Nakuomba Rais Magufuli; Tafuta Fikra Mbadala ili Kujenga Uchumi na Kukuza Biashara kimkakati kama Farao wa Misri katikati ya changamoto ya Covid19 - 2

Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,465
2,859
Habari ya mchana wanabodi.

Kwa ambae hakuweza kusoma part 1, pitia link hii hapa chini.
Nakuomba Rais Magufuli; Tafuta fikra mbadala ili kujenga uchumi na kukuza biashara kimkakati kama Farao wa Misri katikati ya changamoto ya Covid 19 - JamiiForums

Moja ya kazi za viongozi na wasaidizi wa karibu wa viongozi ni kuleta watu wenye mawazo mapya/investment projects mpya ambazo zinatatua matatizo kwa ukubwa wake. Na katika hili, viongozi wana jukumu la kujenga mazingira rafiki ili wawazo mapya, miradi mipya ya uwekezaji Tanzania iweze kutokea kwa watu ambao ni wadau kwa mkutadha huu, Watanzania ni wadau wakubwa hasa wakati huu wa changamoto ya Covid 19; maana hatuna pa kwenda, na Tanzania ndiyo kwetu pa kujihifadhi.

Steve Jobs muasisi wa Kampuni ya Apple, kama mfano wa kiongozi kwenye level yake, si yeye binafsi aliekuja na innovation ya iPod au iTunes au iPhone. Ni watu wa kawaida tu ndani ya kampuni yake ambao walitumia mazingira ambayo Steve Jobs alikiwa kayajenga yeye kama CEO ili waje na mawazo mapya ya kuzalisha products za kuingiza sokoni ili kampuni lipate fedha nyingi zaidi hivyo mara nyingi, Apple kuwa kwenye marketing apex kwa kuuza bidhaa za upekee kabisa hususan soko la Marekani na Ulaya tu. Apple alikusudia niche market yake ni watu wenye high purchasing power. Na alipofanya vile, wenye fedha zao wakamudu nini Apple anauza. In-turn IRS ambayo ni TRA ya Marekani inapata kodi kuoitia mauzo ya various products za Apple. Hoja yangu ni msingi imara ya uongozi wenye vision na ku-assimilate vision kwa kila mtu kwenye kampuni. Shauku yangu hapa nyumbani, innovators hasa wakati huu, watumike vilivyo pasi kutengemea Costech pekee.

Hapa nyumbani kuna fedha nyingi sana na kama zikitumika vema ua government endorsement in term of paper work kama zikitumika vema, sote tutakubaliana na “mkuu wa kaya” anaposema nchi hii ni Tajiri na ndiyo maana kulikuwa na scandal za upigwaji mahali pengi. Nadhani tunakumbuka scandal za kupigwa kama EPA, ESCROW, MEREMETA, Richmond licha ya mikataba mingine iliyowagharimu kama akina kangi.

Tukipima, je fedha hizi kama zingeingizwa kwenye Production, sidhani baadhi ya bidhaa zingendelea kuwa ghali kama ambavyo bidhaa moja ndani ya muda mcheche imetoka sh. 2,500/2,700 na sasa ni zaidi ya 3,000 na kuna mahali ni mpaka 4,500. Nataka niseme hata sasa, kuna Watanzania ambao wana model ya how to end this in mid and long term badala ya kuendelea kuwategemea hawa wa ndani ambao most likely wana create problem ili in the course of solving wanapiga fedha za hatari.

Report ya CAG ya 2017 inaonesha Serikali iliokoa bilioni 268.8 kwa mwaka kama gharama ya uwekezaji ambayo ilikuwa analipwa Symbion mrithi wa Dowans na Richmond.

Mfano mwingine, Ujenzi wa Chuo Kikuu UDOM, moja ya chanzo kinasema iligharimu TZS 5.3Trilioni na chanzo kingine kinasema ilikuwa TZS.3.2Trilion kutoka mifuko ya hifadhi ya jamii. Vyovyoye vile, point hapa ni serikali ilikopa kupitia chanzo cha ndani ili kukidhi mahitaji ya kunjenga miundombinu ya UDOM ili kuongeza udahili wa wanafunzi wanaotoka high school.

