Huu mchezo unaitwa 'mzungukeni'. Kupunguza PAYE na kuongeza VAT

Mkuu umeamka na wazo langu yaani nilikua nawaza leo niandike uzi kama huu ila sio mbaya umenirahisishia.Wale walioshangilia kupunguzwa kwa PAYE nadhani sasa wataelewa ule msemo wa JK kuwa ukitaka kula lazima na wewe uliwe .
Hizi kodi walizotulimbikia wafanyakazi zinaumiza sana sijui hao ambao tukisema tuandamane watupiga mabomu wao huwa haziwakuti hizi gharama.
Ndivyo ilivyo mkuu
 
Waungwana naamini hamjambo!
Nimejiuliza kuhusu hizi kodi kwenye mabenki nikaona bora nikushirikishe labda unaweza kuwa na ufafanuzi mzuri. Swali langu ni kwamba "Mbona wafanyakazi watalipa kodi mara mbili?" kivipi

Mfanyakazi anakuwa ameishakatwa PAYE kwenye mshahara wake anaowekewa kwenye akaunti yake benki (Hiyo ni kodi ya kwanza)

Anaenda kuchukua hela yake benk analipa tena 18% ya huduma ya kibenki (Kodi ya pili)

Mbona mtu huyu ni kama vile anaonewa? Nasubiri ufafanuzi toka kwa yeyote anayejua zaidi. Ila kwa wale nilioongea nao live hoja yao kubwa ni kwamba hiyo hela ni kidogo. Wanashindwa kujua kwamba hakuna hela kidogo. Tshs. 200 ndo mlinzi wa Tshs 500/= na 500/= ndo mlinzi wa 1000/= hivyo hivyo hadi kufikia laki, milioni, tirion n.k
Mkuu ipo hivyo, serikali ya pombe mtakatifu haina chanzo kingine cha mapato zaidi ya kutoka kwa walevi na wafanyakazi.

Tena walevi wa nchi waheshimiwe wao hawalazimishwi ni kwa hiyari yao wenyewe.
 
Janga lote linalokabili nchi hivi sasa linatokana na Mkuu wa nchi kujiona yeye ndiyo EACH AND EVERYTHING na kulazimisha kumweka mtu 'wake' akalie kigoda pale mjengoni Dom na kumpa maelekezo maalum ya kuwa wabunge wa upinzani ambao ndiyo 'kisemeo' kikuu cha wananchi wadhibitiwe vilivyo Bungeni na kuhakikisha wanakula 'ban' hata pale ambapo labda palistahili tu verbal warning.

Ndiyo hali tunayoanza kuiona nchini baada ya wale wabunge wa CCM walioachiwa Bunge, ambao wao wanaona kila kinacholetwa na serikali ni sawasawa na msahafu na hakipaswi kuhojiwa hata kidogo na kinatakiwa kuungwa mkono kwa asilimia 100!!
Upo sawa mkuu
 
Huu mzunguko tulofanyiwa umefanywa na vilaza wanaopenda namba bila kufahamu hesabu.

Angalau wangeongeza kwanza vat wakati digits za PAYE zikiwa mbili bado, afu baada ya kuongeza vat 18, ndo baadae wangepunguza digits za PAYE

Sasa sijui walizani na sisi watumishi ni vilaza kama wao wamepunguza digits afu wanakuja kuleta vat kabla hata hatujaonja kupungua kwa digits.

POMBE BADO HAJATUFANYIA LOLOTE WAFANYAKAZI NA NAFIKIRI HATATUFANYIA CHOCHOTE HADI ANAONDOKA MADARAKANI, MIMI NISHAONA WEWE YAKO MACHO.
 
Mmakonde Ndiyo alikuwa wa kwanza kutuletea mdudu VAT. Alifuta kodi ya kichwa, Wananchi wakamshangili, akaanzisha VAT. Bila kujua wananchi wakajikuta wanalipa VAT kiasi kikubwa mno kuliko ile kodi ya kichwa.
 
Hili jambo tulikwisha liona muda mrefu kuwa litakuja kumwangukia mwananchi/mfanyakazi wa kawaida na kumrundikia makato yatakayo mwacha akifanya kazi kwa ajili ya kula tu huku akisubiria kufa bila kufanya maendeleo yoyote kwenye hii Ardhi ya tz.Sidhani kama Mh Rais alishauriwa vizuri kwenye hili jambo. Mwisho wa siku hata kama utaamua kuacha kazi ya kuajiriwa na kuamua kujiajiri bado utaendelea kukumbana na hiyo vat ya 18% ya mabenki,manake utakumbana na riba ya mkopo ya 22% na kodi ya vat ya 18% kama kawa.Kwenye hili Mh Rais unatuumiza wananchi wako
 
Back
Top Bottom