niah inawezekana ukawa unajua ukweli wa siasa za bongo ila ukaamua kuegemea upande fulani. Suala si chama kilichokufa chadema au CUF au ACT au NCCR, suala lililopo mbele yetu watanzania ni Tanzania kuondokana na umasikini. Wewe jiulize kwanza kabla ya Simba Trust, wapinzani wanaopinga chama tawala cha CCM kuwa madarakani wanalipi ktk kuchangia maendeleo ya nchi?? Je unalielewa kiundani suala la Escrow? Je nani yupo nyuma ya pazia ya EPA, IPTL? Je ni njia gani zinafaa kuchukuliwa ili kuondokana na rushwa, uzembe kazini? Je ni njia gani inafaa kufutwa ili kuboresha elimu yetu? Mimi na wewe inawezekana maisha yetu yapo murua (kie elimu pia na kikipato), je walioko vijijini na wasiokuwa na elimu ni nani anawatetea? Je chama mfu chadema wanawatetea au? Kwa sasa ni CCM na Dkt Magufuli tu ndiyo wanasema rushwa mwiko, uzembe mwiko, wanyonge na masikini lazima wapate haki yao. Kama upo Dar ile barabara ya Mwenge kila mtu anakubali kuwa ulikuwa uamuzi sahihi, lakini watu kama wewe mnajaribu kupotosha umma kuwa rais hafanyi kazi.
Tumuache Dkt Magufuli afanye kazi, kila jambo lina muda wake. Yeye ndiye amri jeshi mkuu, anajua kila kitu.