Aidha juzi juzi hapa, tumepata mkopo wa watoto wetu ili wapate ilimu bora ya sekondari ambapo kwa miaka 5 itakuwa jumla ya USD 500 mil (sawia na 1.15 Tril kwa exchange rate ya 2300)

Point yangu ni kwamba kuna fedha nyingi sana serikali inakopa kuwekeza kwenye watu wake kupitia Elimu, Afya, Ujenzi wa Miundombinu isipokuwa na baada ya hapo kuna mikakati michache sana ya uwekezaji wa kuwafanya wahusika waweze kulipa.

Nataka niwe mahsusi, kwa Trilion 3.2 za Udom, au Tril 1.15 za watoto wa sekondari, kuna mechanism gani za makusudi ambazo zinawekwa ili hizo fedha baada ya muda zirudi na kwa faida (Return on Investment); Baadhi ya wachumi wanasema sio lazima kujua social projects zitarejea vip.

Isipokua contemporary investment project management specialist wana model mpya ambayo inapimika na yenye kuweka mpango maalum wa kuwekeza kwenye jamii na badae jamii ikafanya kazi ili kurejesha kile walichokitumia wakati wanasoma.

Nataka nije na workable models ambazo 2 zimefanyika Afrika (Ugandana Sudan) na moja Vietnam.

Kama ingechukuliwa say robo ya mkopo wa UDOM kujenga uwekezaji kwenye agro processing (najikita hapo kwenye uchakataji wa mazao ya kilimo kwa maana kuna fedha nyingi sana zinatumika ku-import vitu ambavyo ni consumables na kila siku tunalipia kama sukari, mafuta ya kula, maziwa ya unga kwa watoto, maziwa ya maji, samaki, mbolea na viwatilifu, face mask, surgical cotton, madawa ya mifugo, chakula cha samaki, vitambaa vya nguo ikiwemo uniforms za wanafunzi, wafanyakazi, nguo za watu wa kawaida.

Tuki-quantify hizi consumable kwenye balance sheet, tutagundua exports ni kubwa kuliko imports hata vitu ambavyo tungewekeza fedha ya manunuzi nje ingehamia viwanda ya ndani. Viwanda hivyo vingeajira vijana wetu wa Udom wakiwemo na form 4 drop out kwenye kazi za viwandani, kazi za usafirishaji na kazi na ukulima wa kibiashara au ufugaji wa kibiashara kupita mechanization na matumizi ya technology.

Report ya World bank unaonesha mpaka mwaka 1990, uchumi wa Tanzania ulikuwa na thamani ya USD 4.5 bil wakati huo Vietnam ikiwa na USD 6.5 bil

Taarifa za mwaka jana zaonesha Tanzania mwaka jana ilikuwa na uchumi wa USD 62.2 bil wakati Vietnam ikiwa na USD 261.6 bil

Sababu kubwa ya Vietnam kupiga bao na wanatuzidi takribani USD 200 bil kwa mwaka ni matumizi ya technology kuanzia uzalishaji wa mazao shambani, kuzalisha mbolea na madawa ya kilimo na mifugo ndani kupitia viwanda, kuchakata mazao ya kilimo na mifugo kwa kikidhi mahitaji ya soko la ndani ya kuongeza exports.

Leo Tanzania inanuna nguo containers zinakuwa imported toka Vietnam. Hii ni nchi ambayo miaka ya 80 ndiyo ilitoka vitani. Leo wanapata lots of forex basen on exports. Sasa Watanzania mil 60 kujumlisha kusini mwa jangwa la sahara ni zaidi ya watu mil 400 wote wanavaa nguo. Pamba yetu ni kwanini isiwe processed ndani ili kikidhi mahitaji ya soko hili in the course of production ajira zipatikane na tax base iongezeke. Kuna haja tukawa na fikra mbadala na kuwaamini visionaries who can make that happen.

Nasikitika kwa usanii unaofanywa na baadhi ya wawekezaji toka nje pale ambapo kuna wakati wanatengeneza hujuma kwa kutengeneza upungufu wa bidhaa, na ni wao hao hao wenye vibali vya kuagiza nje. Siku wakianza kuzalisha ndani wanapiga fedha nyingi pasi kujali Watanzania.

