Baada ya kugraduate nilipata kazi kwenye kampuni inayomilikiwa na mtu mmoja tunayefahamiana naye, yule baba ni ana roho nzuri jamani...ilikuwa nakaa kwa mtu ambapo ni mbali hadi kufika kazini napanda gari tatu, yule boss akawa ananisaidia ananipeleka hadi sehemu ambapo linakuwa limebaki gari moja, siku asipokuwa na nafasi anamtuma mtu hapo nauli nimepewa. Baadae akaniambia nitafute chumba akanilipia kodi ya miezi sita. Watu wengine wasiomjua wakasema haiwezekani K huyu boss wako anakutaka ila yeye wala hakuwa na hiyo habari hiyo tulikuwa tunaheshimiana kama dada na kaka