzuri wa kumweleza kwanini ameamua kugombea.

Mwalimu alimwelewa Ben na kumpa ushirikiano wa kutosha, baada ya kupata ushindi na kuapishwa kuwa rais wa awamu ya tatu 23/11/1995, mzee Mkapa aliona ni busara aonane na Mwalimu ili apate kumshukuru na pengine apante nafasi ya kushauriwa mawili matatu na mwalimu.

Walipoonana Mwalimu alimpongeza Ben kwa ushindi wake, kisha baada ya hapo Ben akamshukuru Mwalimu na akamuuliza, "Mwalimu unaushauri wowote juu ya nani awepo na nani asiwepo kwenye baraza langu la mawaziri?"

Mwalimu alimjibu hivi, "Ben, hili ni baraza lako, sio langu. Serikali yako sio yangu. Kwahiyo nenda ukaiunde. Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni huu, kwanza, lazima ukumbuke kuwa nchi yetu ina jamii/makabila mengi, kwahiyo hauwezi kulipuuzia hili moja kwa moja, lazima ujaribu kutengeneza uwiano. Pili, pia tuna dini mbalimbali, tunazo dini kubwa mbili, hauwezi kupuuzia huo ukweli. Mbali na hayo, ni serikali yako, baraza lako, nenda kaliunde."

Hizi zilikua ni hekima na busara za mwalimu mwaka 1995, akijaribu kumwonesha njia sahihi kijana wake. Ni matumaini yangu kuwa kila atakayepata nafasi ya kukalia kiti kilichowahi kukaliwa na Mwalimu ataiona thamani ya ushauri huu.
Sawa tumeelewa

Its not over until its over...
 
CCM wahuni
Mkapa na Kikwete walikua kwenye njia sahihi kwenye mabadiliko ya kuhama toka nchi ya chama kimoja kwenda nchi ya vyama vingi.

Kilele cha mageuzi haya kilipaswa kuwa katiba mpya kabla ya 2015, sijui JK alipatwa na uoga gani akaingia mitini.

Kwasasa tumerudi tena miaka ishirini nyuma, chama kimeshika hatamu. Baada ya uchaguzi mwaka huu nchi inaweza kupoteza uelekeo mazima.

Labda kama wazalendo wataacha uoga.
 
Kwenye kundi la wazalendo wewe haupo? au wewe ni muoga
 
Kwenye viapo vya wazalendo, pamoja na mambo mengine hua kuna kipengele cha 'kuilinda na kuihifadhi katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania', mimi nimerudia kukisoma kiapo changu hapa sioni hicho kipengele.
Nadhani mimi ni raia mwema tu.
 
Au upo kundi la wavaa barakoa sehemu ambapo Rais hayupo? na akiwepo na asipovaa barakoa wote hamvai?
 
Back
Top Bottom