Hivyo basi, pamoja na Hazina kuweza kukusanya zaidi ya Tril 1.9 kwa mwezi, kuna haja pia kutoa mikopo ya uwekezaji kwa Watanzania hasa kwenye maeneo ambayo soko lina absorb moja kwa moja products za viwanda vya ndani na kutoa fursa ya kukuza tax base ambapo huenda hazina ikapata cha ziada.

Tunapokuwa kwenye kujiuliza maisha yatakuwaje baada ya Covid 19, ni lazima tusiishiekwenye kujisifu based on collection ya tulichopata mwaka jana au kwa miaka 5 au 10 iliyopita. Let focus and create possibilities ili ongezeko la tax ambalo litapanua wingi wa pato la serikali uendane sambamba na ajira katika sekta ya utumishi kwa maana uwezo wa kulipa mishahara upo kwa kuwa kuna wingi wa kodi.

Kuna tafiti moja ya udadisi ilifanyika kwenye kampuni la Colgate baada ya kuonekana ila aina 32 za dawa ya meno. Utafiti huo uligundua Colgate wamekubatia kuibuka kwa mawazo mapya kila siku ambayo yanalenga kampuni yao izalishe vyanzo vipya vya mapato.

Wapo Watanzania ambao wanaweza kushirikiana na serikali hata wakati huu ili serikali iwe na vyanzo vipya vya mapato ambayo ni

Mauzo ya bidhaa za viwanda serikali ina-charge 18%
Manunuzi ya viwanda ya bidhaa na huduma serikali inacharge 18%
Wafanyakazi wanalipa PAYE
Wafanyakazi na muajiri wanachangia 20% ya kiwango cha mshahara kwenda NSSF
Kuna wafanyakazi kulipia bima ya Afya

Kiwanda kitanunua umeme na maji na vyote hivi viko subject to VAT, EWURA, REA
Kampuni litalipa 30% corporate tax baada ya kuondoa gharama za uwekezaji
Mikopo ya wafanyakazi kutoka mabenki ya biashara
Kukua kwa soko la huduma za consultancy ikiwamo HR, sharia, logistics, ujenzi n.k
Fikiria kama kiwanda kita export, how many USD will be earned in term of forex.

Nasikitika hata wabunge watu, basics kama hizi hawaziongei kwenye nyumba ya kutunga sheria maana haya yakifanyika, ripple effect yake inashuka kwa Watanzania wengi sana.

It’s high time as nationals, to trust those who share our values and beliefs. When we believe someone has our best interest in mind because it is in their benefit to do so, the general public will benefits.

Foreign Direct Investment zina sehemu yake, ila kwa sasa kuna haja ya kuwategemea watu wetu ambao wana fikra mbadala kwenye changamoto za ndani.

Abraham Lincoln anasema, the best way to predict the future is to create it. On my view,the best way to predict more collection in government revenues, it to be create avenues ambapo Wizara za fedha/Viwanda & Biashara/Afya/Kilimo/Mifugo/Vijana/Elimu waje na new strategies on how we create short term investment projects ambazo zenye capacity ya kuzalisha qualitative and quantitative products competitive kwenye soko letu na la nje ya Tanzania.

Worldbank na IMF hawakuwa mkombozi hata siku moja. Juzijuzi hapa tumeona baadhi wa weusi wakibaguliwa Uchina. We need just new brain and new way of thinking ili tuwekeze. Inawezekana.

Kuna fedha chungu mzima toka ndani nahata nje ikiwemo AFDB yenye mkakati maalum kukuza ajira hasa kwa vijana. Vijana ni nguvu kazi na tusipuuze uwepo wao baada ya kugharamia fedha nyingi za elimu kuanzia darasa la kwanza mpaka sekondari na ikiwamo mikopo ya vyuo vikuu. Wakati wa kupambana ni sasa.

Nawatakiwa siku njema tukisimama na Rais JPM ambae ni CiC wakati tunapambana na Covid 19 kama sehemu ya maadui watatu, maradhi, ujinga na umasikini. Wiston Churchill Waziri Mkuu wa Uingereza wakati London inakaribia kuvamiwa na Hitler, alisimama na wanajeshi wake kumdhibiti na hatimaye alishinda.

Tuendelee kuvipigana vita vizuri vya kunjenga uchumi wetu kwa new economic strategic intelligence tools.

Fred
 
Ukishakuwa na hulka ya ubabe ni ngumu sana watu kukushauri hata kama ushauri walionao utakuwa na manufaa.

Hii ni kwasababu wanaogopa kutoa ushauri waonekane wajinga wasiojua, vilevile, wanajua hata wakitoa ushauri wao hautafanyiwa kazi, kwasababu "boss" anaonekana kujua kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungemshauri awe mstari wa mbele kwenye kupambana na corona sio kujifungia chato,. Asifanye maamuzi ya kisiasa bali awaruhusu wataalam wa afya watoe mapendekezo kisha yafuatwe 100%.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAPATA SHAKA KUCHELEA KUSEMA KWAMBA ALIEANDIKA UZI HUU NI ZITTO ZUBERI KABWE
Don't judge a book by it's cover.
ZZK in term of content na mtiririko wake humu JF ni mashariki na magharibi na kila ambacho huwa naandika.

Nadhani ungesoma mpaka mwisho, usingekuja na hitimisho la haraka kuninasibisha na ZZK
 
Ukishakuwa na hulka ya ubabe ni ngumu sana watu kukushauri hata kama ushauri walionao utakuwa na manufaa.

Hii ni kwasababu wanaogopa kutoa ushauri waonekane wajinga wasiojua, vilevile, wanajua hata wakitoa ushauri wao hautafanyiwa kazi, kwasababu "boss" anaonekana kujua kila kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa wale tunaoamini Mungu yupo, na Mungu anajua yote na ana nguvu zote, ila kuna sehemu kwenye maandiko anasema, ..."come and let us reason together"

Kwa kuwa Mungu mwenye nguvu ambae JPM wakati anakula kiapo alisema Ee Mungu nisaidie anaweza kushauriana/reasoning together na wanadamu ambao baadhi yao wana madhambi, bila shaka JPM anashaurika.

Na hasa kipindi kama hiki ambacho ni lazima tuvuke mapambano dhidi ya Covid 19 na maisha ya Tanzania ya kesho yawe bora, kuna haja ya kuwa na fikra mbadala ili kwa hizo new investment projects kama zitafanikiwa, everyone will win ikijumuisha JPM as Commander in Chief katika mapambano yakiwemo dhidi ya umasikini, maradhi na ujinga.
 
Kwa wale tunaoamini Mungu yupo, na Mungu anajua yote na ana nguvu zote, ila kuna sehemu kwenye maandiko anasema, ..."come and let us reason together"

Kwa kuwa Mungu mwenye nguvu ambae JPM wakati anakula kiapo alisema Ee Mungu nisaidie anaweza kushauriana/reasoning together na wanadamu ambao baadhi yao wana madhambi, bila shaka JPM anashaurika.

Na hasa kipindi kama hiki ambacho ni lazima tuvuke mapambano dhidi ya Covid 19 na maisha ya Tanzania ya kesho yawe bora, kuna haja ya kuwa na fikra mbadala ili kwa hizo new investment projects kama zitafanikiwa, everyone will win ikijumuisha JPM as Commander in Chief katika mapambano yakiwemo dhidi ya umasikini, maradhi na ujinga.
Kuapa kwa kutumia vitabu ile ni kutimiza wajibu tu, mbona huapa kwa vitabu mwishowe wanakula rushwa, wanageuka mafisadi n.k.

Una wazo zuri, ila tabia ya huyo jamaa unaemshauri ndio tatizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwa hiyo miradi mikubwa kama SGR, ununuzi wa ndege, Stigler Gauge, Ujenzi Wa Barabara, kwako haina faida
 
kwa hiyo miradi mikubwa kama SGR, ununuzi wa ndege, Stigler Gauge, Ujenzi Wa Barabara, kwako haina faida
I supportive kwa hizo initiatives za JPM 100% na ntatoa mfano wa SGR kwa uchache tu hapa chini.

SGR is such a strategic project. Inatumia cement ya ndani kwa kiasi kikubwa na ikikamilika ita cut down gharama kubwa sana ya kusafirisha iwe ni imports au exports. Uwepo wa viwanda vya ndani hasa kwenye agro processing utatifanya tuwe na trade surplus kupitia SGR unlike Kenya ambao wao kwa sasa SGR yao ina trade deficit.

Kwa lugha rahisi badala ya SGR kusafirisha say pamba, katani au ngozi. Basi SGR isafirishe vitambaa au ikiwezekana nguo, viatu, mikanda, kahawa iliyosindikwa ili tuwe na exports zaidi ku-earn forex.

Pitia graph hii hapa chini utaona uchumi wa China umeanza kuwa na nguvu baada ya exports kuwa kubwa na trade surplus kuwa realized.
 
kwa hiyo miradi mikubwa kama SGR, ununuzi wa ndege, Stigler Gauge, Ujenzi Wa Barabara, kwako haina faida
Jana waziri wa fedha wa afrika kusini kawaambia SAUTH AFRICAN AIRWAYS wafunge kampuni .wanataka ruzuku ya 10 billion rand .wana ndege 70 .kati ya hizo 15 Ni air bus Kama yakwenu. KWANINI MKAGUZI WA SERIKARI HAJATOA TAARIFA YA AIR TANZANIA
 
Jana waziri wa fedha wa afrika kusini kawaambia SAUTH AFRICAN AIRWAYS wafunge kampuni .wanataka ruzuku ya 10 billion rand .wana ndege 70 .kati ya hizo 15 Ni air bus Kama yakwenu. KWANINI MKAGUZI WA SERIKARI HAJATOA TAARIFA YA AIR TANZANIA
Masuala ya ukaguzi tuyape mjadala wa siku nyingine.
Ila nataka nije kwenye ndege kama strategic carrier na kwanini ATC ni lazima i-connect uchumi wake na kilimo biashara kwa mfano, nasisitiza kilimo maana mashamba yapo na maji yapo ila tunahitaji kununua technology na know how ili kuongeza production itakayofanya tuwe consistent kufanya exports kwenye soko.
Gharama za kununua technology ni kubwa ndio, ila mrejesho kwenye uwekezaji uko promising na faida yake ni kubwa kuliko kuendelea na kilimo cha kujikimu ambacho hakina tija na ufanisi hasa tukifikiria international markets.

2017, Israel iliuza maua milioni 60 kwa siku moja tu ya Valentine Ulaya. Imagine kama kila ua lilingiza EURO 5 tu kwenye uchumi wa Israel. Maana yake hizi ni sawa na Bil 750 ziliingia kwa siku moja kwenye bank za Israel.
Israel exports 60 million flowers to EU for Valentine’s Day

Tanzania tuna ardhi kubwa na hali nzuri ya hewa we only need know how and technology. Sidhani haya yanamhitaji Rais ila kama wasaidizi wake wangefikiria kimkakati, ilitakiwa kujenga mazingira ila Watanzania wafanye.

Mbona Kenya hata kwenye Covid 19 wanatumia fursa za KQ kuuza veges ughaibuni??

KQ takes medical supplies to South Africa as carrier turns to cargo business - Citizentv.co.ke

Well, sio mara ya kwanza kusema. Hata huko nyuma nimewahi kushauri wakati mambo yakiwa shwari.
Tutaendelea kushauri kwa kuonesha wenzetu wanafanyaje ili walau nasi tufikie hatua kufanya bora kuliko wao kwa kuingiza forex kupitia domestic produce ambazo pia zinazalisha kazi kwa vijana Tanzania.

Wachumi wetu Hazina na BOT wanafanya nini kuiokoa shilingi yetu au mpaka Magufuli awape TOR ndipo “waamke” usingizini? - JamiiForums

Wachumi wetu Hazina na BOT wanafanya nini kuiokoa shilingi yetu au mpaka Magufuli awape TOR ndipo “waamke” usingizini? II - JamiiForums

Ni wapi Rais Magufuli yuko sawa lakini wasaidizi wake wanamkwamisha kwa bahati mbaya au kwa kukusudia. - JamiiForums
 
Back
Top Bottom